wagonjwa wa;
1.KISUKARI
2.UKIMWI
3.SARATANI
4.MOYO
5.PRESHA
6.TB
tuchukue tahadhari maaana hili wimbi la 3 la delta linapuputisha sana wenye maradhi hayo.
chukua tahadhari piga chanjo

tupo LAMBDA delta ndo inaishia
 
Ni kweli nimewahi kuchanjwa utotoni na pia kumeza Dawa ila tangia mwaka 2018 mpaka leo sijawahi kumeza Dawa Tena Zaidi labda cream za fungus kwenye ngozi.

Kama Ni kufa acha nife ila chanjo sichomwi nachofanya ni kula matikitimaji, matango, kabeji, matembere, ugali, samaki, maboga, maziwa, maji ya kutosha n.k

Na mazoezi ya kutosha japo siku hizi nimekuwa mvivu mwili unakataa kabisa kufanya mazoezi ila ipo siku mwili ukiwa tayari narudi kwenye matizi we ngoja tu nipate raba nzuri nyepesi.

Kwa hivyo tusilazimishane kila mtu abebe msalaba wake na kila mtu afanye biashara na anawaotaka na kuwaamini.

Maisha mbona mazuri tu kila mtu aamini material yake
 
Your browser is not able to display this video.

Ishu ya chanjo ya UVIKO 19 ni very complicated. Ishu hii imeshaligawa taifa. Imegawa wananchi. Imegawa viongozi wa vyama vya siasa na serikali...

Hii ishu kwa 100% haina sura ya program ya kawaida ya serikali...

Sasa ni dhahiri ni ishu ya KIIMANI zaidi...

We all know, kuwa, mambo ya imani siku zote ni very complicated...

Suala la mtu aamini nini, siku zote huwa ni maamuzi ya mtu binafsi...

Imani haina cha kumfuata Rais wala waziri, mama au baba, kaka au dada... Ni suala la maamuzi ya mtu mmoja mmoja mwenyewe...

Rais ni mtu tu kama mimi na wewe tulivyo. Naye Siku ya hukumu atauacha urais wake kule na ataingia hukumuni na kutoa hesabu ya dhambi zake sawasawa na watu wengine...

Kwa hiyo, kwa hili hatuwezi kumfuata Rais au waziri au baba au mama eti kwa kuwa kachanjwa kwanini na Mimi nisichanjwe. Kwa sababu kwa jambo hili, kila mtu ataokoka kwa imani yake...!

Ndo kusema;

Kuna wanaoshadidia chanjo hii wakiongozwa na serikali & madam President Samia S. Hassan..

Wanaoipinga chanjo hii tunaongozwa na Bishop Rev. Josephat Gwajima wa makanisa ya Ufufuo na Uzima. Wango wengi sana ila huyu mawimbi ya sauti yake yanasikika kupitia masafa marefu [high air frequency]...

Mch. Josephat Gwajima akiwakilisha wana wa ufalme Wa mbinguni, ameeleweka vyema...

Leo kijijini kwetu huku Shinyanga, wanafunzi karibu 1,000 walitimua mbio na kuwaacha walimu baada ya gari moja kufika shuleni na wao kudhani wachanjaji wamefika...

Dakika chache baadaye shule ilibaki tupu ikiwa na walimu wachache baadhi...

Dakika chache kundi la wazazi lilifika shuleni likiwa na mawe kuivuruga na kuiponda ponda gari ya chanjo...

Baadaye kiongozi wa serikali wakiwa na askari wachache walifika na kutuliza hali...

Hii ndiyo hali halisi ya chanjo ya UVIKO 19 Tanzania kwa sasa...
 
Mtakuja na maelezo ya Kila namna ila Watanzania waliowengi walimuelewa Sana Magufuli,na Sasa Gwajima.Ndiyo maana matukio ya wanafunzi kukimbia mashuleni wanapotilia Shaka gari kuwa Lina chanjo yameongezeka Sana.

Sasa jiulize hawa watoto ni Nani aliwaambia chanjo hazifai na lini?
 
Watanzania tuchanjwe
Sawa tuchanjwe.
lakini wahakikishe kuwa 70% ya watu watapata chanjo.
Kama watachanjwa watu millioni 1 basi ujuwe hawa wana weza kupata corona na kuwaambukiza walobaki ya hiyo inayo itwa Delta wimbi latatu.

Walochanjwa na kupata corona, wanaweza kuambukiza wasochanjwa na ngoma ikawa hatari sana
 
Kwa trend reading hadi sasa,naona "variant game" ikishika kasi.
Tunaweza kujikuta kizazi cha watu wanaoupdate miili yao kwa kudungwa booster vaccines kila wakati.After two,three,six,ten years tutakuwa wale wale kimwili na kiroho?!
Ripoti kila kona ya dunia sasa zinaconfirm kwamba hata waliochanjwa wanaugua tena kwa hizi new variants hasa delta.
Tunasema unvaccinated ndio husababisha variants.Lakini leo hata vaccinated nao wanatest positive na wanaugua.What does it mean?kwamba wao nao wanaweza kutuletea "super deadly variant"?then whats the point kuinject watu vaccines?
Ni angalizo tu kwenu jamii tutafakari sana kesho yetu.
Pupa ya kutaka kuimaliza covid haraka isituingize kwenye tatizo jingine kubwa sana.I can see from far away!an im mourning!Mungu aingilie kati!

I'll be updating you guys!Tupo hapa!
 
Sasa tumekaa na mamkubwa tukadunga zote mbili sijui hata zinaitwaje potelea karibu, Jana napata taarifa kuna ya 3 sijui imetoka wapi.
Mi bana nimeghairi nakomaa tu kama kufa kupo tu sichomi hiyo ya tatu.
Mungu niwekee jimbo langu huko angalau niwe mkuu wa wilaya au diwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…