Chawa wa Mama wamemgeuka Salim Kikeke; wamempora nafasi yake wamempa Mobhare Matinyi

Chawa wa Mama wamemgeuka Salim Kikeke; wamempora nafasi yake wamempa Mobhare Matinyi

Hahaha msemaji anapika ugali kwenye kigeto London.Jamani si kila alieko Ulaya mambo safi. Kwanza mji wa London ni ghali sana tena sana.
Uafrika hasa utanzania ni laana

Salim kikeke alifanya makosa makubwa sana kurudi kwenye Laana.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Mkataba ulikata,ulitaka afanye nini?Abaki London kufagia mitaa?Maana shule hana.BBC swahili walireview mikataba na waliobaki wamehamishiwa Nairobi.BBC swahili inarusha matangazo yake kutokea Nairobi.
 
Unaona sasa ulivyo muongo eti wazungu wa UK hawajali elimu sana! Jidanganye labda kwa kazi ya kubeba boksi. Haujui lolote nakuhakikishia SK kimemtoa BBC elimu na kashindwa na Mkenya ndio yeye na wenzake wakatoa wengine wakakimbilia Idhaa ya Kiswahili ya Uturuki. BBC bila elimu na kumbuka dunia inapika kwenye bahari ya mabadiliko makubwa sio hizi Local media sina akina Swebe,Baba Levo,Kitenge, Kumwembe na akina Jose Mara zilivyojaza upuuzi na ujinga mtupu. Tena ukome kusema UK hawajali elimu vile vyuo vyao unajua wanavyozilinda kupokea watu wajinga kama wewe.
Wakati BBC ina muajiri kikeke, Je walikuwa hawajui hana shule?

Kwa hiyo unasema kikeke katolewa BBC kwa vile Hana shule, Je BBC ili ajiri mtu asiye na shule?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Unataka kuniambia Gerson Msigwa ni mtu makini sana?
Huyo nae aliwekwa tu hapo kwa vile Mama hakuwa na jinsi baada ya kumuondoa ukurugenzi wa mawasiliano ikulu,si unaona Samia kamuondoa. Zamani kabisa enzi ya JK ninakumbuka alikuwepo hapo mtoto wa Kawawa ambae shule ipo.Yule binti alisoma UDSM.
 
Ndugu, labda na au hunijui na hilo box pia. umekaririshwa kwamba ukienda huko ni kubeba box, kama walibeba ni wao , sio wote.
Jua tu kwamba hayo niliyo yasema ni kweli tupu. Huko UK nimeishi si chini ya miaka 23, nina watoto ambao kwa sasa ni lecturers wa Oxford na Cambridge na nimefanya kazi ya Sheria kama Top QC na au KC kwa zaidi ya miaka 15 ktk tassisi zinazo heshimika duniani mpaka Tanzania pia achilia mbali serikali ya Uingereza yenyewe. Hivyo ukiwa unataka ligi, jiandae. Sasa sema uongo wangu uko wapi ili hali kwa mfano mdogo tu ukitoka huko bongo na masters hawaithamini sana huko UK, na lazima uwe kitchen porter kwanza. Kama unataka ligi, weka contacts zako nikufungulie kesi tuone utachomoka vipi. Ni tumie kwenye private message kama unaogopa kuzimwaga hapa ili tuone muongi ni nani. Mwana kulitafuta , mwana kulipata, twende kwa pilato, si unataka...
Kujali ubora wa Elimu na kujali uzoefu wa kazi ni vitu viwili tofauti.
Mkuu achana na watanzania hawa wame laanika

Wana chuki na ma wivu tu...

Wanamponda kikeke eti hana shule, isitoshe wao hapo walipo ni maskini choka mbaya...!!!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hahaha msemaji anapika ugali kwenye kigeto London.Jamani si kila alieko Ulaya mambo safi. Kwanza mji wa London ni ghali sana tena sana.

Mkataba ulikata,ulitaka afanye nini?Abaki London kufagia mitaa?Maana shule hana.BBC swahili walireview mikataba na waliobaki wamehamishiwa Nairobi.BBC swahili inarusha matangazo yake kutokea Nairobi.
Shule hana kivipi?

