Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Angebaki kama mzee mshauri mbobezi ingemjengea picha njema zaidi. Mimi mzalendo ila sina chama
 
Asante mkuu. Natumai haya ni maoni yako na unaruhusu maoni tofauti na haya.

Maoni yangu, hujafikiria mvutano wa kisiasa ndani ya CHAMA ili kupata nafasi ya kupeperusha bendera yake ktk uchaguzi. Hiyo inaonesha ni namna gani anakubalika, si kwa Taaluma yake pekee, bali na kwa Wananchi/Jamii yake (natumai utawakumbuka Wajumbe). Hali hiyo ni tofauti ikilinganishwa na Vyama Rafiki ambapo kufahamiana na Uongozi wa Juu (mf M'kiti) ni tiketi tosha kupata nafasi hiyo.
Pia hujafikiria CV aliyojijengea Kitaifa na Kimataifa kwa kupata nafasi hiyo ya Ubunge (iwe kwa Chama Tawala au Vyama Rafiki). Na umuhimu wake kiuchumi kwa nchi yetu, akiwa na nafasi ya Ubunge.
Umetolea mfano CEO (rtd) William B. Harrison Jr. wa ABA. Maoni yangu, si sawa. Jitahidi kuifahamu Marekani (wenye maamuzi) na sera za nje za Marekani, badala ya kuwalingalisha hawa Wataaluma wawili wa Benki waliopo mazingira tofauti.

Nakupongeza kuwa umewafikiria wakerekwetwa wa Kambi Mbadala. Nakushauri ujumuishe na uwezo wake wa namna Taaluma yake haikuathiri mahusiano yake na jamii.

NARUHUSU KUKOSOLEWA
 
eti saizi nayeye anauliza swali la nyongeza anajibiwa na Silinde
 
Sioni tatizo sana. Anaweza kutumika vizuri tu kwa manufaa mapana ya nchi akiwa mbunge. Atapata fursa nzuri ya kushauri watunga sera kirahisi zaidi anapokuwa kwenye game.
Kwani asingekuwa mbunge asingekuwa na manufaa kwa taifa mkuu? Huu ni ushauri wangu tu kwake na sio lazima yeye aufuate...
 
Huyu alidanganywa na ccm kwamba atakuwa Waziri wa fedha
 
Kumuheshimu mtu au kumdharau kutokana na mrengo wake kisiasa ni makosa. Kigezo kikuu ni anasaidiaje au kuipotoshaje jamii kupitia taaluma yake.
Upo sahihi sana mkuu, lakini ni wachache sana ndio wataweza kulielewa hili...
 
Kimei mwenyewe anajua heshima yake imeshuka kwa kiasi gani hadi sasa....na najua hakutegemea coz alitegemea apate uwaziri ambao unaendana na hadhi alokua nayo...saiz hana tofauti na jose msukuma
 
Asante kwa maoni yako lakini all in all angebaki kama mzee mshauri mtaalam ingefaa zaidi.
 
Kuna IGP au CDF aliyewahi kugombea nafasi ya kisiasa mkuu?...
 
Mwenyekiti wa Chama Mkoa mmojawapo alikuwa RPC,aligombea uenyekiti na akawashinda makada wengine!
RPC ni ngazi ya mkoa tu kama manager wa CRDB mkoa. Kimei ni top kama IGP
 
Haya bhana mimi nimemshauri tu kama mzalendo mwenzake
 
Duuuh, hii sijui mimi mkuu na sio lengo la mada hii...
 
Acheni mawazo ya kidikteta. Kila mtu haki ya kuamua maisha yake. Nyie makamanda uchwara mnajiona mnaweza kuamua Kimei aishi vipi?
Sasa mbona nawe unajipa usemaji wa familia ya kimei? Kwa nini unaamini upo karibu na kimei kuliko hata mkewe? Kutokuwa dikteta ni kuacha mtu aongee anachotaka pasipo kuvunja sheria. Sasa unapomkataza mtu asiongee unaonesha una mawazo magonjwa.
 
Sasa mbona nawe unajipa usemaji wa familia ya kimei? Kwa nini unaamini upo karibu na kimei kuliko hata mkewe? Kutokuwa dikteta ni kuacha mtu aongee anachotaka pasipo kuvunja sheria. Sasa unapomkataza mtu asiongee unaonesha una mawazo magonjwa.
Wapi nimejipa usemaji wa hiyo familia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…