Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Utawala unafuta fao la kujitoa huku wabunge wakipewa mafao yao yote baada ya miaka 5 pia wabunge wanaunga juhudi halafu unarudia uchaguzi kwa gharama..kwa kweli kwa huo utawala hapanaaaa.
 
Lissu Sasahivi anaitwa Chiba,by Zitto 🤣🤣🤣
 
Nabii Mussa wa wapi?. Mtu anabagua kundi fulani na kuliona halistahili ndio awe Mussa?. Mlimuita yesu ila haikutosha.
Hata kwa nabii Musa kulikuweko na makundi mawili, kulikuweko na kundi la Kola ambalo lilipingana na Musa,hivo hatushangai kumpinga Magufuri,hakuna jambo jipya hapa chini ya jua
 
Magufuli ndio Rais aliyeijenga miundombinu ya hii nchi kuliko Rais mwingine yeyote. Hutaki acha.
 
Mitaani kwa wananchi bado ana nguvu kubwa sana usifikiri serikali nzima kwenda Chato hawajui wanalofanya.

..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.

..serikali nzima ilikuwa huko, lakini unadhani awamu ya 6 inamjali Magufuli na itaendeleza U-magufuli?
 
..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.

..serikali nzima ilikuwa huko, lakini unadhani awamu ya 6 inamjali Magufuli na itaendeleza U-magufuli?
Awamu ya 6 haiwezi U-Magufuli
 
Jpm alikufa 12-03-2021
 
Wananchi wameloweshwa na mvua wao mvua haikuwagusa!! Hapo chacha
 
..Magufuli hana nguvu tena, amebaki historia.
..Na aliyemrithi haamini ktk U-magufuli.
Watu wanaonyesha nguvu ya magufuli katika vitu si rekodi yake kwa ujumla
Rekodi ya JPM inatetewa na flyover, barabara, majengo n.k.

Rekodi yake ingeangaliwa katika maeneo yafuatayo ili tumtendee haki

Utu
Ukweli
Haki za binadamu
Umoja wa Kitaifa
Ukanda/Ukabila/Udini
Nepotism (undugu)
Uhuru wa habari
Demokrasia
Utawala wa sheria
Taasisi za nchi
Mahusiano ya Kimataifa
 
Kufungua daftari la Watanzania wenzetu wengi waliokimbia nchini kuhofia maisha yao na familia zao na kwenda kuishi kwa kuombaomba wakati yeye na viongozi wengine wakiongopa kuwa Tanzania kuna Amani,Demokrasia n.k Aibu sana
 
..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.
Wamekataa siasa na mahusiano ya kujifungia sasa wanafungua nchi
Wamekataa sera za uchumi (Miwgulu na Mabenki)
n.k.
 
Nipe tathimini ya kiuchumi ya ilo daraja refu la busisi , au huko linako elekea Kuna resources gani ambayo itainua uchumi wetu, otherwise ni zawadi kwa mkwe wake kama wanavyosema wengi
Zawadi kwa nani tena ? Usiwe unakuja tu hapa unaandika huu ushubwada wako.

Daraja la Busisi ni kiunganishi kwa kanda ya ziwa nzima na nchi jirani hasa Uganda, Rwanda na hata Burundi. Vile vile kupitia hapa tunaweza pitisha mizigo yetu kwa wingi zaidi kama tutakuwa na eneo la uwekezaji la kimkakati hasa viwanda vinavyokidhi mahitaji yetu wenyewe na hata ya wale walio nje ya nchi.

Mfano, viwanda vya nguo, viwanda vya ngozi, viwanda vya chuma hasa nondo na bati, maghala ya chakula ya kitaifa na maghala ya mafuta hasa ukizingatia tupo karibu na Rwanda na Kongo mashariki ambao wote ni landlocked na wanategemea bidhaa na huduma mbalimbaliu muhimu kutoka kwetu
 
 
Mimi Magufuli sitamsahau kwa alivyotufanyia kwenye ofisi yetu, akabadilisha direction yote. Kuondoka kwake at least kulinifanya nijue Mungu wa kweli yupo ambaye sio mnafiki Kama mwanadamu.

Mlikuwa mnaelekea wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…