CHINA AMEKWISHA SHINDA VITA YA UCHUMI DHIDI YA MAREKANI : MAREKANI ALIKOSEA KUCHANGA KARATA

Kwani kuna uhaba wa mwanga na joto la jua hadi tuhitaji jua la kutengeneza?

Jotoridi lililopo kwasasa duniani linahitaji kupunguzwa kwa mataifa makubwa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu viwandani.

Kama ni jua kwa ajili ya uzalishaji wa umeme mbona jua lipo kali sana kote ulimwenguni hadi mataifa ya ulimwengu yamekuwa yakikutana mara kwa mara ili kuona namna ya kudhibiti joto kali linalotokana na kuwaka kwa jua kusiko kawaida.
 
Mchina kateka soko maana bidhaa yoyote unayohitaji anakutengenezea kwa ela uliyonayo, anakidhi principal ya demand and supply, iyo America yenyewe siyo wote wanaweza kununua bidhaa yao, china anacover ilo gap, unaweza kweli kushindana naye?
 
Hilo Joto kali unalolisema ni kwa Afrika sio China
 
Ni kweli US hapa kwenye tariff kakosea ila tukumbuke kwamba USA bado ina faida za kimkakati katika fedha, teknolojia, na ushirikiano wa kimataifa, na inachukua hatua za kupunguza utegemezi wa China.

Makampuni ya USA yanahamia nchi washirika kwa USA kama India, Vietnam n.k
 

Huyaelewi mambo haya kiundani.

Nikupe shule kidogo:

1. China ndiyo inayoongoza Duniani kwa kuwa na makampuni mengi ya kigeni, hasa toka Ulaya na America.

2. Makampuni mengi ya kigeni yaliyopo China yanatengenezea bidhaa nchini China kisha huzisafirisha kwenda kuuza kwenye mataifa yao (kama ulivyosema, labour nchini China ni cheap), na pia nyingine huziuza bidhaa hizo ndani ya China (China ina soko kubwa, na wachina wengi wenye uwezo kifedha huwa hawataki kununua bidhaa zinazotengenezwa na wachina wenzao kwa sababu ya ubora kuwa chini).
3. China wakati wote imekuwa inahangaika kushawishi makampuni ya Ulaya na America kuwekeza nchini China ili kuweza ku-penetrate masoko ya America na Ulaya, jambo ambalo ni gumu kwa kampuni zinazomilikiwa na wachina wenyewe kufanikiwa, kwa sababu ya ubora duni wa bidhaa zao.

4. Makampuni yanayomilikiwa na wachina wenyewe, soko lake kubwa ni mataifa yasiyozingatia ubora, hasa Africa na baadhi ya nchi za Asia.

5. Siku za karibuni, Serikali ya China imekuwa ikijitahidi kuyanunua kwa gharama kubwa sana makampuni ya wazungu yaliyopo China kwani yale tayari yana majina na yanazingatia viwango, lengo ni kutaka siku moja makamouni hayo ya kigeni yawe yanamilikiwa na China yenyewe.
6. Anachokifanya Trump ni kulazimisha makampuni ya Ulaya na America yaliyopo China ambayo tegemeo kubwa la soko ni USA, yaondoke China. Hilo angefanikiwa zaidi kama angeshirikiana na Ulaya. Yakiondoka masoko ya Ulaya na America, China itatetereka sana kwa sababu soko la Africa na Asia ni dogo sana katika thamani ya mauzo.

Kwa vyovyote vile, haya masuala ya tarrifs yataiathiri China na US.
 
Hilo Joto kali unalolisema ni kwa Afrika sio China
Mkuu unaishi sayari ya Mars?

Miongoni mwa mataifa yanayoonhoza kuzalisha joto kali ni China.

Kitu kinachoitwa 'Global warming ' hujawahi kukisikia?

Sasahivi hata mataifa yaliyokuwa yanapitia vipindi vya baridi kali misimu yote ya mwaka, kwasasa yanapitia vipindi vya jua kali kupitiliza hadi nyuzijoto 40+.

Hujaona ama kusikia siku za nyuma hapo baadhi ya mataifa ya Ulaya wananchi walikuwa wanashinda baharini kupooza miili baada ya joto kuzidi kiwango cha kawaida?

China haipo nje ya sayari ya dunia hivyo na wao wanapitia hali ya joto kali inayoikumba dunia mkuu.
 
Kiongozi MAREKANI inaukubwa karibia sawa na Africa kiujumla. (NNB KARIBIA SAWA)
.
Population yake na pia vivyo hivyo .. na kingine sisi tu anunua bidhaa cheap Sana. MAREKANI ananunua bidhaa zenye thamani kubwa a lot more than us.
population ya marekani haiwezi kuwa sawa na africa sababu usa poluation iko around 340 millions wakati africa kwa ujumla wake tuko around 1.39 billion
 
Trump ni mtu mwenye papara na asiyefikiri vya kutosha kama lissu, na bado anafikiri kujiongezea muda ili kuiua kabisa marekani.(huko baadae sana huenda marekani ikapigana vita na uchina kulinda utukufu wake)
 


Shule kubwa.
 
Trump ni mtu mwenye papara na asiyefikiri vya kutosha kama lissu, na bado anafikiri kujiongezea muda ili kuiua kabisa marekani.(huko baadae sana huenda marekani ikapigana vita na uchina kulinda utukufu wake)

Wote walipigwa risasi waka survive.
 
Trump ni mtu mwenye papara na asiyefikiri vya kutosha kama lissu, na bado anafikiri kujiongezea muda ili kuiua kabisa marekani.(huko baadae sana huenda marekani ikapigana vita na uchina kulinda utukufu wake)
Hapo sijui Tundu Lissu ameingiaje! Lakini kuhusu Trump itoshe tu kusema ni kibaraka atumikaye kuisambaratisha Marekani... Soon zile 50 zitasambaratika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…