Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Mzee Kwayu alikuwa ni the best Principal kwa ile shule. Alipoondoka likaja dubwana fulani linaitwa chavila. Lile zee sijui lilitumwa. Likaja na system ya roll call, kukamata watoro, likaziba lile geti dogo la kuingilia jangwani kule.

Lile zee jamani....
 
Mmea mzuri sana unanikumbusha mbali ,naweza upata wapi huo mmea gheto ulikua unawekwa na bi mkubwa kwenye kile kifuniko cha jiko la kichina lisilotumika lile la mafuta ya Taa .Mleta mada nauhitaji
Na mimo bi mkubwa alikuwa anaweka kwenye hiyo kitu.
 
mkiupata nami nahitaji, nimeishywa sana kwa bibi miaka ya 90, watu walianza kuzusha ni mapepo watu wakaanza kuzitupa
Mimi pia bi mkubwa wangu alimwaga chapati zote zilikuwa zimeshika na kumea sana kulikuwa na sufuria kama sita hivi. Akamwaga baada ya kuambiwa na pastor kuwa hayo ni mapepo na ni maagano ya kuzimu.

Yule pastor nilimchukia hadi leo fala yule.
 
Tulikuwa tunaita Chapati ya Ajabu
 

Daah, kitambo sana mzee!

Lile geti dogo la kutokea kule jangwani nilikuwa nalitumia kama nikichelewa tu,hasa kama ni session ya mchana!
Nikiwahi napitia kule mbele kwenye lile container la duka la stationery!

Japo matozi walikuwa wanapita kule geti dogo kwa yao! Aha ha haaaa!
 
Nipo china miaka yote na nilikuwa siujui, leo ndo nimeusearch hapa baada ya kusoma huu uzi[emoji4][emoji4].. Ningekuwa na uwezo wa kukunulia mtoa mada na kukutumia maybe uje kushare na wenzako ningefanya mpango.. Maybe nikiupata we can see frm there
 
Initwa "Kombucha" kwa lugha ya kigeni. Kuna kampuni baadhi hapa TANZANIA wanasindika hii
Kampuni kama zipo mkuu? Kama unazijua kwa majina zitaje maana watu hapa wanahitaji hii kitu. 'Kombucha'. Isije kuwa hayo ma kampuni ya nauza juice tu kwenye chupa. Huuziwi ile 'Mother cell' ili ukazalishe mwenyewe na ukagawie wenzako.
 
Huo mmea kuna jamaa yake alinikatia kipande nikaenda weka kwenye maji kikakua namimi nikawa nagawia wengine. Tulifaidi sana juice yake mwaka 1996/97 ndio nilikua nao. Lilikua dude jeupe hivi laini. Ukiwa nalo enzi hizi unaanzisha kikombe cha babu utapiga hela balaa
 
Nipo china miaka yote na nilikuwa siujui, leo ndo nimeusearch hapa baada ya kusoma huu uzi[emoji4][emoji4].. Ningekuwa na uwezo wa kukunulia mtoa mada na kukutumia maybe uje kushare na wenzako ningefanya mpango.. Maybe nikiupata we can see frm there

Daaah,,, kweli sharing is caring! Tusinge-share hii mada pengine tusingepata mtu anayejua wapi uliko!

Mkuu, kwanza nikupongeze kwa kujali na kuutafuta mpaka umeupata!

Pili please nikuombe sana ikiwezekana Fanya hima juu chini tuupate mkuu, utakuwa umefanya jambo la kishujaa sana hapa jamiiforum, please!
 
Sasa mkuu ulikaa nao kichoyo hata hukutusambazia wadau mapema, saiv tungekusaidia mbegu

Hapana mkuu, miaka ile ya tisini (90's) wengi walikuwa hawaujui na wengine walikuwa wanauhusisha na ushirikina (ulozi) kwahiyo inakuwa ngumu sana kushare na mtu hasiye uamini.

Pili tulikuwa bado wadogo sana mayanki, kufikiria jambo hilo! Ndio maana unaona wengi humu wana-comment kuwa waliwahi kuwa nao lakini ukafa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…