Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Unajua hawa wamiliki wanataka waue ndege kwa jiwe moja. Wanataka kuwa kama Brighton kwa kununua chjipukizi na kuwauza bei ya juu lakini hapo hapo watengeneze timu ya kubeba makombe baada ya miaka 3-5. Sasa si9si mashabiki kwa vile sio wawekezaji hatuna habari na hilo lengo la kufanya biashjara ya faida. Sisi tunachojali ni kubeba makombe asubuhi kama ilivyo desturi ya Chelsea kitu ambacho hakityawezekana. Tuwe wavumilivu hadi 2026/27 ndipo tuanze kuwaza makombe hata yale ya mbuzi
 
Mr. Lembu hili tuliongea kuanzia mwanzo huu mpango wa kununua makinda wengi ilihali tuna academy inazalisha makinda kila siku maana yake ni nini?

Majibu ndio haya unayosema ni kuwekeza kibiashara nunua makinda wengi + zalisha makinda wengi = Faida sokoni.

Wamiliki watahakikisha wanarudisha kwanza ile £1B waliotumia kusajili mazagazaga. Ndio zije habari za makombe.
 
Hii ina maana kwamba sisi mashabiki tumekuwa hatumtendei haki Enzo Maresca.

Kocha huyo alikuwa na kikao na bodi siku moja kabla ya jana ambapo walijadili kuhusu usajili wa wachezaji na matokeo mabaya ya hivi karibuni.

Alitaja hitaji la mshambuliaji mahiri tena, angalau kwa mara ya tatu sasa, na anaamini hatuna wasifu katika nafasi ya 6.

Kwa kifupi, ameitaka bodi kwa mara ya tatu kusajili mshambuliaji mwenye uwezo wa kumalizia nafasi zinazotengenezwa.

Pia ameomba kusajiliwa kwa kiungo mkabaji katika namba 6.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo huwasifu na kuwalinda wachezaji kwenye vyombo vya habari tu, lakini mambo ni tofauti sana nyuma ya pazia.

Kwa upande wao, wakurugenzi wa michezo wanaamini kuwa hakuna mshambuliaji mzuri sokoni wakati wa dirisha hili la Januari hadi dirisha la kiangazi.

 
Kama Maresca amewasilisha mahitaji ya wachezaji kwa hizo nafasi hapo sawa tupo nyuma yake. SD"s ndio maadui wetu kwa sasa
 
Bournemouth hawajapoteza tangu Dean Huijsen (19) na Illya Zabarnyi (22) walianza kucheza pamoja michezo 10 iliyopita.

Mhimili wa walinzi wachanga zaidi katika Ligi ya Uingereza wanaosimama kidete kulinda lango la timu yao isifungwe kiholela.

 
Liam Rosenior juu ya Santos:

"Andrey atakuwa na taaluma nzuri ya mpira. Andrey anacheza kama ana umri wa miaka 32. Ninamwita Dunga. Yeye ni Mbrazil lakini hachezi kama mbrazili.

Yeye ni mjanja na makini sana na takwimu zake ziko juu sana, kwa suala la kufunga mabao, kushinda mipira ya juu. Atakuwa na taaluma bora."
~
@TheAthleticFC

 
Sporting directors ndio wanampanga Sanchez kila siku golin?
Mashabiki wengine wanaamini kuwa Kocha wa Makipa, Ben Roberts ndiye mwenye shinikizo la Sanchez kuwa golkipa namba 1.

Ben Roberts alikuwa ni kocha wa makipa huko Brighton
Kaja kuwa kocha wa makipa katika Chelsea (chini ya Potter na Pochettino)
Sasa amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Kipa wa Kimataifa.👀

Yeye ndiye mwenye msukumo nyuma ya uhamisho wa Sanchez Chelsea wakati huo huo sababu kwa nini Sanchez anaendelea kuwa kipa wa kwanza hata baada ya performance yake kuwa mbaya wiki hadi wiki.
 
The Blues kwa sasa haina tofauti na Brighton, Bournemouth. Imekuwa timu ya daraja la kati kiushindani. Imekuwa timu ya kusaka vipaji kununua na kuuza kwa faida.
 
Nani aliyemsajil ???? Kipq anasajiliwa ashapoteza namba kwa team km brighton kwa sabab ya makosa yake
Nikurekebishe mkuu.
Kapewa demotion na Roberto De Zerbi kwa sababu ya makosa yale yale yan ayojirudia. Katika umri wake wa miak 27 tusitegemee atabadilika
 
The Blues kwa sasa haina tofauti na Brighton, Bournemouth. Imekuwa timu ya daraja la kati kiushindani. Imekuwa timu ya kusaka vipaji kununua na kuuza kwa faida.
Ondoa Borenamouth wao wako vizuri
Chelsea imeiga model ya Brighton na wamiliki wa Chelsea walishakiri kuipenda model ya Brighton
A mid tgablke team yenye kulipa wachezaji mshahara mdogo lakini inapata faida kubwa.
Ndio maana imekazana kuwanunua wachezaji wadogo hata ambao hawatapata nafasi ya kucheza ili iwauze.
Ila hawajui kuwa mchezaji asipopata nafasi ya kucheza hakun a timu itakayomtaka.
Mchezaji akicheza sana na kuonyesha uwezo wake ndipo timu zitamfuatilia.
Caicedo tuliweza kumfuatilia Brighton kwa sababu alikuwa akicheza kila mechi.
 
Enzo Maresca:
"Tuna makipa wawili wazuri, kwa hivyo tunaweza kufanya maamuzi tofauti. Haimaanishi kwamba Robert anaweza kufanya makosa kila mchezo na kubaki golini."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…