Chanjo ya COVID-19: Hivi wataalam hamjui ukweli au mmeamua kumpotosha Rais?

Hahahahahah.....biology ya form foo tena?
Ndiyo, hiyo biology ya fomu foo mnayofundishwa platelets hazipo kwenye kundi la chembe nyeupe za damu, ukisoma zaidi utapata maarifa kiundani dogo, kwa sasa kalili hivyo hivyo ulivyofundishwa.......
 
Sawa tumekusoma lakini kumbuka Mama aliteua jopo la wataalam kupitia yote hayo na kumshauri nini la kufanya na technology ya mRNA katika Corona vaccine inatumika na vaccines za Pfizer na Moderna ambazo ni chanjo za USA na mpaka sasa watu karibi 70% ambao ni 200 millions kati ya 300 millions ya wamerekani wamepata chanjo ya kwanza.

Kuna chanjo nyingine za Corona ambazo hazitumii
mRNA technology haujacomment lolote kwenye hizo chanjo.

Madhara kwa vaccines ya aina yoyote yapo lakini inaweza kuwa ni margin ndogo sana, katika hao 200 Millions ya wamarekani ni wachache sana ndio wanapata hizo athari.

Sasa ulitaka chanjo zisitumike na ugonjwa uenee na kuzidi kuuwa watu duniani
sababu ya hizo athari kwa watu wachache sana.
Mambo ya wataalam waachie wataalam usituletee over generalization za conclusions zako ambazo hazina utafiti kamili.
 
Tunashukuru kwa kushiriki, ngoja wataalamu hasa waje....
 
Mimi sinaga ubishi wa kijinga.Mimi na familia yangu tutachanja kama tulivyochanja chanjo ya pepo punda na kifaduro na surua

Nyie endeleeni kujifukiza
Kila la heri...
 
Naomba tusisambaze habari ambazo hatujachungulia, Ulaya hawakukataa Covishield (=Astrazeneca kutoka Uhindi). Inaonekana kiwanda cha Uhindi wamesahau hadi sasa kuomba kibali kwa dawa kwa nchi za Ulaya (jinsi ilivyo kwa kila chanjo, ipate kibali cha Mamlaka ya Tiba Ulaya)
Soma hapa:
No Ban On Covishield, Request Must For Approval Process: EU Envoy To India
Asian News International 4 minutes
New Delhi: European Union (EU) Ambassador to India Ugo Astuto has clarified there is no ban in the EU on the Covishield vaccine produced by the Serum Institute of India (SII) and developed by AstraZeneca and Oxford University.
Astuto told ANI in an interview that Pune-based SII has apparently not yet applied to European Medicines Agency (EMA) with a request for approval of the COVID-19 vaccine. Chanzo: No Ban On Covishield, Request Must For Approval Process: EU Envoy To India
Tatizo lilitokea kuhusu chanjo nyingine ambayo ni Covaxin; India waliruhusu kuitumia wakati majaribio hayakumalizika. Hii ilikuwa sababu wataalamu wengi wa kimataifa walikosoa uamuzi huo.
Soma hapa: Moderna, Covovax, Biological E: What we know about India's new Covid vaccines
 
Wewe una uhakika gani kuwa wanachoma kitu kingine na siyo chanjo ya covid? Wewe ndiye unayewacoma Marais wote hizo chanjo feki? Chanjo zimepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Covid huko USA na maeneo mengine Duniani. Acha uongo wa kishamba wewe.
Mbona afrika waliochanjwa ni kidogo sana lakini maambukizi yamepungua sana ukilinganisha na 2020? Kilichopunguza maambukizi ni natural immunity wala siyo chanjo!
 
