Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lissu Sasahivi anaitwa Chiba,by Zitto 🤣🤣🤣Wakati Lissu analimwa risasi wafuasi wa Magufuri walishangilia wakijua Lissu atakufa wakaongea kila aina ya kejeli. Cha kushangaza Lissu hakufa, akawa hai. Huo ulikuwa ushindi mkubwa kwa Lissu dhidi ya Magufuri. Muuaji kafa mwenyewe, kamuacha aliyetaka kumuua.
Hata kwa nabii Musa kulikuweko na makundi mawili, kulikuweko na kundi la Kola ambalo lilipingana na Musa,hivo hatushangai kumpinga Magufuri,hakuna jambo jipya hapa chini ya juaNabii Mussa wa wapi?. Mtu anabagua kundi fulani na kuliona halistahili ndio awe Mussa?. Mlimuita yesu ila haikutosha.
Magufuli ndio Rais aliyeijenga miundombinu ya hii nchi kuliko Rais mwingine yeyote. Hutaki acha.Unaongea kana kwamba Tanzania ilianza mwaka 2015. Mimi nilimshangaa Magufuri alipomponda Nyerere kwanini akujenga ukuta wa mererani mwaka 1961. Bila kufahamu Tanzanite imevumbuliwa miaka ya 80 mwishoni. Yani wenyewe wanaichukulia Tazania ya 1960 ndio Tanzania ya 2015.
Nguvu ya JPM ni kubwa sana mitaani otherwise kama upo ughaibuni haupati feedback ya moja kwa moja toka uswahilini.Tanzania ina watu zaidi ya Milioni 45. Kwanini unadhani maelfu ya chato ni kigezo cha kukubalika?
Je, ni kiasi gani hawamkubali?
JokaKuu Pascal Mayalla
Nguvu ya JPM ni kubwa sana mitaani otherwise kama upo ughaibuni haupati feedback ya moja kwa moja toka uswahilini.
Mitaani kwa wananchi bado ana nguvu kubwa sana usifikiri serikali nzima kwenda Chato hawajui wanalofanya.
Mitaani kwa wananchi bado ana nguvu kubwa sana usifikiri serikali nzima kwenda Chato hawajui wanalofanya.
Awamu ya 6 haiwezi U-Magufuli..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.
..serikali nzima ilikuwa huko, lakini unadhani awamu ya 6 inamjali Magufuli na itaendeleza U-magufuli?
Jpm alikufa 12-03-2021Hii tarehe Nina mashaka nayo.
Kabla ya tarehe 17 mwezi wa 3 kufika siku tatu nyuma niliona mizinga na wanajeshi wakitokea bagamoyo na kuelekea DAR.
Na mizinga hyo hyo ndo ilitumika kwenye kumuaga magufuli pale uwanjani.
Swali walikuwa keshakufa au walijua kuwa atakufa?wakajiandaa mapema
Wananchi wameloweshwa na mvua wao mvua haikuwagusa!! Hapo chachaMangula kasema leo hakuna aliepewa kadi ya mwaliko wote waliokuwepo pale ni kwa upendo na mvua ikawanyeshea lakini wakakaa bado japo wapate maneno ya faraja iliwapunguze machungu yao….
Mimi binafsi yangu kwa leo Jaji Mkuu, Mpango na Mangula ndio walionifariji…
Watu wanaonyesha nguvu ya magufuli katika vitu si rekodi yake kwa ujumla..Magufuli hana nguvu tena, amebaki historia.
..Na aliyemrithi haamini ktk U-magufuli.
HakunaUseme, ilikuwa lini ulikatika ikapita siku nzima na ikawa mfululizo na hatimaye mgao?
Kufungua daftari la Watanzania wenzetu wengi waliokimbia nchini kuhofia maisha yao na familia zao na kwenda kuishi kwa kuombaomba wakati yeye na viongozi wengine wakiongopa kuwa Tanzania kuna Amani,Demokrasia n.k Aibu sanaKuwatetea mama ntilie, machinga, bodaboda na wenye shughuri ndogondogo, ni sehemu ya kuwafanya watu wengi kuwa wazalishaji na si kuwa tegemezi
Lakini pia, ni kutengeneza watu wengi kuwa walipa kodi na nchi kuwa na maendeleo
Unapowafukuza hao watu bila kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia kazi, ni kuwafanya wawe tegemezi, kitu ambacho kinawafanya watu wachache kuwa ndio wazalishaji na wengi kuwa kama kupe!
