#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
wagonjwa wa;
1.KISUKARI
2.UKIMWI
3.SARATANI
4.MOYO
5.PRESHA
6.TB
tuchukue tahadhari maaana hili wimbi la 3 la delta linapuputisha sana wenye maradhi hayo.
chukua tahadhari piga chanjo

tupo LAMBDA delta ndo inaishia
 
Ni kweli nimewahi kuchanjwa utotoni na pia kumeza Dawa ila tangia mwaka 2018 mpaka leo sijawahi kumeza Dawa Tena Zaidi labda cream za fungus kwenye ngozi.

Kama Ni kufa acha nife ila chanjo sichomwi nachofanya ni kula matikitimaji, matango, kabeji, matembere, ugali, samaki, maboga, maziwa, maji ya kutosha n.k

Na mazoezi ya kutosha japo siku hizi nimekuwa mvivu mwili unakataa kabisa kufanya mazoezi ila ipo siku mwili ukiwa tayari narudi kwenye matizi we ngoja tu nipate raba nzuri nyepesi.

Kwa hivyo tusilazimishane kila mtu abebe msalaba wake na kila mtu afanye biashara na anawaotaka na kuwaamini.

Maisha mbona mazuri tu kila mtu aamini material yake
 

Ishu ya chanjo ya UVIKO 19 ni very complicated. Ishu hii imeshaligawa taifa. Imegawa wananchi. Imegawa viongozi wa vyama vya siasa na serikali...

Hii ishu kwa 100% haina sura ya program ya kawaida ya serikali...

Sasa ni dhahiri ni ishu ya KIIMANI zaidi...

We all know, kuwa, mambo ya imani siku zote ni very complicated...

Suala la mtu aamini nini, siku zote huwa ni maamuzi ya mtu binafsi...

Imani haina cha kumfuata Rais wala waziri, mama au baba, kaka au dada... Ni suala la maamuzi ya mtu mmoja mmoja mwenyewe...

Rais ni mtu tu kama mimi na wewe tulivyo. Naye Siku ya hukumu atauacha urais wake kule na ataingia hukumuni na kutoa hesabu ya dhambi zake sawasawa na watu wengine...

Kwa hiyo, kwa hili hatuwezi kumfuata Rais au waziri au baba au mama eti kwa kuwa kachanjwa kwanini na Mimi nisichanjwe. Kwa sababu kwa jambo hili, kila mtu ataokoka kwa imani yake...!

Ndo kusema;

Kuna wanaoshadidia chanjo hii wakiongozwa na serikali & madam President Samia S. Hassan..

Wanaoipinga chanjo hii tunaongozwa na Bishop Rev. Josephat Gwajima wa makanisa ya Ufufuo na Uzima. Wango wengi sana ila huyu mawimbi ya sauti yake yanasikika kupitia masafa marefu [high air frequency]...

Mch. Josephat Gwajima akiwakilisha wana wa ufalme Wa mbinguni, ameeleweka vyema...

Leo kijijini kwetu huku Shinyanga, wanafunzi karibu 1,000 walitimua mbio na kuwaacha walimu baada ya gari moja kufika shuleni na wao kudhani wachanjaji wamefika...

Dakika chache baadaye shule ilibaki tupu ikiwa na walimu wachache baadhi...

Dakika chache kundi la wazazi lilifika shuleni likiwa na mawe kuivuruga na kuiponda ponda gari ya chanjo...

Baadaye kiongozi wa serikali wakiwa na askari wachache walifika na kutuliza hali...

Hii ndiyo hali halisi ya chanjo ya UVIKO 19 Tanzania kwa sasa...
 
Mtakuja na maelezo ya Kila namna ila Watanzania waliowengi walimuelewa Sana Magufuli,na Sasa Gwajima.Ndiyo maana matukio ya wanafunzi kukimbia mashuleni wanapotilia Shaka gari kuwa Lina chanjo yameongezeka Sana.

Sasa jiulize hawa watoto ni Nani aliwaambia chanjo hazifai na lini?
 
Watanzania tuchanjwe
Sawa tuchanjwe.
lakini wahakikishe kuwa 70% ya watu watapata chanjo.
Kama watachanjwa watu millioni 1 basi ujuwe hawa wana weza kupata corona na kuwaambukiza walobaki ya hiyo inayo itwa Delta wimbi latatu.

Walochanjwa na kupata corona, wanaweza kuambukiza wasochanjwa na ngoma ikawa hatari sana
 
Tunasema chanjo hupimwa effectiveness na safety.

Hivi vyote vinataka muda wa kutosha kuvihakiki in short and long term basis.

Chanjo ya corona imetengenezwa under pressure kwa uharaka wa kudhibiti ugonjwa usiendeleee kusambaa zaidi duniani,na haswa ikizingatia ugonjwa wenyewe husambaa kwa njia ya hewa(njia hatari sana).