Mbona afrika waliochanjwa ni kidogo sana lakini maambukizi yamepungua sana ukilinganisha na 2020? Kilichopunguza maambukizi ni natural immunity wala siyo chanjo!
Kumbe umefanya utafiti? Kinachokinga Waafrika hadi sasa ni 1) idadi ndogo ya wazee (maana watoto halafu vijana mara nyingi hawana matatizo makubwa). Halafu 2) tabia ya watu wengi kuishi vijijini na kutosafiri sana. Halafu 3) hali ya watu wengi ambao wanakaa mazingira ambako hewa inapita; wengi hukalia nyumba bila madirisha yenye kioo hivyo hewa inapita.

Habari ya sasa ni ile aina mpya ya virusi, inayoitwa variation "delta". Inaonekana inaambukiza haraka zaidi kuliko aina zilizotangulia. Pia imeonekana inaathiri vijana kuliko zile za awali.
Hii sababu ya onyo.
 
Hali ni tete ndugu zanguni. Watu wanapoteza life, hili gonjwa msilichukulie poa. Tujihadhari, kumbi za harusi, sherehe za aina yoyote tuepukane nayo bandugu. Mkitaka kujua ukweri nendeni hospitalini mukajionee hali inatisha bandugu.
 
Magufuli aliachia sana adi gonjwa likasambaa na wengine kupoteza life. huyu mama anajitahidi kupambana tumpe sapoti bandugu.

Mikusanyiko, maharusi na mashelehe ya aina yoyote kuepukananayo.
 

You must always be willing to truly consider evidence that contradicts your beliefs and admit the possibility that you maybe wrong..


Intelligence isn’t knowing everything it’s the ability to challenge everything you know
 

Kwani mkuu wamekwambia ukichanjwa hautaugua tena Corona...

Ukipata maambukizi utaugua na hio chanjo yako inaweza ikawa tatizo kwako vile vile madhara yapo ya papo kwa papo na mengine ni ya muda mrefu ndio maana nchi zingine wataalamu wameomba zistop kwanza nasisitiza sio Magufuli alioomba chanjo istop kwanza ni wanasayansi wa nchi za ulaya...ila tofauti ni kwamba Magufuli aliwatangulia kusema na wao wakafuata

Takwimu za watu waliopatwa na madhara ya chanjo inasemekana ni nyingi kuliko zinazotangazwa ...
 
Kuzungumzia chanjo bila kunyambulisha chanjo gani ni uvivu, kwa sababu, si chanjo zote ziko sawa.

Leo nilikuwa nasikiliza BBC World Service wanasema Indonesia kuna madaktari wamechanjwa chanjo mbili za Mchina na bado wanaambukizwa Coronavirus na kufa.

Sasa hapo watu wamekuwa specific kutaja chanjo za China, hata kama kuna kuchunguza wanaanza kuchunguza za China.

Sasa chanjo haziwezi kukosa matatizo, huu ugonjwa mpya.

Lakini, chanjo gani? Zina matatizo gani? Hatari ikoje? Hatari ya kuchanjwa na kutochanjwa ipi ni kubwa?

Maana kama kuna chanjo ina nafasi ya kukuua mtu mmoja kwa kila watu laki moja wanaochanjwa, halafu ukipata ugonjwa unakufa kati ya watu 100 watakaougua, na una nafasi kubwa ya kuambukizwa, hapo unaweza kuwa justified kupiga chanjo.

Wewe ukiongelea chanjo hata hujaitaja chanjo gani nakuona unaongea vitu usivyovijua.
 
Ushasema BBC....

Mkuu jiongeze chanjo ni biashara za wenye power they control everything mpaka hizo media..takwimu utazisubiria sana..

Ushaambiwa na baadhi ya wanasayansi madhara yanayotokana na hio chanjo...inatosha
 
Ushasema BBC....

Mkuu jiongeze chanjo ni biashara za wenye power they control everything mpaka hizo media..takwimu utazisubiria sana..

Ushaambiwa na baadhi ya wanasayansi madhara yanayotokana na hio chanjo...inatosha
Sawa. Usichanje. Wanaotaka waache wachanje.

Halafu tuangalie watakaokufa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…