Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Chato: Yaliyojiri katika Maadhimisho ya mwaka 1 wa kifo cha Hayati Magufuli. Kasala, tusimamie ukweli na haki. Samia kuendeleza Mema

Utawala unafuta fao la kujitoa huku wabunge wakipewa mafao yao yote baada ya miaka 5 pia wabunge wanaunga juhudi halafu unarudia uchaguzi kwa gharama..kwa kweli kwa huo utawala hapanaaaa.
 
Wakati Lissu analimwa risasi wafuasi wa Magufuri walishangilia wakijua Lissu atakufa wakaongea kila aina ya kejeli. Cha kushangaza Lissu hakufa, akawa hai. Huo ulikuwa ushindi mkubwa kwa Lissu dhidi ya Magufuri. Muuaji kafa mwenyewe, kamuacha aliyetaka kumuua.
Lissu Sasahivi anaitwa Chiba,by Zitto 🤣🤣🤣
 
Nabii Mussa wa wapi?. Mtu anabagua kundi fulani na kuliona halistahili ndio awe Mussa?. Mlimuita yesu ila haikutosha.
Hata kwa nabii Musa kulikuweko na makundi mawili, kulikuweko na kundi la Kola ambalo lilipingana na Musa,hivo hatushangai kumpinga Magufuri,hakuna jambo jipya hapa chini ya jua
 
Unaongea kana kwamba Tanzania ilianza mwaka 2015. Mimi nilimshangaa Magufuri alipomponda Nyerere kwanini akujenga ukuta wa mererani mwaka 1961. Bila kufahamu Tanzanite imevumbuliwa miaka ya 80 mwishoni. Yani wenyewe wanaichukulia Tazania ya 1960 ndio Tanzania ya 2015.
Magufuli ndio Rais aliyeijenga miundombinu ya hii nchi kuliko Rais mwingine yeyote. Hutaki acha.
 
Mitaani kwa wananchi bado ana nguvu kubwa sana usifikiri serikali nzima kwenda Chato hawajui wanalofanya.

..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.

..serikali nzima ilikuwa huko, lakini unadhani awamu ya 6 inamjali Magufuli na itaendeleza U-magufuli?
 
..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.

..serikali nzima ilikuwa huko, lakini unadhani awamu ya 6 inamjali Magufuli na itaendeleza U-magufuli?
Awamu ya 6 haiwezi U-Magufuli
 
Hii tarehe Nina mashaka nayo.

Kabla ya tarehe 17 mwezi wa 3 kufika siku tatu nyuma niliona mizinga na wanajeshi wakitokea bagamoyo na kuelekea DAR.

Na mizinga hyo hyo ndo ilitumika kwenye kumuaga magufuli pale uwanjani.

Swali walikuwa keshakufa au walijua kuwa atakufa?wakajiandaa mapema
Jpm alikufa 12-03-2021
 
Mangula kasema leo hakuna aliepewa kadi ya mwaliko wote waliokuwepo pale ni kwa upendo na mvua ikawanyeshea lakini wakakaa bado japo wapate maneno ya faraja iliwapunguze machungu yao….

Mimi binafsi yangu kwa leo Jaji Mkuu, Mpango na Mangula ndio walionifariji…
Wananchi wameloweshwa na mvua wao mvua haikuwagusa!! Hapo chacha
 
..Magufuli hana nguvu tena, amebaki historia.
..Na aliyemrithi haamini ktk U-magufuli.
Watu wanaonyesha nguvu ya magufuli katika vitu si rekodi yake kwa ujumla
Rekodi ya JPM inatetewa na flyover, barabara, majengo n.k.

Rekodi yake ingeangaliwa katika maeneo yafuatayo ili tumtendee haki

Utu
Ukweli
Haki za binadamu
Umoja wa Kitaifa
Ukanda/Ukabila/Udini
Nepotism (undugu)
Uhuru wa habari
Demokrasia
Utawala wa sheria
Taasisi za nchi
Mahusiano ya Kimataifa
 
Kuwatetea mama ntilie, machinga, bodaboda na wenye shughuri ndogondogo, ni sehemu ya kuwafanya watu wengi kuwa wazalishaji na si kuwa tegemezi
Lakini pia, ni kutengeneza watu wengi kuwa walipa kodi na nchi kuwa na maendeleo

Unapowafukuza hao watu bila kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia kazi, ni kuwafanya wawe tegemezi, kitu ambacho kinawafanya watu wachache kuwa ndio wazalishaji na wengi kuwa kama kupe!

