Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

1. Charles Kimei kama Mtanzania yeyote ana haki ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote cha siasa, au kutojiunga,ana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, au kuomba kuchaguliwa.

2. Charles Kimei kwangu mimi hakuwa na integrity yoyote ya maana. Alisema anamuogopa Magufuli sana na atafanya chochote Magufuli atakachosema.

Kauli hii kutoka kwa mtu mume inawekea shaka utu wake na uanaume wake. Kutoka kwa CEO wa Benki, inatilia shaka integrity ya benki hiyo.

Maana ni kama alisema kwamba Magufuli angetaka kuiba hela za CRDB aende kuzitumia kwenye uchaguzi, Kimei angekubali tu.

Hivyo sioni Kimei atapoteza integrity gani, wakati alikuwa hana integrity tangu mwanzo.
Viongozi wengi walio kuwa na nyadhifa za uteuzi wapo kisiasa na kwa maslahi ya waliowateua.

Ukifuatilia sanà,utagundua mpaka viongozi wa taasisi za vyombo vya dola wengine wamestaafu na kugombea nafasi za kisiasa.Kwa hiyo wengi wamo au wanatumikia siasa wakiwa katika nyadhifa za uteuzi.

Kwa suala la huyu ndugu hata zile fedha zilizokuwa na kashfa ya makampuni ya EPA zilipitia/ kupigwa katika taasisi aliyokuwa anaisimamia yeye, na hakuwahi kuzungumzia wala kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kashfa ile bali alikaa kimya au kuachwa na wakubwa!
Kwa hiyo hapo alipo ndipo anaona yupo salama na amani ndani ya nafsi yake(Sisi tunamtazama kitaaluma,lakini yeye binafsi anajitazama na kuishi kisiasa)!
 
Sioni tatizo sana. Anaweza kutumika vizuri tu kwa manufaa mapana ya nchi akiwa mbunge. Atapata fursa nzuri ya kushauri watunga sera kirahisi zaidi anapokuwa kwenye game.

Kumuheshimu mtu au kumdharau kutokana na mrengo wake kisiasa ni makosa. Kigezo kikuu ni anasaidiaje au kuipotoshaje jamii kupitia taaluma yake.

Sio wanachana wote wa chama kimoja wanakubaliana kwa kila kitu. Na motives za kujiunga na chama fulani zinatofautiana kati ya mtu na mtu. Ni mapema kuhukumu
 
Uzoefu wa wengi waliokuwa wafanyakazi wa mashirika na taasisi za umma, hujiunga na siasa na hasa na chama tawala kama kinga ya kutoweza kutakiwa kuwajibika kwa yale mapungufu ya yale walioyafanya katika taasisi waliokuwa wanaziongoza. Kimei is no exception!!
 
Mbona naye aliajiriwa?maneno kama hayo yanatakiwa yatoke kwa watu kama akina shabiby,msukuma,Abooud ,sylvester koka na wabunge wengine ambao mi wamefanikiwa katika biashara zao wenyewe.Hilo la kusema fundi simu nalo ni nadharia kama nadharia zingine.

amimi namshauri Raisi angeteua baadhi ya hawa matajiri kwenye wizara zile zinazihusika na uwekezaji,biashara na viwanda .Hata wakiwa wana negotiate mikataba wanakuwa wanaelewa kitu wanasema.siyo kutumia elimu ya darasanu waliosoma miaka 20 iliyopita.Trust me ukiwaweka profesor wa uchumi pamoja na Aboud yule wa Morogoro ,Aboud yuko mbali zaidi ki uelewa wa biashara.

Tukitaka mapinduzi ya kweli tuwaweke watu wenye uzoefu wa kukuza uchumi wa biashara zao katika nafasi za maamuzi.watakuwa na mchango mkubwa nakwambia. Hata kwenye madini naona kama yule waziri Doto ni kama anatosha tosha hivi huenda alishafanyabiashara ya madini.
 
Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

Wadau woooooote wa tasnia ya banking waliokuwa wanakupenda "unconditionally" sasa umewagawa. Nusu wapo na wewe na nusu nyingine wapo upande ule wa upinzani. Mzee toka kwenye siasa rudi kuwa mshauri katika taaluma yako.
Wewe huna uzalendo wala utu.

Ungekuwa na uzalendo ungechukia kila anayeharibi taifa hili na

Ungekuwa na utu ungechukia kila anayefanya mauaji ya Raia wasio na hatia.
 
Mambo vp JamiiForums.

Ninapoandika hoja hii, ninaomba ifahamike kuwa i have nothing personal with mzee Kimei na ninatambua kuwa yeye ni moja katika ya hazina kubwa ambazo taifa hili linazo katika masuala mazima ya uchumi na banking.

Watu walikuwa wanapenda sana kumshambulia kaka yangu Pascal Mayalla kuwa amejiingiza katika siasa kwa sababu ya njaa. Sasa huyu CEO mstaafu yeye ana njaa gani? Mzee Charles Kimei alipaswa kubaki kama mshauri wa masuala ya uchumi/banking hapa Tanzania/Africa Mashariki na sio kujiingia katika siasa hizi za vyama.

He is one of the most exposed and reputable top executives in banking and finance industry kwa hapa Tanzania na East Africa. Hakupaswa kuonesha mlengo wa wazi wazi wa chama chochote cha kisiasa kiwe upinzani au tawala.

Siasa hizi za vyama angewaachia mzee Dr. Bashiru Ally na Mheshimiwa Mbowe. Kimei angebaki kuwa kama William B. Harrison Jr. CEO mstaafu wa bank ya Marekani ya JPMorgan Chase ambaye sasa ni mshauri mwandamizi katika umoja wa The American Bankers Association (ABA)

William B. Harrison Jr.
=====

View attachment 1694756

Hata kama asingekuwa mbunge wa CCM akaamua kujiunga na CHADEMA, CUF au ACT, kitendo cha kujiingiza katika siasa za vyama kunampotezea intergrity yake aliyotumia nguvu kubwa na miaka mingi sana katika kuijenga kwenye tasnia ya masuala ya uchumi/banking.

Watumishi wa CRDB wenye mlengo tofauti wa kisiasa (upinzani) waliokuwa wanamuona kama role model wao sasa wataanza kuzozana naye hata kama sio face to face hata kupitia mitandao. Alistaafu kwa heshima nzuuuuri mzee wa watu, sasa anajiharibia heshima alipojiingiza kwenye siasa.

Achilia mbali CRDB, wale watumishi wa banks zingine waliokuwa wanamuona kama kioo bora kwa maana aliitoa CRDB kutoka kuwa bank ya kitanzania mpaka kufungua matawi yake nchi jirani, sasa nao atakuwa anajibizana nao kwa sababu za kisiasa. Yeye CCM wao wapinzani. Ipo wapi tena heshima ya mzee Kimei katika industry ya banking?

Kimei kwa levels zake angepaswa awe anaendesha kampuni kubwa sana ya masuala ya ushauri wa kiuchumi/kibank Africa Mashariki na sio kwenda bungeni kurushiana vijembe na wanasiasa ambao wengi ni umri wa watoto wake wa kuzaa, tena anawazidi mpaka exposure.

Kuna mada ilianzishwa humu kuhusiana na kauli yake moja ya kisiasa ( Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu? ) ambayo inaonekana imewakera wengi na watu wanamshambulia kweli kweli.

Mzee Kimei kwa sasa ni mwanasiasa wa mlengo wa chama tawala (CCM), ina maana watu waliokuwa wanamuheshimu kama CEO bora kwenye banking/uchumi ambao wapo mlengo wa siasa za upinzani sasa wataanza kumtukana na kumrushia maneno ya kejeli jambo ambalo mzee hakuwa na ulazima wa kulifanya.

