Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Uzoefu wa wengi waliokuwa wafanyakazi wa mashirika na taasisi za umma, hujiunga na siasa na hasa na chama tawala kama kinga ya kutoweza kutakiwa kuwajibika kwa yale mapungufu ya yale walioyafanya katika taasisi waliokuwa wanaziongoza. Kimei is no exception!!
Angebaki kama mzee mshauri mbobezi ingemjengea picha njema zaidi. Mimi mzalendo ila sina chama
 
Asante mkuu. Natumai haya ni maoni yako na unaruhusu maoni tofauti na haya.

Maoni yangu, hujafikiria mvutano wa kisiasa ndani ya CHAMA ili kupata nafasi ya kupeperusha bendera yake ktk uchaguzi. Hiyo inaonesha ni namna gani anakubalika, si kwa Taaluma yake pekee, bali na kwa Wananchi/Jamii yake (natumai utawakumbuka Wajumbe). Hali hiyo ni tofauti ikilinganishwa na Vyama Rafiki ambapo kufahamiana na Uongozi wa Juu (mf M'kiti) ni tiketi tosha kupata nafasi hiyo.
Pia hujafikiria CV aliyojijengea Kitaifa na Kimataifa kwa kupata nafasi hiyo ya Ubunge (iwe kwa Chama Tawala au Vyama Rafiki). Na umuhimu wake kiuchumi kwa nchi yetu, akiwa na nafasi ya Ubunge.
Umetolea mfano CEO (rtd) William B. Harrison Jr. wa ABA. Maoni yangu, si sawa. Jitahidi kuifahamu Marekani (wenye maamuzi) na sera za nje za Marekani, badala ya kuwalingalisha hawa Wataaluma wawili wa Benki waliopo mazingira tofauti.

Nakupongeza kuwa umewafikiria wakerekwetwa wa Kambi Mbadala. Nakushauri ujumuishe na uwezo wake wa namna Taaluma yake haikuathiri mahusiano yake na jamii.

NARUHUSU KUKOSOLEWA
 
eti saizi nayeye anauliza swali la nyongeza anajibiwa na Silinde
 
Sioni tatizo sana. Anaweza kutumika vizuri tu kwa manufaa mapana ya nchi akiwa mbunge. Atapata fursa nzuri ya kushauri watunga sera kirahisi zaidi anapokuwa kwenye game.
Kwani asingekuwa mbunge asingekuwa na manufaa kwa taifa mkuu? Huu ni ushauri wangu tu kwake na sio lazima yeye aufuate...
 
Mambo vp JamiiForums.

Ninapoandika hoja hii, ninaomba ifahamike kuwa i have nothing personal with mzee Kimei na ninatambua kuwa yeye ni moja katika ya hazina kubwa ambazo taifa hili linazo katika masuala mazima ya uchumi na banking.

Watu walikuwa wanapenda sana kumshambulia kaka yangu Pascal Mayalla kuwa amejiingiza katika siasa kwa sababu ya njaa. Sasa huyu CEO mstaafu yeye ana njaa gani? Charles Kimei alipaswa kubaki kama mzee mshauri wa masuala ya uchumi/banking hapa Tanzania/Africa Mashariki na sio kujiingia katika siasa hizi za vyama.

He is one of the most exposed and reputable top executives in banking and finance industry kwa hapa Tanzania na East Africa. Hakupaswa kuonesha mlengo wa wazi wazi wa chama chochote cha kisiasa kiwe upinzani au tawala.

Siasa hizi za vyama angewaachia mzee Dr. Bashiru Ally na Mheshimiwa Mbowe. Kimei angebaki kuwa kama William B. Harrison Jr. CEO mstaafu wa bank kubwa kuliko zote ya Marekani ya JPMorgan Chase ambaye sasa ni mshauri mwandamizi katika umoja wa banks za nchini humo - The American Bankers Association - (ABA)

William B. Harrison Jr.
=====

View attachment 1694756

Hata kama asingekuwa mbunge wa CCM akaamua kujiunga na CHADEMA, CUF au ACT, kitendo cha kujiingiza katika siasa za vyama kunampotezea intergrity yake aliyotumia nguvu kubwa na miaka mingi sana katika kuijenga kwenye tasnia ya masuala ya uchumi/banking.

Watumishi wa CRDB wenye mlengo tofauti wa kisiasa (upinzani) waliokuwa wanamuona kama role model wao sasa wataanza kuzozana naye hata kama sio face to face hata kupitia mitandao. Alistaafu kwa heshima nzuuuuri mzee wa watu, sasa anajiharibia heshima alipojiingiza kwenye siasa.

Achilia mbali CRDB, wale watumishi wa banks zingine waliokuwa wanamuona kama kioo bora kwa maana aliitoa CRDB kutoka kuwa bank ya kitanzania mpaka kufungua matawi yake nchi jirani, sasa nao atakuwa anajibizana nao kwa sababu za kisiasa. Yeye CCM wao wapinzani. Ipo wapi tena heshima ya mzee Kimei katika industry ya banking?

Kimei kwa levels zake angepaswa awe anaendesha kampuni kubwa sana ya masuala ya ushauri wa kiuchumi/kibank Africa Mashariki na sio kwenda bungeni kurushiana vijembe na wanasiasa ambao wengi ni umri wa watoto wake wa kuzaa, tena anawazidi mpaka exposure.

Kuna mada ilianzishwa humu kuhusiana na kauli yake moja ya kisiasa ( Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu? ) ambayo inaonekana imewakera wengi na watu wanamshambulia kweli kweli.

