CHINA AMEKWISHA SHINDA VITA YA UCHUMI DHIDI YA MAREKANI : MAREKANI ALIKOSEA KUCHANGA KARATA

CHINA AMEKWISHA SHINDA VITA YA UCHUMI DHIDI YA MAREKANI : MAREKANI ALIKOSEA KUCHANGA KARATA

05CUBA

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2025
Posts
1,106
Reaction score
1,650
CHINA imechukulia vikwazo vya MAREKANI Kama fursa tukio linalotueleza kuwa MAREKANI ALIKOSEA kuchanga karata zake na ushuru wake wa asilimia Zaid ya 230 kwenye bidhaa za uchina.

Kitu Dunia haikujua ni kwamba Kuna bidhaa nyingi Sana za kimarekani Hasa zile za mavazi na kielectronic huwa hazizalishwi MAREKANI Bali huzalishwa CHINA na kufanyiwa finishing (brandunga in specific) ndani ya MAREKANI.

Bidhaa Kama nguo za brand kubwa, simu za brand kubwa na VIFAA vingi vya kielectronic huzalishwa CHINA na ma supliyer wa kichini Kisha MAREKANI huvijumua ... akisha kuandika nembo yake hupandisha Bei kwa zaidi ya mara 100 ya Bei halisi na Kisha kuziuza Kama bidhaa ya kimarekani akipata faida kubwa kupita kiasi.

Mtu atauliza kwanini MAREKANI hufanya hivyo ?
Well kimsingi MAREKANI hawez kuzalisha bidhaa kwa ukubwa kama china kwa sabab mbali mbali ikiwepo mazingira magum ya kiuzalishaji ndan ya Taifa lake, mfano malipo ya wafanyakazi na gharama za usimamizi na uendeshaji wa viwanda ni ngum Sana ndan ya MAREKANI .

Pia upatikanaji wa Malighafi kwa bidhaa nyingi ni mwepesi Sana china as kwa nchi ya china Kuna cheap labour na Kuna Kila aina ya kiwanda , hivyo ni rahisi kupata the needed materials there.

Mchina kufanya Nini ?
Mchina hajamwaga ugali baada ya MAREKANI kumwaga mboga, mchina amebeba ugali kaenda kutafuta mboga na anataka kula ugali peke yake bila kumgawia MAREKANI.

Nimeona namma Ali express, Alibaba, na mitandao mwingine ambayo situmie nimeona Wana tangaza kwa nguvu Sana huko kwenye social media juu ya bidhaa zao kwa Sasa.

Kinachochekesha ni pale influencers na brand ambassadors wa CHINA wanapo onekana kuanza ku expose bidhaa ambazo huwa Zina bandikwa nembo za made in AMERICA na kuaminiwa kuwa ni Bora kuliko za UCHINA.

watu wanaanza kuelezwa ukweli kwamba bidhaa husika ni zakichina Ila MAREKANI ndiye huzijumua na kumaliza kuandika nembo Kisha kiziuza kwa Bei ya juu Sana kwa watumiaji ambapo Bei huzidi zaidi ya Mara 100 ya Bei HALISI. (Ila bidhaa nyingi huzidi hata 100 % ya Bei HALISI)

Baada ya ku expose ujinga huo wa producers wa mchongo wa kimarekani , real producers now wwanakuwekea offer mezani...

Producers from China wanasema : ukitaka bidhaa husika mfano bidhaa za nguo na urembo za LV , Nike ,Levi's , Ralph Lauren ,Tommy ,Hilfiger ,Calvin Klein ,Under,Armour ,Guess ,Supreme ,Abercrombie & Fitch , American, Eagle Outfitters
, Hollister Co. , The North Face , Gap , Balenciaga na Adidas

UKITAKA BIDHAA ZA HAWA JAMAA AINA ZOTE KAMA ZILIVYO SOKONI watakusafirishia bure Hadi MAREKANI, na watalipia import fee na tax zote wenyewe Kisha wewe utapata bidhaa OG zenye mark ya made in America as usual ... Kasoro nembo ambazo zile huwekwa na kampuni husika

This means MAREKANI inaenda kupoteza Pato kubwa Sana la kizandiki na kiwizi lililokuwa likiipata from UCHINA.

na China hapotezi kitu Bali ana gain umaarifu kwa WEREDI wake.
😁🙏😁.
round kick
Eli Cohen meza imepinduka mchina hajajipiga Pini Ila MAREKANI ndo kajipiga Pini mze.

JAMUHURI YA WATU WA UCHINA ????
KAZI IENDELEEEE. 🙏🙏🙏.

