Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Wacha kupotosha hilo shamba halijaporwa hao smz wanalimiliki ki halali kabisa nyerere kwa mahaba yake Alimpa Aboud Jumbe litumiwe na Smz
Acha maneno ndugu, leta hati utasemaje unamiliki ardhi na hauna hati
 
Kwa mujibu wa huyo msemaji wa Smz aliejenga humo ndio imekula kwake
Sheria ya ardhi haiendeshwi na kauli ya msemaji wa SMZ. Siku akisema ardhi ya Zanzibar nzima ni ya bilionea mmoja kutoka Oman mtakubali kisa ni msemaji?
 
Angalizo tu; wachangiaji baadhi wajue hilo eneo limetolewa tangu enzi za Mwalimu. Wasije kufikiria ni awamu ya sita. Maana kuna wavivu wa kusoma history ya nchi ila wepesi kujadili history ya nchi wasiyoijua.🙏🙏🙏
Hati ipo
 
Sasa kama alizaliwa miaka 56 iliyopita (1967); miaka 59 iliyopita (1964) alinusurika vipi kuuwawa ilhali kwa maelezo yako hakuwa amezaliwa?
SOMA UELEWE, ACHA TALALILA
 
Kwa kauli hii wananchi iwa Tanganyika wana haki ya kuichukua ardhi hiyo maana hakuna mtu aliye juu ya sheria. Rais aliyepo alipoingia tu madarakani akaanza kupindua maamuzi ya mtangulizi wake kwa hiyo hata yeye akiondoka kile alichokiamua sasa kitaondoshwa na waliopewa wakishupaza shingo watanyang'anywa na kugawiwa wananchi wenye mahitaji ya ardhi.

Haiwezekani Zanzibar ambayo ina ardhi yake ambayo wananchi wa Tanganyika wakiomba wanakataliwa halafu wao wanapewa haki ya kumiliki kienyeji bila kufuata sheria na taratibu huku wenyeji wakikosa ardhi ya kuendeleza shughuli za kijamii.

Mpaka Oktoba hizo ekari 6,000 zinazodaiwa kubaki zitakuwa zimebaki ekari 500 tu na hakuna wa kuwanyang'anya na atakayetghubutu kufanya hivyo ama kwa kutumia madaraka au sheria watashindwa.
 
Sheria ya ardhi haiendeshwi na kauli ya msemaji wa SMZ. Siku akisema ardhi ya Zanzibar nzima ni ya bilionea mmoja kutoka Oman mtakubali kisa ni msemaji?
Wewe kama unabisha nenda kajenge hilo eneo halafu uone watafanyaje
 
Wewe nenda kajenge halafu uone watafanyaje
 
Yaani umepewa eneo bila nyaraka, na miongo kadhaa imepita hujaendeleza chochote, watu wameingi na kufanyia kazi zadi ya 60% ya eneo. Leo imebaki 40% unadai una haki nayo, shuleni watakuwa wameenda kusomea ujinga tu.

Waambieni wanakula na kipofu... Wachunge sana.
 
Acheni kipoteza focus ya watanzania waanze kujadili ardhi hewa ya Wazanzibari badala ya kujadili Bandari za Yanganyika.
 
Nyerere aliwaadhima wanenepeshe ng'ombe. Ila awamu ya 6 ndio inataka kutoa hati ya umiliki. Kama si hivyo Nyerere kwa nini aliwapa bila hati?
 
Hii ni skandali nyingine in the making.
Eneo halina hati za umiliki mpaka sasa!
Nchi ya Zanzibar kumiliki ardhi bara kama nani? Kama mwekezaji?
SMZ washauriwe kuachana na hiyo ardhi maana hivi karibuni itageuka kuwa issue nyingine ya kuhojiana kuhusu Muungano.
Kwa kuwa Nyerere aliwapa kwa maneno, na hawakufatilia kupata hati za umiliki wakati huo, kujaribu kuzipata sasa hivi ni kutafuta kumzulia skendo nyingine SSH.
Just let it go, mwisho wa maneno.
 
Unasaidiwa eneo kwa muda, baadae unasema mali yako.
Pia kuna Sheria inasema ukipewa au ukiwa na Ardhi na haujaiendeleza kwa miaka 3 , Ardhi hiyo utaweza kuipoteza..na hati nyingi za zamani ukomo wake ulikua ni 33yrs... alafu naomba kujua.. serikali pia inajitengenezeaga hati!?... Na kama jibu ni ndio...hati za upande wa bara zinaandikwa kwa jina gani!? Na ni nani custodian wake!?....wanaojua wanisaidie majibu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…