Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Ndomaana nikasema hatua sitahiki zichukuliwe kwa wote waliohusika.Sipo hapa kusupport kilichotokea.
Kwa vurugu za chato anayepaswa kujisafisha ni rais, akikaa kimya atakuwa amechafuka vibaya.Kwa rais alipaswa kuwa mfano kufanikisha usalama wa kutosha unawepo Kwake kwa wagombea wenzie..
 
Tangu 1995 wapinzani wanatuhumiwa kuwa waleta fujo, vita na vurugu lakini hakuna ushahidi wa kumpopo au kupopoana kutoka kwao kwanda ccm.

Haya ya chato nayo ni ya aina yake.
 
Ni upuuzi kutowaandaa vijana wa cdm kujibu kwa namna hiyo hiyo kwa kujihami dhidi ya hao wapuuzi wa uvccm.Chadema muache unyumbu,watu wanawashambulia mnashindwa kujibu? Hili ni tukio takribani la 3
 
Mheshimiwa Tundu Lissu aamuru Barabara ya Chato Kufungwa baada ya wafuasi wa CCM kushambulia kwa mawe msafara wake na kuharibiwa gari la vifaa vya muziki (PA).
View attachment 1599022

Lissu ndio alikuwa wa kwanza kuzusha kuwa Rais kazomewa na asiwatishe wapiga kura hahaha leo hao wapiga kura nao wamemshambilia ana anza kulialia hahahaha
 
Lissu ameamua kufanya siasa za uchokizi, kutukanana, Nzega alivyo mtukana magufuli, alikuwa anapeleka ujumbe Chato kuwaomba wamshambulie, ili apate ajenda ya kuzungumzia kesho na keshokutwa. Apigwe tuu
 
Daaaah nilikua nasomaga kuhusu intarahamwe Sasa naona tumefika huko.

TISS lisaidieni TAIFA linapotea chini ya Meko
 
Huko jimboni kwa Lissu watu wanampenda Magufuli ndio maana hawakumrushia mawe. Ukisema kwamba hawakumrushia kwasababu ya mamlaka yake, Basi angalau hata wangemzomea tu....
Siyo hulka ya Watanzania kuwafanyia fujo wanasiasa wanaoomba kura. Ukiona fujo imefanyika ujue kuna watu na wanasiasa wa hovyo waliochochea, kuratibu na hata kuwezesha fujo. Wanasiasa wa aina hiyo hawatufai hata kidogo.
 
Sio kulaani tu, wagombea wangeenguliwa kabisa kutoka katika nafasi za kugombea, ila kwa sababu ni upinzani basi tume itabariki kila aina ya udhalimu unaofanywa dhidi ya wapinzani na hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya hao wahalifu
Wapinzani acheni kulia lia, juzi Kati hapa Magufuli alivamiwa na vijana wa Chadema kwenye kampeni huko Bukoba, Cha kushangaza viongozi wa Chadema ndo walikuwa wa Kwanza kushabikia hicho kitendo. Kama kweli mna nia njema mnatakiwa muwe wa Kwanza kukemea pale wanachama wenu wanapowafanyia viongozi au wanachama wa vyama vingine.
 
Huko jimboni kwa Lissu watu wanampenda Magufuli ndio maana hawakumrushia mawe. Ukisema kwamba hawakumrushia kwasababu ya mamlaka yake, Basi angalau hata wangemzomea tu...

Hata kwa Waziri mkuu wagombea wa upinzani walitekwa na kupigwa sana ili waziri mkuu apite bila kupingwa. Hayo ndio maagizo ya viongozi wa amani hii.
 
Halafu viongozi wa dini wanamrambamramba miguu jpm.siwapendi wale viongozi wa dini hatarii
Unakosa heshma unaposema "viongozi wa dini , hapanaa , wale ni "masadukayo na mafarisayo, wanafiki waliopo kushibisha matumbo yao na kudhulumu wajane kuwaambia wauze kila kitu ili wamtumikie mungu ilhali wao wanakula kondoo za Bwana".

Viongozi wa Kiroho hawawezzi kuwa wanafki na kukaa upande wa wakandamizaji, never!
 
Mshkaji wamempopoa na mawe, katoka katoro kwenda kwenye mkutano chato. Shida hapo atajitibia mwenyewe wala sidhani kama lissu atakuwa tena na habari nae

Ni wangapi wame umizwa na Visa vya Dunia hii ili wewe uwe kama hivyo ulivyo Mkuu !?..Au unafikiri hakuna wanao hatarisha Maisha yao kwa ajili yako !?
 
Dunia inashuhudia huu ubaribariki wa baadhi ya watanzania.
Imeonya kabla na sidhani kama kuna watakacho onya tena. Ni bahati mbaya kwa taifa kuwa na aina hii ya uhuni. Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Back
Top Bottom