Ila kwa sisi Tanzania hapa tufanye NNE kwanza .. Ila ikifeli CHADEMA wamejiua....
Tukimaliza siasa uchwara zetu tutageukia haya mengine
 
Mkuu kila siku nasikia soko kubwa la bidhaa za mchina ni marekani, na nikiangalia nchi za afrika karibia 90% ya bidhaa tunazotumia ni made in china. Kuna Haja gani ya mchina kung'ang'ania solo la marekani?

Kiongozi MAREKANI inaukubwa karibia sawa na Africa kiujumla. (NNB KARIBIA SAWA)
.
Population yake na pia vivyo hivyo .. na kingine sisi tu anunua bidhaa cheap Sana. MAREKANI ananunua bidhaa zenye thamani kubwa a lot more than us.
 
Mkuu kila siku nasikia soko kubwa la bidhaa za mchina ni marekani, na nikiangalia nchi za afrika karibia 90% ya bidhaa tunazotumia ni made in china. Kuna Haja gani ya mchina kung'ang'ania solo la marekani?
Yaani wewe unayeng'ang'ania kuuziwa smatifoni ya kichina kwa elfu ishirini uwe soko sawa na la Marekani? Acha utani bwana!
 
Naona hili ulilozingumza ni kidogo
Hawa macho kuvimba wamezuia export ya rare earth metals ...hizi ndo dili kubwa kwa tech yoyote
Hebu waza silaha za kisasa,electronic devices kama simu,tv,taa,computer,magari ya umeme na vingine vingi havutaweza kutengenezwa baada ya stock ya rare earthmetal kuisha
Hii Dunia itaenda kuwa ngumu sana
 
Juzi Trump alivifutia Kodi VIFAA VYA kielectroniki vyote.... Lakini mvimba macho akabaki kuwabania raw materials za VIFAA muhim Kama usemavyo ....

Kasheshe kubwa imebaki kwenye viwanda vya MAREKANI kupata soko na raw materials as anategemea kule. .. na kubwa kuliko middle man wake wote wanaotegemea kulangua bidhaa za china wanaenda kuporomoka this year ....

Mabilionear wengi wa kimarekani wanaenda kudhoofika Hasa wale wanaotegemea sekta ya fashion na electronic devices.

Mwenzie soko atalipata palepale marekani hata akipandisha kodi Mara dufu Tena.
 
Hakuna kitu kama kama hicho

Ni Artificial na haliwaki ama kuwekwa juu kama la Asili

Lipo kwenye chumba maalum na ni kwa ajili ya kuzalisha Umeme

Sahihi mkuu ...
Matumizi yake siyo kumulika nadhani.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa .. hii ni SAYANSI ya nuclear fusion (muungano wa nyuklia)

Jua husika kitakuwa Lina zarisha nishati Safi na ya Bei rahisi Sana ... Inazalisha nyuzi joto milioni 120 katika Kila kipindi Cha SEKUNDE 101.
 
Habari yako hujaifanyia utafiti wa kutosha kiongozi.

Ni kweli kiongozi ....
Ila kuliko nyuzi zangu za kipuuzi hii ni Bora zaidi. Inaongeza mawazo flan na uwezo wa kufikiri .

Ukisoma huu Uzi ahsubuh unajifunza kuwa mtu mwenye kuchukua maamuzi kwa kufikiri . Na sio kipuuzi Kama Trump.

Ila next time nta improve mkuu. The Assassin
 
Juzi Trump alivifutia Kodi VIFAA VYA kielectroniki vyote.... Lakini mvimba macho akabaki kuwabania raw materials za VIFAA muhim Kama usemavyo ....

Kasheshe kubwa imebaki kwenye viwanda vya MAREKANI kupata soko na raw materials as anategemea kule. .. na kubwa kuliko middle man wake wote wanaotegemea kulangua bidhaa za china wanaenda kuporomoka this year ....

Mabilionear wengi wa kimarekani wanaenda kudhoofika Hasa wale wanaotegemea sekta ya fashion na electronic devices.

Mwenzie soko atalipata palepale marekani hata akipandisha kodi Mara dufu Tena.
Huyu angeendelea na Dunia kama inavyotaka......hii vita haifai
Wa us wanasema tutanunua India,Vietnam etc ila huko India hadi dawa wanafanya assembly tu
 
Huyu angeendelea na Dunia kama inavyotaka......hii vita haifai
Wa us wanasema tutanunua India,Vietnam etc ila huko India hadi dawa wanafanya assembly tu

Vita ya uchumi hajawahi kuwa na mshindi wa moja kwa moja.

Wamemshindwa mrusi. Watamuweza mchina Sasa ???
 
Back
Top Bottom