Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Lissu na Chato wapi na wapi wacha yamkute analeta siasa za majitaka wacha chato wamfundishe tena wampige mawe haswaa
Tumia Busara broo.

Mtumzima matured anajua jinsi ya kuzuia Hisia na kutumia akili badala yake
 
Lissu na Chato wapi na wapi wacha yamkute analeta siasa za majitaka wacha chato wamfundishe tena wampige mawe haswaa
Siasa za majitaka hizo mkuu. Tangu lini mgombea wa urais akapangiwa ni wapi asifike? Sasa mmeshaishiwa mbinu na hoja za majukwaani eti unasema Tundu Lissu wapi na wapi Chato? Hivi unajielewa kweli au unafuata mkumbo tu? Nyie subirini tu 28 tuna jambo letu hakika hamtaamini enyi banyamulenge.
 
Lissu na Chato wapi na wapi wacha yamkute analeta siasa za majitaka wacha chato wamfundishe tena wampige mawe haswaa
Kwani chato siyo Tanzania. Magufuli hajapita ikungi wiki iliyopita na hajasumbuliwa na mtu yeyote? Mkiambiwa mnatumia NGUVU kushinda mapovu pipa. Pumbavu.
 
Kwa vurugu za chato anayepaswa kujisafisha ni rais, akikaa kimya atakuwa amechafuka vibaya.Kwa rais alipaswa kuwa mfano kufanikisha usalama wa kutosha unawepo Kwake kwa wagombea wenzie..
Ni kweli mkuu.
 
Mkuu kukubalika mimi pia sikatai lakini kurusha mawe huo ni ushenzi na uhuni wa hali ya juu na unapaswa kukemewa.
Wewe unadhani magufuli anakubalika sehemu zote kwa 100%?
Hicho kitendo sijakisapoti hata kidogo, na Wala siwezi kushangilia Jambo Kama hilo, maana hata ningekuwa mimi nisingefurahia.Ndomaana nikasema Hatua Kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waliohusika.

Hakuna sehemu ambayo mtu anaweza kukubalika kwa 100%,hata kwenye level ya kifamilia huenda zisifike mia 😃,na sidhani Kama nimekuja na hoja ya namna hii.
 
Hii nchi siyo ya watu wa Chato peke yake, hii Nchi ya wote na kila mmoja anatakiwa awe anaishi na anaenda kwa amani mahali kokote nchini.

Mgawanyo wanini sasa?
Well siku ukiitwa BBC kuwaelezea hayo malalamiko yako usisahau kuwauliza kwanini unionist awaendi maeneo ya separatist kwenye campaign za siasa huko North Ireland na wakati ni haki ya mgombea kwenda popote kwa taifa linalojidai ku promote democracy duniani.

Ni hivi Lissu anayo haki ya kwenda popote ndani ya Tanzania lakini kuna maeneo anajua wazi hana hiyo support na kwenda huko kumtukana Magu kama anavyofanya kwingine he wont be well received it’s just common sense, sasa anaenda fanya nini kama sio kutafuta kilichotokea.

Tatizo lenu Chadema mnapenda hype sana za mitandaoni kibaya zaidi baadhi yenu mnaishia kuamini your own hype, ndio hiki kilichomfanya Lissu aamini anaweza enda mtukana Magufuli in his own backyard na akashangiliwa.
 
Hata kwa Waziri mkuu wagombea wa upinzani walitekwa na kupigwa sana ili waziri mkuu apite bila kupingwa. Hayo ndio maagizo ya viongozi wa amani hii.
Mmmh, hilo mimi sina uhakika nalo Wala ushahidi wowote, kwahiyo siwezi kujadili chochote.
 
Siyo hulka ya Watanzania kuwafanyia fujo wanasiasa wanaoomba kura. Ukiona fujo imefanyika ujue kuna watu na wanasiasa wa hovyo waliochochea, kuratibu na hata kuwezesha fujo. Wanasiasa wa aina hiyo hawatufai hata kidogo.
Huenda ikawa kama unavyowaza,na kama ndivyo basi viongozi wa namna hiyo hawawezi kutufaa kwa namna yoyote ile.
 
Lissu ameamua kufanya siasa za uchokizi, kutukanana, Nzega alivyo mtukana magufuli, alikuwa anapeleka ujumbe Chato kuwaomba wamshambulie, ili apate ajenda ya kuzungumzia kesho na keshokutwa. Apigwe tuu
Alimtukanaje?
 
Mkapiga risasi Singida tukanyamaza leo mnapiga mawe kila mtu abaki na nchi yake
 
Huyu msaliti na kibaraka hapaswi kupewa nafasi kuendelea kupanda mbegu za chuki miongoni mwa watanzania, asubiri kipigo cha kura kiduchu ndiyo ataelewa this is Tanzania
Kama kweli ni kibaraka wa Wazungu basi ccm mnapoteza muda wenu bure...
Ikulu mtatoka mbio Kama Kuna nyuki
 
Ku attack msafara wa mgombea yeyote sio jambo la kiungawana.

Lakini lazima uulize akili za strategist wa CDM kuna ulazima gani wa kumpeleka Lissu Chato?

This is just a provocation kwa watu wa Chato mambo mengine ni ya kujitakia anawapa walinzi wake binafsi na jeshi la polisi kazi ya ziada wakati mwingine.
What happened to JPM when was in Singida?
 
Lissu na Chato wapi na wapi wacha yamkute analeta siasa za majitaka wacha Chato wamfundishe
Kwa nini mnapenda vurugu?nyie ndio chanzo cha kuvuruga amani, na machafuko ndani ya nchi hii yataanzishwa na nyinyi, nashangaa sijui kwa nini vyombo vya Dora vinawakumbatia
 
Lisu anachokitafta atakipata very soon! Maana asidhanie matusi na maneno anayotumia kila mtu anao uvumilivu.

Mbona tunatazama na kusikiliza hotuba za Tundu Lissu kila mahali hatuyaoni hayo matusi?

Nyie mnamsikiliza Tundu Lissu gani labda?

Sema kwa miaka mitano hamkuzoea kukutana na ukosoaji Mkubwa na wa maneno makali kiasi ambacho kwenu mnatafsiri kuwa ni matusi..!!

Hakuna matusi bwashee hapo. Ni kwa sababu tu Tundu Lissu ana break off TABOOS na TRADITIONS mbovu za kutokoselewa kwa mfalme. Sasa hili linaonekana ni geni kwenu. Haraka haraka nyie mnasema haya ni matusi!!

Poleni sana
 
Back
Top Bottom