Hebu elezea elimu yake mpaka kufika BBC, unayosema shule hana.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ndugu, labda na au hunijui na hilo box pia. umekaririshwa kwamba ukienda huko ni kubeba box, kama walibeba ni wao , sio wote.
Jua tu kwamba hayo niliyo yasema ni kweli tupu. Huko UK nimeishi si chini ya miaka 23, nina watoto ambao kwa sasa ni lecturers wa Oxford na Cambridge na nimefanya kazi ya Sheria kama Top QC na au KC kwa zaidi ya miaka 15 ktk tassisi zinazo heshimika duniani mpaka Tanzania pia achilia mbali serikali ya Uingereza yenyewe. Hivyo ukiwa unataka ligi, jiandae. Sasa sema uongo wangu uko wapi ili hali kwa mfano mdogo tu ukitoka huko bongo na masters hawaithamini sana huko UK, na lazima uwe kitchen porter kwanza. Kama unataka ligi, weka contacts zako nikufungulie kesi tuone utachomoka vipi. Ni tumie kwenye private message kama unaogopa kuzimwaga hapa ili tuone muongi ni nani. Mwana kulitafuta , mwana kulipata, twende kwa pilato, si unataka...
Kujali ubora wa Elimu na kujali uzoefu wa kazi ni vitu viwili tofauti.
Nimesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ila sijafikia level ya kutojua mambo kama akili yako. Sasa unaongea nini? Unasema UK hawathamini elimu halafu unakuja na hoja tena watoto wako wasomi mpaka wamekuwa wakufunzi hauoni kama hauna mwelekeo. Nahisi wewe uzee unakusumbua. Tulia ulee wajukuu.
 
Du! Mkuu sasa si ujibu hoja tu mbona unajihami bila hoja?
 
Hakuna salamu hapa, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kama ilivyokuwa kwa Tido Mhando aliyetolewa BBC na kuletwa kusimamia TBC, ndivyo ilivyokuwa kwa Salim Kikeke. Taarifa za kiintelejensia zinapenya kuwa ndugu Kikeke aliombwa kung’atuka BBC ili arudi nchini kuandaliwa kuwa msemaji wa serikali. Baada ya kufika nchini alisubiri kwa muda mama aachie nafasi ya uteuzi bila mafanikio. Ndipo akaamua kwenda kujishikiza pale EFM ili mama akipangua nafasi za uteuzi yeye ateuliwe kuwa msemaji wa serikali. Inavyoonekana ni kama vetting bado ilikuwa haijakamilika.

Baadaye upekuzi ulipofanyika kwa kina zaidi, ikaonekana nafasi ya usemaji wa serikali haitamfaa. Nafasi ile inamfaa mtu muongeaji na mwenye uwezo wa kuelekezwa kusema uongo akatoka hadharani kuusema na kuutetea kwa macho makavu. Kikeke ni mtu wa msimamo na asiyefundishwa nini cha kuongea. Ni mtu mwenye kusimamia maadili ya habari na anamuogopa Mungu. Ni vigumu sana kumwambia aende hadharani kusema uongo kwa lengo tu la kutetea jambo au madudu ya serikali.

Hiki ndiko kilichomponza kijana wa watu licha ya kushawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi na serikali lakini kazi aliyoahidiwa amekuja kupewa mtu mwingine. Wafanyakazi wa BBC huwa wanafundishwa maadili ktk taaluma ya habari yanawafanya waive sawasawa na kutokubali kuyumbishwa.

Tukumbuke pia Tido Mhando misimamo yake ni sawa na ya Kikeke. Tido aliombwa kurudi nchini akapewa TBC. Baada ya kunyesha msimamo usioyumba katika kusimamia ukweli kwenye habari, serikali ikamtupa nje na kisha kumfungulia kesi ya bandia ya uhujumu uchumi. Mpaka sasa nadhani hiyo kesi anateseka nayo mahakamani.

Kumbuka mtu kaacha kazi BBC anakolipwa mamilioni ya paundi za kingereza anashawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi nzuri halafu hapewi! Hii sio sawa. Kama kazi hakuna au huna uhakika wa kumpa kazi, ni bora wangemuacha abaki BBC aendelee kuvuna paundi zake angerudi nyumbani afungue media awaajiri vijana wenzake.

Tazama mfano wa Abdalla Bulembo Majura aliyevuna paundi za kutosha akiwa BBC aliporudi nyumbani amefungua kituo cha redio ABM FM kule Dodoma amewaajiri vijana wa kitanzania wanapata ridhiki zao za kila siku bila tatizo. Kama Kikeke angeachwa aendelee kukaa BBC hadi astaafu angerudi nchini akiwa na paundi za kutosha akafungua kituo cha TV au redio akawaajiri vijana wenzake. Sio haki kumuahidi mtu kuacha kazi ya pesa nyingi halafu anarudi nyumbani kwa matumaini ya kupewa kazi, anatoswa mazima. Tabia hii sio nzuri na haitoi mfano mzuri kwa vijana wachapa kazi kama Kikeke.

USHAURI WANGU
Naishauri serikali impangie kazi nyingine ndugu Salim Kikeke kwa kuwa wameamua kugawa nafasi yake kwa mtu mwingine kinyume na makubaliano. Huu mchezo wa kutosana ukiendelea, itakuwa vigumu kuwashawishi vijana wezalendo kutoka ughaibuni kurudi nyumbani kuitumikia nchi yao. Nchi hii ni yetu sote, sio mali ya kikundi fulani cha watu.

Nawasilisha.
Kikeke kaponzwa na vyeti tu,diploma haitoshi kuwa msemaji mkuu wa serikali
 
Back
Top Bottom