Wapo watu watahoji mbona kuna professors na PhD holders wapo katika siasa miaka nenda rudi, lakini ni nani kama Kimei katika taaluma ya banking? Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Lengo lake lilikuwa kujakuwa waziri wa fedha pungufu balozi USA au Uingereza. Matarajio yake hayakutofautiana na mama Lwakatare aliyetarajia kuwa waziri wa elimu.
Je, swala la benki ya Geita lilimuacha salama?
 
Viongozi wengi walio kuwa na nyadhifa za uteuzi wapo kisiasa na kwa maslahi ya waliowateua.

Ukifuatilia sanà,utagundua mpaka viongozi wa taasisi za vyombo vya dola wengine wamestaafu na kugombea nafasi za kisiasa.Kwa hiyo wengi wamo au wanatumikia siasa wakiwa katika nyadhifa za uteuzi.

Kwa suala la huyu ndugu hata zile fedha zilizokuwa na kashfa ya makampuni ya EPA zilipitia/ kupigwa katika taasisi aliyokuwa anaisimamia yeye, na hakuwahi kuzungumzia wala kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kashfa ile bali alikaa kimya au kuachwa na wakubwa!
Kwa hiyo hapo alipo ndipo anaona yupo salama na amani ndani ya nafsi yake(Sisi tunamtazama kitaaluma,lakini yeye binafsi anajitazama na kuishi kisiasa)!
Halafu watu wanamsifia kwamba alikuwa role model mzuri, ila sasa kaharibu kuingia katika siasa.

Role model mzuri my foot!

Wengi wetu wana low standards na high tolerance for bullshit.

Kwa msingi huu, maendeleo ni kazi sana.
 
Wewe huna uzalendo wala utu.

Ungekuwa na uzalendo ungechukia kila anayeharibi taifa hili na

Ungekuwa na utu ungechukia kila anayefanya mauaji ya Raia wasio na hatia.
Mtu ambaye hana deep understanding ya issues ni vigumu kuwa mzalendo.

Hata pale anapotaka kuwa mzalendo kwa nia ya kweli.

He will back some hustling showman, thinking he is backing a true patriot.

The English have a saying.

The road to hell is paved with good intention.
 
"UDAKU":

Kwa siasa za sasa iliikuwa muhimu kwake kujipambanua mrengo wake na kuungana "nao" (hata kama kiroho hayupo nao!). Nje ya hapo, angepata tabu.

Kuna wale tunaoamini kuwa hakutoka crdb kwa "ridhaa yake"......tunahisi wenye nchi walimwambia atoke! Au alitoka kwa woga!
 
Mbona naye aliajiriwa?maneno kama hayo yanatakiwa yatoke kwa watu kama akina shabiby,msukuma,Abooud ,sylvester koka na wabunge wengine ambao mi wamefanikiwa katika biashara zao wenyewe.Hilo la kusema fundi simu nalo ni nadharia kama nadharia zingine.

amimi namshauri Raisi angeteua baadhi ya hawa matajiri kwenye wizara zile zinazihusika na uwekezaji,biashara na viwanda .Hata wakiwa wana negotiate mikataba wanakuwa wanaelewa kitu wanasema.siyo kutumia elimu ya darasanu waliosoma miaka 20 iliyopita.Trust me ukiwaweka profesor wa uchumi pamoja na Aboud yule wa Morogoro ,Aboud yuko mbali zaidi ki uelewa wa biashara.

Tukitaka mapinduzi ya kweli tuwaweke watu wenye uzoefu wa kukuza uchumi wa biashara zao katika nafasi za maamuzi.watakuwa na mchango mkubwa nakwambia. Hata kwenye madini naona kama yule waziri Doto ni kama anatosha tosha hivi huenda alishafanyabiashara ya madini.
Ni sawa na prof anayefundisha ujasiriamali wa vitu mbalimbali anajua theory kuliko experience ya Field sasa huyo akiwekwa mfano na muuza genge KWA biashara lazima amushinde so ni Bora kuwapa wazoefu wa Mambo ka ni biashara kuliko mtu wa too much theory .
 
Back
Top Bottom