Mpaka sasa tunaweza kuzungumzia athari chanya au hasi za chanjo hii in short term basis sababu bado ugonjwa wenyewe na chanjo hatujakaa navyo muda mrefu.

Katika short term basis tayari kumeibuka variants ambazo upo ushahidi there is a need for additional booster apart from vaccine itself ili kuweza kupambana na variants watakaokuwa wanajitokeza.

Hatujui how many variants we are going to encounter.

Hapa tayari kwa upande wangu effectiveness ya vaccine ishaingia mashaka.

Na kama effectiveness iko mashakani in long term basis hata safety nayo inaingia doubts,tutakuwa watu wa aina gani tukiwa kila wakati tunadungwa kemikali zinazotemper na dna zetu?!hizi dawa za kawaida tu matumizi ya mara kwa mara zinatuathiri what about chanjo?(tena ya respiratory disease ambayo kila mwaka yana msimu wake lazima yatokee).

Chanjo za magonjwa yaliyopita zilichanjwa huku kukiwa na idadi kubwa tu ya watu ambao hawakuchanjwa na idadi hiyo ya wasiochanjwa haijawahi kuleta new deadly variants kama hii corona.Whats so special about corona variants?!(ambazo ni always deadly hakuna variant inayokuwa less).

Kuna jamii duniani ambazo bado ugonjwa huu sio tishio sana to the extent of taking risk measures kama kuwaintoxicate na a lot of chemicals in the name of vaccine.
Mfano ni sisi waafrika.

Ukitazama speed ya maambukizi Tanzania na kiwango cha athari kilichojitokeza,je,possibility ya kuathirika na deadly variants inaendana na uzito wa kudunga watu wetu haya machanjo ambayo hatujayapa muda wa kutosha wa kuyajua effectiveness na safety in long term basis?

kwanini hatutumii hii resistance ya kinga zetu za asili kuweka other strict measures kuhakikisha tunazuga kidogo muda wa kutosha ili kuona nini kinachoendelea kwingineko?Is it neccessary na sisi kuichukulia corona kama national emergency of level one response?!

Tusisahau kuwa response tunayoipata toka kwa wananchi wa kawaida juu ya chanjo ya corona inatueleza jinsi gani jamii yetu haina habari kabisa na tishio la corona.Kwa hiyo naamini wakati wenzetu kwingineko wanachanja jamii zao kama hatua ya KUDHIBITI(unadhibiti athari ambayo ipo na imeshaleta madhara makubwa) maambukizi,sisi tunachanja jamii yetu ili KUIKINGA(unakinga athari isiyokuwepo au iliyopo kwa kiwango kisicho na madhara lakini yenye uwezekano mkubwa wa kuongezeka baadae).

Kwa kuzingatia njia inayotumika kudhibiti si njia salama sana(kuingiza kemikali mwilini kama ilivyo kwa kunywa madawa mengine na chanjo)then upo umuhimu wa kuzingatia pia kile kinachosababisha hadi sasa ugonjwa huu hausumbui sana jamii ya watanzania.Nacho kizingatiwe na kitumike kutufanya always tuwe ahead of time na advantage.Ikibidi twende mdogo mdogo,tusikimbizane sana na dunia ila tuilinde sana jamii yetu kwa njia za kawaida kwanza.

Waafrika tungeungana kuhakikisha dunia inaheshimu na kukubali uhalisia wa ugonjwa wa corona na njia tunazotumia huku Afrika.
Kwa trend reading hadi sasa,naona "variant game" ikishika kasi.
Tunaweza kujikuta kizazi cha watu wanaoupdate miili yao kwa kudungwa booster vaccines kila wakati.After two,three,six,ten years tutakuwa wale wale kimwili na kiroho?!
Ripoti kila kona ya dunia sasa zinaconfirm kwamba hata waliochanjwa wanaugua tena kwa hizi new variants hasa delta.
Tunasema unvaccinated ndio husababisha variants.Lakini leo hata vaccinated nao wanatest positive na wanaugua.What does it mean?kwamba wao nao wanaweza kutuletea "super deadly variant"?then whats the point kuinject watu vaccines?
Ni angalizo tu kwenu jamii tutafakari sana kesho yetu.
Pupa ya kutaka kuimaliza covid haraka isituingize kwenye tatizo jingine kubwa sana.I can see from far away!an im mourning!Mungu aingilie kati!

I'll be updating you guys!Tupo hapa!
 
Sasa tumekaa na mamkubwa tukadunga zote mbili sijui hata zinaitwaje potelea karibu, Jana napata taarifa kuna ya 3 sijui imetoka wapi.
Mi bana nimeghairi nakomaa tu kama kufa kupo tu sichomi hiyo ya tatu.
Mungu niwekee jimbo langu huko angalau niwe mkuu wa wilaya au diwani.
 
Back
Top Bottom