Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Kampuni kama zipo mkuu? Kama unazijua kwa majina zitaje maana watu hapa wanahitaji hii kitu. 'Kombucha'. Isije kuwa hayo ma kampuni ya nauza juice tu kwenye chupa. Huuziwi ile 'Mother cell' ili ukazalishe mwenyewe na ukagawie wenzako.

Nikitaka kuuliza hili swali nikasahau!

Akitujibu atakuwa ametusaidia pia, maana chamsingi ni kupata ule mmea wenyewe na sio juice yake tu!
 
Kwa sisi tuliuita mkate wa Mecca. Miaka ya nyuma wengi waliotoka Hijja walirudi nao, na ukizaa/ totoa unampatia na mwenzio, ukweli ni kwamba mmea ule ulikuwa ni Tiba. Sasa hivi mahujaji wengi waakiridi waanarudi na vitu vya kippuuzi zikiwemo simu na dildo.
Dildo tena !?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hii kitu alikuja nayo shangazi kama sio dingi kutoka mkoani mbeya.

Huu mmea hata Tanzania tunao sababu tuna utajiri wa species nyingi sana za mimea.

Ngoja nikutafutie jina na ukipatikana nitashare na ninyi hapa jina na ikibidi tugawane mbegu ni mzuri sana ile kitu tulikuwa tunaigida sana juice yake.

Tuliweka kwenye zaidi ya vyomba sita tukilina maji yake. Alikuja kuharibu bi mkubwa alipookoka akaambiwa na pastor wake kuwa kile kitu ni mapepo na ni maagano ya mizimu. Yule pastor choko sana hadi leo namind kichizi nikimuona natamani nimlabue makofi na mitama maaana ndie alimchanganya bi mkubwa akaona ule m'mea una uhausiano na maswala ya giza na kumbe ni ukosefu tu wa elimu ya mimea na tiba asili.

Bi mkubwa aliyamwaga yale masufuria yote kimya kimya ndo hadi leo sijuagi pa kuupata.
Kweli pastor choko , manina zake [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Huo mmea kuna jamaa yake alinikatia kipande nikaenda weka kwenye maji kikakua namimi nikawa nagawia wengine. Tulifaidi sana juice yake mwaka 1996/97 ndio nilikua nao. Lilikua dude jeupe hivi laini. Ukiwa nalo enzi hizi unaanzisha kikombe cha babu utapiga hela balaa

Ha ha haaaa! Mkuu umeshachungulia fursa tayari, "ukiwa nao enzi hizi unaanzisha kikombe cha babu unapiga hela!"
Tena kuna mdau huko juu alisema "ukiongeza na maneno kuwa unaongeza nguvu za kiume aisee unakuwa millionaire ghafla bin vuuu!!"

Aha ah haaaa!!

*By the way, ulikuwa mmea mzuri sana, sijui hata tulikosea wapi ukatoweka kabisa!
 
Huu mmea sidhani kama una mbegu, kinachofanyika ni kuwa kila unapotanuka ukikata kipande na kutia kwenye maji na chenyewe kinakua, kwahiyo cha muhimu ni kufanya timing kila unapokaribia kucover eneo lote la chombo chako unakata kidogo unatumbukiza kwenye chombo kingine chenye maji. Kifupi sijui kama kuna mbegu na sijui unapatikana wapi,ila hata mimi niliwahi kupewa na rafiki,nikakaa nao karibu miezi 2, nikajisahau ukawa ndio mwisho wake.
Nakumbuka ilikuwa inatoa layers za chapati nyingine, hivyo unabandua tu ile layer ndio mbegu hiyo.
 
Ni kweli mkuu,

Wanasema unatibu magonjwa mengi, ikiwemo high blood pressure (hypertension), blood infections (mchafuko wa damu), mifupa, depression, (msongo wa mawazo), stress, sononi, kusafisha figo, magonjwa ya uambukizi kwenye utumbo , kusafisha kibofu, n.k.
Ungeongeza unatibu na nguvu za kiume uzi ungekuwa mbali Sana.
 
Umenikumbusha mbali sana Mwaka 92 na tangu kipindi hiko sijawahi kusikia wala kuona popote pale zaidi ya kwa yule mama duuh! Nilikuwa nakunywa sana juice yake halafu watoto wake wakawa hawaipendi mimi nikuipa mambo tu kumbe yalikuwa yanapandwa? Mi nikajua ni ukwaju.
 
Unaitwa KOMBUCHA nakumbuka enzi hizo tumeinywa sana juice yake kwa Bibi hukoooo Marangu. Aisee umenikumbusha mbali sana

Kombucha (also tea mushroom, tea fungus, or Manchurian mushroom when referring to the culture; Latin name Medusomyces gisevii[1]) is a fermented, lightly effervescent, sweetened black or green tea drink commonly consumed for its purported health benefits. Sometimes the beverage is called kombucha tea to distinguish it from the culture of bacteria and yeast.[2] Juice, spices, fruit or other flavorings are often added.

Kombucha
Google
download.jpg
images.jpg
 
Umenikumbusha mbali sana Mwaka 92 na tangu kipindi hiko sijawahi kusikia wala kuona popote pale zaidi ya kwa yule mama duuh! Nilikuwa nakunywa sana juice yake halafu watoto wake wakawa hawaipendi mimi nikuipa mambo tu kumbe yalikuwa yanapandwa? Mi nikajua ni ukwaju.

Yanapandwa mkuu,

Nikama ua linalopandwa kwenye chupa ya maji,

Yana zaana na yanakufa pia, mimea mizuri sana, tulijisahau ikapotea kabisa!
 
Hawa wanazo price range 10,000 - 20,000 k chupa moja

View attachment 2117189

Duuh,,, maisha yanaenda kasi sana!

Wakati enzi zile tulikuwa tunakunywa na kumwaga!

Tulikuwa tuna yatupa mazalia yake vichakani au tunayazika chini!

Leo ni biashara nono?! Duh, kweli wakati si milele!

Labda kwavile wanavyo kuandalia na kufanya packaging hiyo lazima bei iwe juu!

Any way, sisi wakulungwa tuendelee na mchakamchaka wetu wakutafuta chapati yetu ya Kombucha kisha tusambaziane hapa, maana ukisema ununue hiyo chupa ya kombucha utanunua ngapi?! Na Mara ngapi?! Bora tupate mbegu yetu ya kombucha tea mushroom itatufaa zaidi...!!
 
Nimefurahi sana kuona mada kuhusu huu mmea, nakumbuka miaka ya 90's tuliwahi kuutumia nyumbani na mama alisema kuwa aliutoa kwa bibi. Mama ameshafariki na nilitamani kweli kujua huu mmea chapati ni nini haswa lakini kila nikimuuliza bibi anasema haujui.
Habari wakuu,

Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.

Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.

Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!

Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa!

Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana!
View attachment 2116778
Nimefurahi ku

Back
Top Bottom