Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Mimi nilitafutaga sana kipindi fulani ila nikakosa. Watoto wa elifu mbili hawajui hii kitu
 
Nakumbuka sisi home tulikuwa tunautumia kama dawa.
 
Unaitwaje kwa English ni google naona mmeshindwa kuweka picha

Mkuu, sifahamu unaitwaje kwa kiingereza, lakini kuna mdau hapa kanikumbusha jina moja nadhani ni la kiswahili "kombucha" nakumbuka pia hilo jina!
 

Dah, aha aha haaa!

Pole sana mkuu, inachekesha lakini pia inafurahisha!

Ni kweli hata Mimi kuna wakati lile lichapati lililopokuwa linazaa nilikuwa natenga masufuria mengine na mabakuli makubwa kama yakunawia mikono nayaweka hayo machapati mimea humo! Basi bi.makubwa akawa ana mind sana! Analalamika,"sasa wewe unataka kugeuza vyombo vyote kuwa vya kuwekea hilo lidude lako?!" Alafu sisi tutapikia wapi?!" aha ha haaa! ilikuwa zahama!

Ule mmea ulikuwa mzuri sana aisee,,, mpaka leo nautafuta lakini bado sijaupata!

Mwenye nao tunaomba wandugu!
 
Ungekuwa unashare na wengine now usingepata shida ya kupata mbegu.

Mkuu, tatizo miaka ile ya katikati mwa 1990, watu wengi walikuwa hawaujui huu mmea, mengine walikuwa hata wana uogopa! Wengine wanauonea kinyaa! Na mengine mpaka wanadiriki kuuita ni mambo ya kishirikina!(kichawi).

Kwahiyo kumpa mtu ambaye anauhisi labda ni mambo ya kishirikina sio rahisi mkuu, sisi zile mbegu zake tulikuwa tunafukia chini, tunachimbia shambani.
 

Kabisa mkuu!

Ukiwa na huu mmea, hata magonjwa ya ajabu ajabu hayakupati kirahisi, unasaidia ku-boost kinga mwili na pia unasaidia mfumo wa usagikaji wa chakula digestion.
 
Unaitwa KOMBUCHA nakumbuka enzi hizo tumeinywa sana juice yake kwa Bibi hukoooo Marangu. Aisee umenikumbusha mbali sana


Kombucha (also tea mushroom, tea fungus, or Manchurian mushroom when referring to the culture; Latin name Medusomyces gisevii[1]) is a fermented, lightly effervescent, sweetened black or green tea drink commonly consumed for its purported health benefits. Sometimes the beverage is called kombucha tea to distinguish it from the culture of bacteria and yeast.[2] Juice, spices, fruit or other flavorings are often added.


Kombucha
 
Sifa ya kukaa na ule m'mea ni kushare na wengine usiposhare unakuwa unaukosea.

Unatakiwa uwe unawakatia watu na kuwagawia usambae. Ni m'mea ambao hautakiwi kumchaji mtu kuupata.
 

Ni kweli mkuu,


Kama unao au ukisikia mtu anao tujulishane ndugu yangu!
 
Sifa ya kukaa na ule m'mea ni kushare na wengine usiposhare unakuwa unaukosea.

Unatakiwa uwe unawakatia watu na kuwagawia usambae. Ni m'mea ambao hautakiwi kumchaji mtu kuupata.

Ni kweli kabisa,

Lakini miaka ile watu wengi walikuwa hawaujui huu mmea, na mengine walikuwa wanauogopa hata kuuhusisha na ulozi.
Hivyo inakuwa ngumu kumpa mtu. Kwasasa nadhani wengi wanaufahamu hivyo kuwa rahisi kushare!
 
Huu mmea uliwahi kuniponya Athma nikiwa binti mdogo...Nilikuwa nikibanwa Mara kwa Mara na kutumia vidonge vya hospital na zile dawa za ku inhale lakini Mambo yalikuwa mperampera, Kama kawaida ya Tanzania Mambo ya milipuko Ni mengi,Mara Ngetwa3,Mara Ngoka11,Mara mayai ya kwale,Mara Kikombe Cha Mwaisapile...Basi ikatokea hili lichapati ,hii kitu nilikunywa Kama miezi miwili Nakumbuka mama yangu aliyapanda kwenye madishi,Basi nakunywa Kama juisi daily....ninachokumbuka baada ya hapo sijabanwa Tena kifua mpaka Sasa nimezeeka....Ila linachefua ukiliona Kama miutelezi gani sijui🥴
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…