View attachment 1695012

Mzee Kimei kwa sasa ni mwanasiasa wa mlengo wa chama tawala (CCM), ina maana watu waliokuwa wanamuheshimu kama CEO bora kwenye banking/uchumi ambao wapo mlengo wa siasa za upinzani sasa wataanza kumtukana na kumrushia maneno ya kejeli jambo ambalo mzee hakuwa na ulazima wa kulifanya.

Wapo watu watahoji mbona kuna professors na PhD holders wapo katika siasa miaka nenda rudi, lakini ni nani kama Kimei katika taaluma ya banking? Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Huyu alidanganywa na ccm kwamba atakuwa Waziri wa fedha
 
Kumuheshimu mtu au kumdharau kutokana na mrengo wake kisiasa ni makosa. Kigezo kikuu ni anasaidiaje au kuipotoshaje jamii kupitia taaluma yake.
Upo sahihi sana mkuu, lakini ni wachache sana ndio wataweza kulielewa hili...
 
Kimei mwenyewe anajua heshima yake imeshuka kwa kiasi gani hadi sasa....na najua hakutegemea coz alitegemea apate uwaziri ambao unaendana na hadhi alokua nayo...saiz hana tofauti na jose msukuma
 
Sioni tatizo sana. Anaweza kutumika vizuri tu kwa manufaa mapana ya nchi akiwa mbunge. Atapata fursa nzuri ya kushauri watunga sera kirahisi zaidi anapokuwa kwenye game.

Kumuheshimu mtu au kumdharau kutokana na mrengo wake kisiasa ni makosa. Kigezo kikuu ni anasaidiaje au kuipotoshaje jamii kupitia taaluma yake.

Sio wanachana wote wa chama kimoja wanakubaliana kwa kila kitu. Na motives za kujiunga na chama fulani zinatofautiana kati ya mtu na mtu. Ni mapema kuhukumu
Asante kwa maoni yako lakini all in all angebaki kama mzee mshauri mtaalam ingefaa zaidi.
 
Viongozi wengi walio kuwa na nyadhifa za uteuzi wapo kisiasa na kwa maslahi ya waliowateua.

Ukifuatilia sanà,utagundua mpaka viongozi wa taasisi za vyombo vya dola wengine wamestaafu na kugombea nafasi za kisiasa.Kwa hiyo wengi wamo au wanatumikia siasa wakiwa katika nyadhifa za uteuzi.
Kuna IGP au CDF aliyewahi kugombea nafasi ya kisiasa mkuu?...
 
Mwenyekiti wa Chama Mkoa mmojawapo alikuwa RPC,aligombea uenyekiti na akawashinda makada wengine!
RPC ni ngazi ya mkoa tu kama manager wa CRDB mkoa. Kimei ni top kama IGP
 
Viongozi wengi walio kuwa na nyadhifa za uteuzi wapo kisiasa na kwa maslahi ya waliowateua.

Ukifuatilia sanà,utagundua mpaka viongozi wa taasisi za vyombo vya dola wengine wamestaafu na kugombea nafasi za kisiasa.Kwa hiyo wengi wamo au wanatumikia siasa wakiwa katika nyadhifa za uteuzi.

Kwa suala la huyu ndugu hata zile fedha zilizokuwa na kashfa ya makampuni ya EPA zilipitia/ kupigwa katika taasisi aliyokuwa anaisimamia yeye, na hakuwahi kuzungumzia wala kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kashfa ile bali alikaa kimya au kuachwa na wakubwa!
Kwa hiyo hapo alipo ndipo anaona yupo salama na amani ndani ya nafsi yake(Sisi tunamtazama kitaaluma,lakini yeye binafsi anajitazama na kuishi kisiasa)!
Haya bhana mimi nimemshauri tu kama mzalendo mwenzake
 
Mleta uzi amempamba sana Kimei kuwa ni mbobezi wa mambo ya kibenki Tanzania na Afrika Mashariki nzima; cha kushangaza ni kwamba huyo Kimei hajajitambua na ndio maana akakubali kwenda kudhalilishwa wakati wa kuusaka ubunge na kwenda kwa Sangoma!!!! Unajua kiasi gani cha mikopo chefuchefu Kimei aliiacha alipostaafu CRDB? Unajua kuwa hiyo mikopo chefu chefu aliitoa kwa hao wanaoitwa mafisadi wakina Manji? Je hakufaidika na hiyo mikopo chefu chefu kwa wakina Manji?
Duuuh, hii sijui mimi mkuu na sio lengo la mada hii...
 
Acheni mawazo ya kidikteta. Kila mtu haki ya kuamua maisha yake. Nyie makamanda uchwara mnajiona mnaweza kuamua Kimei aishi vipi?
Sasa mbona nawe unajipa usemaji wa familia ya kimei? Kwa nini unaamini upo karibu na kimei kuliko hata mkewe? Kutokuwa dikteta ni kuacha mtu aongee anachotaka pasipo kuvunja sheria. Sasa unapomkataza mtu asiongee unaonesha una mawazo magonjwa.
 
Sasa mbona nawe unajipa usemaji wa familia ya kimei? Kwa nini unaamini upo karibu na kimei kuliko hata mkewe? Kutokuwa dikteta ni kuacha mtu aongee anachotaka pasipo kuvunja sheria. Sasa unapomkataza mtu asiongee unaonesha una mawazo magonjwa.
Wapi nimejipa usemaji wa hiyo familia?
 
Back
Top Bottom