Pumzika kwa amani hayati JPM
Wamekataa siasa na mahusiano ya kujifungia sasa wanafungua nchi..wanateua watu waliokataliwa na Magufuli, halafu wanakwambieni wanamuenzi Magufuli.
Zawadi kwa nani tena ? Usiwe unakuja tu hapa unaandika huu ushubwada wako.Nipe tathimini ya kiuchumi ya ilo daraja refu la busisi , au huko linako elekea Kuna resources gani ambayo itainua uchumi wetu, otherwise ni zawadi kwa mkwe wake kama wanavyosema wengi
Jpm alikufa 12-03-2021
Waliifuta mkuu.
1. Daraja la Tanzanite Dar
2. Mikataba ya madini
3. Ukuta wa mererani
4. Utumbuaji
5. Uzinduzi wa malipo ya serikali kupitia control number
5. Umeme wa Tsh 27,000/=
6. Elimu bure darasa la kwanza hadi form four
7. Ukarabati wa. Viwanja vya ndege na meli
8. Bomba la mafuta Hoima kwenda Tanga
9. Kuanzisha Tarura, Latra,
10. Kununua radar kwenye viwanja vya ndege vyote.
11. Kuivunja bodi ya ununuzibwa madini
12. Kuanzisha tume ya madini na madoko ya kuuzia madini
13. Kuvunja Jiji la Dar es salaam
14. Kumfukuza kazi Nape mnauye, mchechu wa NHC,
15. Kwa miaka mitano kutokwenda ulaya
16. Kuzirudisha halmashauri zote ofisi ya Rais.
17. Kuondoa watu wenye vyeti feki kwenye mfumo wa mishahara ya serikali.
18. Kukarabati shule za serikali za zamani
19. Kununua ndege mpya 11
20. Kufufua reli ya Dar to arushaTanzania
21. Kukarabati bandari ya mtwara, tanga na Dar
22. Kukusanya na kuzitambua mali za CCM
23. Kuanzishwa wizara mpya ya Madini
24. Miaka mitano umeme haujawahi kukatika
25.ujenzi wa hospitali za kanda, mikoa na wilaya
26. Ujenzi wa mshakama za wilaya
27. Kuongeza idadi ya hifadhi za tsifa na jeshi usu.
28. Kufuta mishahara ya 45,000,000
29. Kuongeza viwanda nchini
30. Kuwaeleza ukweli watanzania kuhusu covid 19
31. Kupunguza urasimu kwa watumishi wa umma
32. Kuanxisha ofisi za msajili wa hati za ardhi kila mkoa na kufuta ofisi za kanda
33. Kukamata wakwepa ushuru
34. Kampuni ya Halotel ya JK , wabia wake kwenda segerea kwa kutokulipa kodi
35. Serikali kununua magari yake kwa mfumo maalumu kupunguza madalali
36. Kiswahili kuanza kutumika mahakamani kutolea hukumu
37. Kuanzisha mji mkuu Dodoma.
38. Ujenzivwa uwanja wa ndege wa msalato.
39. Uzambazaji wa maji jiji la arusha, mradi wa bilion 500
40.…..,, Samia haya niliyoyataja anayaweza kuyasimamia?kuyaendeleza?kubuni vingine ? CCM tujiuliza maswali kabla hatujamwambia Samia achukue fomu 2025
Mimi Magufuli sitamsahau kwa alivyotufanyia kwenye ofisi yetu, akabadilisha direction yote. Kuondoka kwake at least kulinifanya nijue Mungu wa kweli yupo ambaye sio mnafiki Kama mwanadamu.
Mimi nauzungumza ukweli wa Jiwe kuwa alikuwa muovu lakini tushukuru Mungu kwa kumuondoaSasa kama unajua hivyo kwanini unasema kama vile wewe utaishi milele?
Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app