#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

unataka kuniambia kwamba mwendazake alituongopea kuwa hakukuwa na korona

Asiyejua kuwa mwendazake alituongopea kuwa hakuna Corona na watu hawafi kwa Corona, bila shaka atakuwa pia kaaminishwa chanjo haina sababu na kaamini hivyo.

Bila shaka aliyeamini hivyo angali pia anaamini kwenye nyungu, michai chai, mikaratusi, malimao na matango pori mengine.

Hiiiiii bagosha!
 
Mbowe yupo sahihi ila kwa Tanzania iliyojaa vilaza ataonekana kituko.

Watu wamedanganywa chanjo ni vita ya kiuchumi hivyo wazungu wanataka kutuangamiza.

Makanisani kina Gwajima wanasema chanjo ni alama ya mpinga Kristo 666 hivyo huu ni ujio wa NEW WORLD ORDER.

Na huku ulaya Nani katudanganya. Acha Siasa. Hakuna chanjo ya lazima hasa kwa hizi za corona. Wengi tu hawataki. So sio huko kwenu tu.
 
Uko sahihi, Mbowe ameweka mbele maslahi ya watu wengi, anaamini kwa dhati ili kunusuru uhai wa watu wengi basi wachanjwe
Na Mbowe Mwenyewe kaonyesha mfano kuwa hayuko kimanenomaneno tu yeye keshapokea chanjo tayari

Mbowe angaliweza kuchagua kunyamaza kwa maslahi yake binafsi kisiasa.

Nani asiyejua kuwa pana watu wanaoufanyia siasa ugonjwa huu kwa maslahi yao binafsi bila kujali maisha ya watu?

Kwani haijulikani kuwa vigogo wengi tayari wameshachanjwa na kwa ubinafsi wao ni faida kwao (au haiwahusu) hata kama tukiaminishwa kuwa ugonjwa huu haupo sasa hata kama upo?

Mbowe ni wa kupigiwa mfano.
 
Kama watu wote hawatachanjwa hii chanjo yao itakuwa ni kupoteza muda. Chanzo iwe lazima ili kuokoa maisha ya wengi
 
Kama watu wote hawatachanjwa hii chanjo yao itakuwa ni kupoteza muda. Chanzo iwe lazima ili kuokoa maisha ya wengi

Hamna haja ya kuwalazimisha watu wasioelewa umuhimu wa kuchanjwa kama idadi inayotakiwa inaweza kufikiwa kwa uelewa wa wengine au kwa kuwaelimisha au kuwashawishi tu wasioelewa.

Hata hivyo kama threshold hiyo haiwezi kufikiwa, kujifunza mbinu mbadala tokea kwa ma quarter pin (Kagame na Museveni) ni halali.

Wajinga na wapumbavu wengi au wachache hawawezi kuachiwa ku dictate "fate" za wengine na hasa zihusuzo maisha au vifo.

"Fate" za maisha au vifo ni kwa walio na dhamana wala si vinginevyo.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Uganda na Rwanda hapana kuendekeza ujinga. Huko wala si ukuda bali utachezea kichapo!

Kumbuka ujinga si tusi. Ni suala la kutokuelewa tu. Ujinga dawa yake ni elimu dunia tu mkuu.

Huku kwetu tutabembelezana kwanza, ila baadaye kutakuwa na vikwazo hapa na pale. Mdogo mdogo tutafika tu.

Hiyo ndiyo sayansi ya chanjo.

Asante Mkuu ni kweli najua ni suala la Mda tu chanjo itakua lazima. Tena naamini itakubalika iwe chanjo moja tu.

Ila Mimi Hapana.
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
Pale MACHAGA wanavyorukia hoja ya makengeza Mbowe 🤣🤣

images (2).jpeg
 
Hivi hii nchi mbona watu hawajitambui? eti chanjo ni lazima! kachanje wewe siyo uwaamulie watu afya zao. Eti mbowe kasema yeye ni daktari? anajua nini kuhusu huo ugonjwa? harafu nyie mlikuwa wapi awamu ya 5? maana awamu hii mna kihere2 kweli! lazima muwe na mipaka ya kusema, serikali iwadhibiti maana mmekuwa wajinga kupitiliza sasa!
 
Asante Mkuu ni kweli najua ni suala la Mda tu chanjo itakua lazima. Tena naamini itakubalika iwe chanjo moja tu.

Ila Mimi Hapana.

Inahitaji ujasiri mkubwa kama wako, Mbowe, mimi na yule kuusema ukweli hata kama ni mchungu kama huu:

"Asante Mkuu ni kweli najua ni suala la Mda tu chanjo itakua lazima. Tena naamini itakubalika iwe chanjo moja tu."

Heshima kwako mkuu.

Hata hivyo kuwa na amani. Safari itakuwa hivi:

1. Wapo wanaouelewa muhimu wa chanjo. Wanaisubiri na kwa hakika, kwao imechelewa mno. Hao pia si wachache.
2. Wapo watakao elewa kirahisi kwenye elimu na uhamasishaji. Hasa hasa Mama Samia, Kabudi, Mbowe, Lissu, Jaffo, Msukuma, Kibajaji, Kishimba, Gwajima, na binamu zao watakapochukua jukwaa moja kuhamasisha.
3. Wapo watakao shawishika kirahisi ili kusafiri, fursa, nk

Inshallah, kwa hao tu threshold itakuwa imefikiwa na kiboko kitakuwa kimekuepuka wewe kama wewe.

Yote kheri, Mungu ni mwema. Tena ni mwema sana.

Niweke wazi: "Mimi na nyumba yangu tutachanjwa mwanzoni tu."
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
Mawazo ya hovyo sana kusema chanjo iwe ya lazima katika hili mbowe amefail kabisa chanjwa wewe na familia yako tu ya watu wengine yaache waamue wenyewe wala halihitaji kampeni
 
Mbowe aache upumbavu, ni ujinga kama nchi kuanza kuangaika na vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.
 
Yego Masika. Wasiba Mo?

Uliuona utambulisho mwanzoni lakini?

!! 😂😂😂😂😂😂😂 !!

Hii siyo zile ngoma mlizozowea kule Ukara zisizokesha.

Hiiiiii bagosha!
Mimi ni Mzanaki zungumza kizanaki nikuelewe. Usiruke ruke kama umepakwa pili pili huko chuma.

images (1).jpeg
 
Mawazo ya hovyo sana kusema chanjo iwe ya lazima katika hili mbowe amefail kabisa chanjwa wewe na familia yako tu ya watu wengine yaache waamue wenyewe wala halihitaji kampeni

Unayasoma wapi hayo uliyoyaandika jombi? Tulia kunywa maji soma. Elimu haina mwisho:

IMG_20210719_184727_684.jpg

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom