Okay, kumbe tatitizo ni enforcement.Mkuu, katika vitu kama hivi, ambavyo vinaingia kwenye mambo tunayoita public administration, kuna kitu kinaitwa cost of enforcement of directives.
Fikiria, ikiwa tutasema kama konda hajafanyiwa chanjo basi mtu asipande basi lake, kutia ndani daladala nk, utawezaje kuhakikisha hilo linatendeka? - How do you enforce that? Kwa hiyo ni rahisi ku-enforce makonda wachanje kuliko kuratibu watu wasipande basi au daladala lenye konda hajachanjwa.
Suala la matabibu kuchanjwa kwa mfano, ni kwamba hadi unapoenda hospitali, tayari una weakness katika immunity yako. Na watu wenye weakness katika immunity sio tu ni rahisi kuambukizwa Covid-19, bali pia ni rahisi wao kufa wanapoambukizwa. Mtu mwenye weak immunity kutokana na tatizo fulani la kiafya, akiambukizwa Covid-19 huwa mara nyingine atakufa baada ya siku mbili tu. Sasa nesi mmoja tu aliye na Covid-19 ambaye haonyeshi dalili za ugonjwa (asymptomatic) anaweza kuambukiza wodi zima la wagonjwa ambao wamelazwa kwa tatizo nje kabisa ya Covid-19. Ndio maana ni rahisi kudhibiti hilo kwa kumchanja huyu nesi. Au fikiria dokta anapiga round hospitali yote, kumbe ana Covid-19. Kuna siku utasikia waginjwa wote wa hospitali ya Mwananyamala wameambukizwa Covid-19.
Wewe utajisikiaje pale baba yako amelazwa hospitali kwa tatizo la BP, halafu unaambiwa amepata Covid-19 kutoka kwa nesi na sasa hali yake ni mbaya? Kumbuka ukiwa na kitu kama kisukari , ukipata Covid-19 uwezekano wa kufa ni zaidi ya 80%. Sasa utalindaje watu kama hawa wakiwa hospitali, kwa kumwambia nesi ana hiari ya kuchanja au kutochanja?
Natumaini somo limeeleweka.
Miaka 9 yupo peke yake?Basi hiyo kazi yako ya ukonda wa daladala acha utafute kazi nyingine utakayofanyia chumbani kwako na mkeo. Nina kijana wangu hapa ana miaka 9 japo uwezekano ni mdogo, lakini anaweza kuambukizwa Korona na mtu kama wewe
Basi hata wewe unayo...Unajuaje kama huna? Unaleta yale yale ya kuwapima watu HIV kwa macho. Kuwa na Korona sio lazima uumwe na kushindwa kupumua
Acha ujinga we mjinga, kwa hiyo kabla ya corona watu walikuwa hawafi?Inasikitisha sana kuona watu wanavyobisha kwa furaha na kicheko bila kuelewa lolote kuhusu Covid-19.
Tatizo ni kwamba Covid-19 wana mutate kupitia watu ambao hawajachanjwa, kiasi kwamba inafikia wakati msiochanjwa mnawapa uwanja wa Covid-19 ku-mutate hadi wanafikia kuwaambukiza tena wale waliochanjwa kwa kuwa chanjo yao ilikuwa ni kwa Covid-19 ambaye alikuwa haja-mutate.
Kwa hiyo dawa ni watu wote kuchanja ili kutowapa Covid-19 hosts watakaowatumia ku-mutate. Ndio maana mnasikia juu ya South Africa variant, UK variant etc.
Tulipoanza na Covid-19, hatukuwa na Delta variant ya Covid-19. Delta ni Covid-19 ambaye ame-mutate kupitia wajinga ambao hawataki kuchanja. Kama dunia nzima tunhechanja kwa wakati mmoja, tusingekuwa na Covid-19 Delta. Na kadiri watu wanavochelewa ndivyo tutazidi kuwa na mutations zaidi za Covid-19, na kufikia ambapo chanjo zitakuwa hazisaidii tena.
Siku wakifa mama, baba, watoto, dada, kaka zenu, ndio mtajua uchungu wa Covid-19. Kwa sasa chekeni sana.
Kwa nini mnakuwa wabishi bila kusumbua akili zetu kuelewa mambo kwanza?
Very good, yaani vikibadilika wachanjwe Tena .Sasa kama umepata chanjo kwanini una mashaka na mimi ambaye sijachanjwa hali ya mimi siwezi kukuambukiza wewe ambaye hujac
Nyie mnaotaka kuchanjwa endeleeni kwa kadri virusi vinavyo badilika........
Wewe si uende kuchanjwa?Utaki chanjo nenda Burundi, unataka kubaki tanzania lazima uchanje pumbafu msiwe wabishi kila kitu.
Ushindwe na ulegee,Nahisi kuna siku humu tutaona tanzia juu yako wewe kama mwana JF - mwenzetu kafa kwa matatizo ya kupumua. Kwa mtazamo wako huu ni suala la muda tu.
Wanadamu wote njia moja, kwa hiyo wengine watapata chinjo la chanjo..Kwa uzembe na hii mentality, lazima itakuwa wanaendelea na maisha yao kuelekea kufa kwa Korona
Kuna watu tutapata chanjo ya Corona, na wengine mtapata chinjo la Corona
Tutavuka salama. Acha kuogopesha watu na kifo. Kila nafsi itaonja kifo. Jenga hoja tu usitishe watu.Sawa, acha mungu wenu awavushe salama kama alivyomvusha raisi wetu Magufuli. Anza kuimba kabisa mtakutana na Magufuli mtoni.
Kachanjeni na familia zenuUtaki chanjo nenda Burundi, unataka kubaki tanzania lazima uchanje pumbafu msiwe wabishi kila kitu.
Unaogopa kifo π€£π€£Sawa, acha mungu wenu awavushe salama kama alivyomvusha raisi wetu Magufuli. Anza kuimba kabisa mtakutana na Magufuli mtoni.
Unaogopa kifo π€£π€£Sawa, acha mungu wenu awavushe salama kama alivyomvusha raisi wetu Magufuli. Anza kuimba kabisa mtakutana na Magufuli mtoni.
Zilikuwa za majaribio?Mkuu, hivi unajua tangu uzaliwe umeshafanyiwa chanjo ngapi? Na kitu gani kilikufanya uwe na imani na hizo chanjo lakini sio hii ya Korona, hadi kuwapeleka watoto wako wanapozaliwa kuchanjwa?
Kuna watu kama Magufuli kwa mfano, walidai wazungu wanaweza kuwa na ajenda ya siri katika hizi chanjo. Lakini ni chanjo na dawa za wazungu ngapi unaingiza mwilini mwako ambazo wameshindwa kuzitumia kama nia yao ni kukudhuru wewe mswahili? Hivi ni akili kudhani kama wazungu wangetaka kutudhuru watu weusi wangetumia chanjo ya ugonjwa ambayo hata wao unawaua? Huoni kama wangetumia chanjo za tropical diseases ambazo kwao hazipo?
Hiyo yellow card tunayolazimishwa kuwa nayo ikiwa na chanjo za kipindupindu, yellow fever, dengue sijui nk, unafikiri wazungu wanachanja hayo madude? Vidonge vya uzazi wa mpango sijui, mbegu za mahindi nk, kwa nini wasivitumie wakijua athari upande wao zitakuwa kidogo sana kwa sababu hawatumii ugali kama Wasukuma wa Mwanza? Unafikiri mafuta ya kupikia unayotumia sijui Korie wazungu wanatumia hayo?
Vitu vingine unapaswa kutumia akili kidogo tu kuelewa
Anataka tuumie wote πππ, si unajua kifo cha wengi hakiumi πππ, keshachanja huyo πππChomeni mnaotaka msilazimishe wengine
unahofia nini na una chanjo tayari?.
Ndio naogopa, kwa sababu nafurahia maisha vyuma havijakaza kwangu. Kuna watu mmefulia hadi mnaona kufa kwa Korona ni suluhishoUnaogopa kifo π€£π€£