Chawa wa mama yazinduliwa Rasmi

Chawa wa mama yazinduliwa Rasmi

Haya mambo hayataki hasira kabisaa...
Chama kubwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM wameshasema nani apinge😋😋😋

Ndugu zangu chuki na makasiriko tuweke pembeni tufanye siasa za afya




Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hasan

Kazi iendelee
 
Viongozi wa juu wa chama wasipoliangalia hili mapema litakitafuna chama ingawa haliwezi kukimaliza (zimwi likujualo halikuli likakwisha)

Kwa kuzingatia maana halisi pamoja na tabia za mdudu Chawa neno hili au haka kakikundi hakafai kabisa kutumika ndani ya siasa za chama Cha Mapinduzi au chama kingine chochote!

Chawa au kupe ni mdudu hatari sana na ana sifa ya unyonyaji pasina kufanya Kazi na humdhoofisha host wake na hata kumsababishia kifo ikibidi kufanya hivyo kwani Hana huruma ilimradi TU Tumbo lake lijae na hajali ananyonya wapi hata kwenye jicho!

Kwa maana hiyo basi MAMA NI RAIS WA NCHI (MAMA NI STATE IDENTITY) amepewa dhamana kikatiba kusimamia rasilimali za nchi hii kwa manufaa ya watanzania wote kwa maana hiyo tukimtazama tunaiona Tanzania!

Linapojitokeza kundi na kujiita Chawa wa mama tafsiri yake sahihi ni kundi ambalo limejitanabaisha kuwa wao ni wanyonyaji wa nchi na kwakua nchi sio Safi umeamua kukaa na Chawa Ili waendelee kuinyonya! Matokeo yake Chawa hawa wanasifia kila uchafu na uzuri wa nchi (Rais) Ili waendelee kuneemeka!
Kwa mfano kule katika ngazi za uongozi wa chama Kuna kitu inaitwa kamati ya utekelezaji ya chama ambayo inajukumu la kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama kwa kuangalia miradi ya chama inavyotekelezwa lakini kule ndio Kuna Chawa kwani fedha za umma kila siku zinapotea na husikii hata sauti Yao! (10%)

Mmemsikia huyo mama ambaye sijui ndio mwenyekiti wa jukwaa la wanawake mkoa wa pwani! Niulize jukwaa la Nini wakati Kuna UWT? anasisitiza tukajibu HOJA hoja zipi aweza kujibu wakati Kuna baraza la mawaziri ambalo limepewa dhamana ya kutekelezwa shughuli za serikali na kuzitolea majibu ama bungeni au kwa wananchi Moja kwa Moja?

Haka kakikundi machawa katatumiwa vizuri na vyama pinzani kuelezea athari za Chawa kwa jamii na kwa misingi hiyo itabainika wazi wazi kwamba maisha magumu ya nchi hii yanasababishwa na Chawa ambao wamepata baraka kutoka kwa chama Cha mapinduzi ambacho kina dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi hii Ili kutengeneza ustawi wa jamii kijamii na kiuchumi.

Bado tutaamini kwamba licha ya rais kukopa sana kwa Nia njema machawa wanafurahia kwa sababu mishipa ya damu inazidi kujaa na wao kunyonya bila kujali kwamba nchi inadhoofika kwa madeni na Huku wananchi wakikabiliwa na matatizo lukuki ikiwemo mfumuko wa Bei na huduma duni za jamii ambazo kuzipata kwahitaji gharama kubwa!

Yes wananfurahi hayo na watayatetea sana bila kuwa na hoja na kutuambia hamuoni madaraja na mameli na mabarabara? Swali je ni thamani halisi (value for money? ) Wakati CAG report yake kila mwaka Inalalamika Chawa wanyonyaji?
Matumizi ya Neno Chawa sio sahihi hata kidogo na yakitumiwa vizuri na wapenda haki yanakiumiza chama!
 
Chama kubwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM wameshasema nani apinge😋😋😋

Ndugu zangu chuki na makasiriko tuweke pembeni tufanye siasa za afya




Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hasan

Kazi iendelee

Mwanzoni, nilidhani CHAWA ni miradi inayotekelezwa, kuzuia mfumuko wa bei, kuleta maendela kwa wananchi, ETC..!! Maana hayo humtangaza aliyeyafanya..!! Ukiona tu unahitaji chawa ili watu waone ulichokifanya, BASI HAPO HAMNA KITU.
 
Chama kubwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM wameshasema nani apinge😋😋😋

Ndugu zangu chuki na makasiriko tuweke pembeni tufanye siasa za afya




Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hasan

Kazi iendelee

Hivi hawa chawa wa mama wanakaa sehemu gani ya mwili wake? Tunajua chawa hupenda kukaa kwenye sehemu zenye nywele tu.
 
Chama kubwa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM wameshasema nani apinge😋😋😋

Ndugu zangu chuki na makasiriko tuweke pembeni tufanye siasa za afya




Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hasan

Kazi iendelee

Nonsense
 
Si ni bora wangetafuta hata jina lingine kuliko hili la chawa?
 
Back
Top Bottom