Pumzika kwa amani hayati JPM
Kufungua daftari la Watanzania wenzetu wengi waliokimbia nchini kuhofia maisha yao na familia zao na kwenda kuishi kwa kuombaomba wakati yeye na viongozi wengine wakiongopa kuwa Tanzania kuna Amani,Demokrasia n.k Aibu sana
 
..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.
Wamekataa siasa na mahusiano ya kujifungia sasa wanafungua nchi
Wamekataa sera za uchumi (Miwgulu na Mabenki)
n.k.
 
Nipe tathimini ya kiuchumi ya ilo daraja refu la busisi , au huko linako elekea Kuna resources gani ambayo itainua uchumi wetu, otherwise ni zawadi kwa mkwe wake kama wanavyosema wengi
Zawadi kwa nani tena ? Usiwe unakuja tu hapa unaandika huu ushubwada wako.

Daraja la Busisi ni kiunganishi kwa kanda ya ziwa nzima na nchi jirani hasa Uganda, Rwanda na hata Burundi. Vile vile kupitia hapa tunaweza pitisha mizigo yetu kwa wingi zaidi kama tutakuwa na eneo la uwekezaji la kimkakati hasa viwanda vinavyokidhi mahitaji yetu wenyewe na hata ya wale walio nje ya nchi.

Mfano, viwanda vya nguo, viwanda vya ngozi, viwanda vya chuma hasa nondo na bati, maghala ya chakula ya kitaifa na maghala ya mafuta hasa ukizingatia tupo karibu na Rwanda na Kongo mashariki ambao wote ni landlocked na wanategemea bidhaa na huduma mbalimbaliu muhimu kutoka kwetu
 
Waliifuta mkuu.
1. Daraja la Tanzanite Dar
2. Mikataba ya madini
3. Ukuta wa mererani
4. Utumbuaji
5. Uzinduzi wa malipo ya serikali kupitia control number
5. Umeme wa Tsh 27,000/=
6. Elimu bure darasa la kwanza hadi form four
7. Ukarabati wa. Viwanja vya ndege na meli
8. Bomba la mafuta Hoima kwenda Tanga
9. Kuanzisha Tarura, Latra,
10. Kununua radar kwenye viwanja vya ndege vyote.
11. Kuivunja bodi ya ununuzibwa madini
12. Kuanzisha tume ya madini na madoko ya kuuzia madini
13. Kuvunja Jiji la Dar es salaam
14. Kumfukuza kazi Nape mnauye, mchechu wa NHC,
15. Kwa miaka mitano kutokwenda ulaya
16. Kuzirudisha halmashauri zote ofisi ya Rais.
17. Kuondoa watu wenye vyeti feki kwenye mfumo wa mishahara ya serikali.
18. Kukarabati shule za serikali za zamani
19. Kununua ndege mpya 11
20. Kufufua reli ya Dar to arushaTanzania
21. Kukarabati bandari ya mtwara, tanga na Dar
22. Kukusanya na kuzitambua mali za CCM
23. Kuanzishwa wizara mpya ya Madini
24. Miaka mitano umeme haujawahi kukatika
25.ujenzi wa hospitali za kanda, mikoa na wilaya
26. Ujenzi wa mshakama za wilaya
27. Kuongeza idadi ya hifadhi za tsifa na jeshi usu.
28. Kufuta mishahara ya 45,000,000
29. Kuongeza viwanda nchini
30. Kuwaeleza ukweli watanzania kuhusu covid 19
31. Kupunguza urasimu kwa watumishi wa umma
32. Kuanxisha ofisi za msajili wa hati za ardhi kila mkoa na kufuta ofisi za kanda
33. Kukamata wakwepa ushuru
34. Kampuni ya Halotel ya JK , wabia wake kwenda segerea kwa kutokulipa kodi
35. Serikali kununua magari yake kwa mfumo maalumu kupunguza madalali
36. Kiswahili kuanza kutumika mahakamani kutolea hukumu
37. Kuanzisha mji mkuu Dodoma.
38. Ujenzivwa uwanja wa ndege wa msalato.
39. Uzambazaji wa maji jiji la arusha, mradi wa bilion 500
40.…..,, Samia haya niliyoyataja anayaweza kuyasimamia?kuyaendeleza?kubuni vingine ? CCM tujiuliza maswali kabla hatujamwambia Samia achukue fomu 2025
 
Mimi Magufuli sitamsahau kwa alivyotufanyia kwenye ofisi yetu, akabadilisha direction yote. Kuondoka kwake at least kulinifanya nijue Mungu wa kweli yupo ambaye sio mnafiki Kama mwanadamu.

Mlikuwa mnaelekea wapi
 
Back
Top Bottom