CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Jamani Mimi naomba mnitoe kwenye mambo zenu za siasa za bongo. Nitauliza maswali nitaomba wajibu wenye kufikiria tu.

Hivi ile hali kama ya Italy ikija Kwetu (God forbid) bado tutasema hivi hivi kwamba sisi tukijifungia ndani hatuwezi kuishi??

Hivi hali ikija km USA sasa je tutakua tunachapa kazi tu ili majirani zetu wapate huduma?
Trump mpk leo wazi wazi ametamka hii kujifungia ndani sitaki kusikia. Na alisema kabisa Easter ntafungua nchi watu wafanye kazi. Lakini Easter ndio hiyo death rate ina surge tu day in day out. Je mbona Trump hafungui nchi? Si hapendi?! Kama ambavo na sisi hatupendi. Kwa wenye kufikiria hapa waseme kwa nini lockdown marekani ipo wakati Raisi roho yake inamuuma uchumi unashuka? Kwa nini?
 
Wakati wa Kikwete mlisema hakuna Rais wa Hovyo kama huyu mpaka mkadai mnataka Rais Dikteta sio huyu anayechekacheka. Leo mnadai hakuna Rais mshamba kama Magufuli. Tena sasa hivi mnasema eti Kikwete alikuwa 'bonge' la president. Sasa niwaambie; Watanzania sio nyumbu kama ninyi. Subirini kwenye uchaguzi wa Oktoba ndio mtajua Watanzania wana akili kuliko mfikiriavyo.
 
Sarcastic! Hivi Raising wenu huko sijui wapi anajua maana ya neno Sarcasm.
 
Hii nchi hatupo seriaz saiv tunapeana kauli za kishujaa

Yakifika kama ya Italy na Spain tutaanza kuuza kesi kwa Mabeberu na wapinzani
 
Nipo napiga picha kwenye mawe na kunywa kahawa kwenye vijiwe pigeni kazi.
 
Wajua hapa Malawi tumekuwa DONOR country tangu 2015 kwahiyo huo ugonjwa umeletwa na mabeberu na kama ujuavyo sisi hatuogopi mabeberu na tunachapa kazi kama inavyotuchapa sisi.
Mungu ibariki Malawi na nyinyi Tanzania endeleeni kuogopa CORONA sisi hapa job tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
8
T
That's My President; ever confident!
 
Walivyofanya Corona imeisha kwao?

Kila mtu ana mfumo wa ku deal na matatizo yake, hivi unataka kusema wewe na rais nani mwenye ACCESS mzuri wa kupata habari kuhusiana ukubwa au udogo wa hili tatizo?
katika zama hizi kitu pekee kinachoweza kufichika kisijulikane na Mtanzania wa kawaida ni ufisadi unaofanywa na watumishi wa umma kupitia miradi ya mabilioni na matrilioni ambayo CAG kakatazwa kufanya ukaguzi. bila kusahau mipango ya kidhalimu inayofanywa na "watu wasiojulikana" - hii mwananchi wa kawaida haijui kweli.

mengine yote (likiwemo kujua ukubwa wa tatizo la korona) yapo wazi. yapo wazi kama lilivyokuwa suala la korosho ambalo wananchi tulikuwa more informed kuliko serekali kuhusu madhara ya state kuingilia supply chain framework.

kwa taarifa yako tu, COVID-19 detection rate hapa Tanzania Bara ni ndogo sana ukilinganisha na nchi zinazoizunguka in demographically relative terms.

Tanzania Bara ndiyo the most populated kulinganisha na majirani zake, yet detection rate ipo very low. this beats logic in its entirety kwani si kwamba Tanzania Bara ina mikakati yoyote iliyo imara kuliko majirani zake hawa katika kupunguza maambukizi, hasha, bali Watz msiojitambua mpo mpo tu kama misukule mkikubali kulishwa contradictions za kina Bashite ambaye asubuhi atasema hili na jioni anapiga u-turn kuhusu jambo lile lile. kwenye kundi hili wengine hatumo!

hii ina maana moja tu... kuwa Tanzania Bara kuna usiri mkubwa sana kuhusu janga hili, which's going to be a costly gamble in the long run.

kimahesabu, kwa kigezo cha detection rate ya Zanzibar yenye population ya wakaazi 700,000, kadirio sahihi la Corona cases huku Tanzania Bara ni wagonjwa over 500 huko.
 
Ushamba na kuchanganyikiwa ndiyo huu. Nchi unazodai zinakutegemea zimefunga mipaka wewe unanitutumua kuwa zinakutegemea.

Sababu halisi ni kuwa tumechelewa kufunga mipaka. Soon majirani zetu watapiga marufuku mtanzania yeyote kuingia kwao kwa sababu ya uzembe tulio nao kwenye hii crisis.

Majirani zetu wote wanahamasisha kupunguza misongano sisi tunahamasishwa tukakusanyike makanisani na misikitini na mabarabarani tukichapa kazi.

Sina uhakika kama kauli kama hii ilipaswa kutolewa wakati kama huu. Sijui pia kama tutatoboa bila kuacha maangamizi kwenye hii nchi. Kisha tutakuja kumsingizia Mungu kuwa ndiye kapanga. Mungu wetu hayuko hivyo.
 
Hivi raisi akikosea, ni lazima mokosee naye? Hamuoni kuwa hapo amepotea njia kabisa? Subirini tuangamie maana COVID-19 imepoga hodi kwa nguvu sasa!
 
Kwahiyo sisi tufe kwaajiri ya kutetea nchi 8!?
Yaani igekuwa heri corona ingekata kona kama risasi ivyokata kona kwa dadaetu mpendwa Akwina R. I. P. Iende kwa wanaowazia kodi na ushuru na siyo afya na maisha ya watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu ibariki Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…