Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Wazanzibari hawana shukrani! Tanganyika iliwapa favours nyingi sana kwenye elimu na vitu kama hivi. Naamini Baba wa Taifa alipolitoa, ilikuwa katika kujaribu kuwasaidia kupata nyama. Tangu wamelitelekeza, leo ndo wamekumbuka! Wakwende zao huko!
Weka ushahidi wa hicho unachokisema
 
Mh.Charles Hillary yuko sahihi....

Tanzania ni moja....

Muungano wetu ni wa KIPEKEE....majibu yake ni uwepo wa SERIKALI MBILI badala ya hamu ya wanaoitaka DOLA YA TANGANYIKA....

Tanganyika ILIFUTWA....

Hayati Nyerere akasema "Siwezi kuimeza Zanzibar ...ni ndogo sana....ardhi ya bara ni kubwa sanaa....".

Wajinga wa mambo haya wajue kuwa Zanzibar nako kumejaa sisi wenyeji wa kutoka huku bara....

Sensa ya 2012 ,Zanzibar ilikuwa na wakazi wanaokaribia milioni 1....

Sensa ya 2022 Zanzibar ina wakazi milioni 1.9.....

Ni kwa kuzaana kupi kwa wazanzibari kulikosababisha ongezeko hilo kubwa kwa muda mfupi huo ?!!!

Jibu ni kuwa TANZANIA ni moja na MUUNGANO wetu ni wa KIPEKEE na hauna REJEA kutoka miungano ya nchi nyingine......

#SiempreJMT[emoji120]
Huyu tumjibu au tumuache?
 
Angalizo tu; wachangiaji baadhi wajue hilo eneo limetolewa tangu enzi za Mwalimu. Wasije kufikiria ni awamu ya sita. Maana kuna wavivu wa kusoma history ya nchi ila wepesi kujadili history ya nchi wasiyoijua.🙏🙏🙏
Hayo ndiyo matatizo ya mikataba/makubaliano yasiyokidhi sheria. Kama kungekuwepo mkataba wa maandishi, leo hii hakungekuwa na haja ya mjadala. Vivyo hivyo, suala la bandari linahitaji mkataba ambao hautazua malumbano siku za usoni. Tayari tumeona si chini ya nchi tisa zilizofikishana mahakamani na DP World. Lazima tugutuke na kuchukua tahadhari zipaswazo.
 
Huyu ni mzazibar lazima atetee Zanzibar.
Hilary, ambaye pia aliasisi kipindi cha Charanga Time kilichomzidishia umaarufu akiwa Radio One Stereo, alizaliwa Zanzibar miaka 56 iliyopita eneo la Jang’ombe. Aliwahi kunusurika kuuawa kwa risasi mwaka 1964, siku moja baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoundoa utawala wa Sultan na kuiweka Serikali ya Watu wa Zanzibar.
Sasa kama alizaliwa miaka 56 iliyopita (1967); miaka 59 iliyopita (1964) alinusurika vipi kuuwawa ilhali kwa maelezo yako hakuwa amezaliwa?
 
Back
Top Bottom