China ataiua US kwa presha, katangaza Kirin 9006C(chip) ya 5nm tech

Hapa mnajadili wenyewe kwa wenyewe!!
WABONGO BHANA 🤣🤣🤣😂😂 WANAJADILI WENYEWE KWA WENYEWE NA WAKITAKA KUTAFUTA MAISHA WATAKIMBILIA UBALOZI WA USA KUOMBA VISA...
NB:TOKA MWAKA 1970 TUNAONA HARAKATI HIZI ZISIZOFANIKIWA KUIONDOA USA KWENYE USIKANI NA MTAKUFA MTAIACHA USA ON TOP.
Hakuna wa kuipa USA govt presha!!!!Wanajua kucheza fair play na rough pia
 
Swali zuri
 
Instagram beta

Nilichokuwa napenda Windows phone hamna app za kitoto Kama ile ya Android et una download solar inaonesha Kama inachaji simu😁😁

Na games zake zilikuwa nzuri Sana hata ukiwa na Lumia 620 ram 512 Ina perfom vizuri


Unaeza cheza game leo uka minimize ukakaa hata week unakuja fungua linaendelea pale pale ,,, au zile app za ku track distance speed nk hata ukifungua app zingine ile hujaigusa utakuta inaendelea Soma speed na distance travelled as well


Nakuja kwa Android ukitumia wasap dk kadhaa unakuta ile app ishajifunga
 
Windows ilikuwa poa sana. Miaka ile nilikuwa nafanya kwenye ofisi moja ya nokia simu hizo tulikuwa tunaoewa bure kila toleo linapotoka.
Looking back android kwa windows ilikuwa takataka kipindi hicho. Kweli apps zilikuwa zina crash na windows phone ilikuwa ahead of its time UI flat ambayo ndiyo ya sasa
 
Niliumia Sana baada ya kusikia update hazitotoka Tena ki ukweli nilikuwa nazipenda Sana,, napenda kuwa unique hivo njia ya kuwa unique nikutumia Zile simu zilikuwa na Raha yake


Lumia 620 spika yake Kuna ile 1520 camera yake Ni balaa ,, kwa miaka ile walikuwa ahead of time
 
Hakuna aliyesema anaikimbiz kwa tech tunachosema hapa ni kwamba vikwazo vya marekani havifanyi kasi anazidi kuipa presha kuwa anaweza kuendelea kuunda vitu bila kuitegemea
Mchina hayupo kushindana na USA wala hamuwezi ila yupo kwa ajili ya kupata hela tu.
Mchina yupo radhi atumie OS ya android ili apate hela na kuendelea kupata hela ila hayupo radhi kutengeneza OS yake ambapo kuingia sokoni, kupata developer na kutumiwa mpk kuezoeleka itamchukua miaka mingi kupata hela au kukosa kabisa.
Ukifuatilia bidhaa au vitu vingi anavyotengeneza mchina Original yake ni Marekani anaweza kuborosha kidogo au kutoiborosha kabisa.
Huawei ilipigwa stop kutumia Google play store iliyumba sana kiuchumi leo hii Marekani ikasema hakuna kutumia Android OS kwenye simu za kichina, soko la bidhaa la simu za kichina zinaweza kufa kabisa.
 
Hakuna sababu ya kuunda OS mpya na ndio maana si china tu hata nchi nyi gine hawaundi OS nyingine na wakitaka OS kwa ajili ya shughuli fulani wanatumia linux based OS.
Haya masuala ya kuunda OS kila mtu ya kwake yalikuwa ya miaka ya 80 huko kipindi kila kampuni inaunda OS yake.
China is progressing kwa speed ya 5G na hizi breakthrough ni hatari kwa maslahi ya US.
Wakati anamlima ban ya kuaccess hizo technology, yeye mwenyewe US alisema kuwa china kuwa na hizo technology ni tishio la usalama kwake US.
Sasa china kadevelop kuunda hivyo vifaa bila msaada wake US, so tishio lipo pale pale.
 
Mchina anachojua ni kutengeneza hela kupitia OS za wengine na kutumia majina ya wengine.
Leo hii ukitafuta iPhone utaikuta na iPhone ya kichina yenye Android.
Nilitegemea mchina naye atakuwa na OS yake lkn anachofanya ni clone os za wengine.
Angalia hii battle
1. Symbian
2. Windows phone
3. Blackberry OS
4. Android
5. IOS
Zote hizi ni za wamerekani na ni OS za kipekee na muonekano na app zinazojitegemea.
Leo hii mchina anasema ametengeza OS inayoitwa Harmony inayotumia applications za Android.😁😁😁😁
 
Umekalili OS OS OS.
Mbona linux imetengenezwa na Mfinnish na inatumika dunia nzima iliwemk Marekani? Kampuni kibao Marekank zinatumia linux hasa kwenye server side. Android yenyewe ni linux based system.
Biashara ya OS sio kama biashara ya hardware
 
Kama siyo muhimu
Kati ya Android na IOS ipi ilianza?
Wenye akili za kutengeneza OS ni wamerakani. Hapo mchina pamoja na kukopy na kupaste kwake amenyoosha mikono haiweI kutoboi.
Hiyo ya haina haja ni kisingizio tu
 
Kama siyo muhimu
Kati ya Android na IOS ipi ilianza?
Wenye akili za kutengeneza OS ni wamerakani. Hapo mchina pamoja na kukopy na kupaste kwake amenyoosha mikono haiweI kutoboi.
Hiyo ya haina haja ni kisingizio tu
Nimekuuliza, linux aliyeitengeneza si Mmarekani unakalili vitu tu.
Hata android ni linux based OS...
Iliyoanza kwenda public ni iOS wakati Google akijiandaa kuzindua simu yake yenye android ikabidi oroject aifute naye aunde OS itakayosupport full touch.
Kuunda OS watu wanaweza kuunda lakini kwa manufaa gani?
 
Tukiachana na anga, unaongeleaje byd wang u8 inayotembea km 1000 per charge?
 
Umekalili OS OS OS.
Mbona linux imetengenezwa na Mfinnish na inatumika dunia nzima iliwemk Marekani? Kampuni kibao Marekank zinatumia linux hasa kwenye server side. Android yenyewe ni linux based system.
Biashara ya OS sio kama biashara ya hardware
  • Marekani katengeneza Windows
  • Mfinish katengeneza Linux
Mchina ambaye unasema ni giant kwenye tech ametengeneza OS gani?
Mchina yupo kwa ajili ya kupata hela tu ndiyo maana yupo radhi akopy bidhaa hata brand ya mwenzake ili apige hela tu.
Leo hii kuna iPhone za kichina za Android😁😁😁😁
 
Tukiachana na anga, unaongeleaje byd wang u8 inayotembea km 1000 per charge?
Amejitahidi kwa kiasi chake
Mimi sisemi kuwa Mchina ni mbovu, najaribu kupinga hiyo "FALL OF USA"
Of course as a tech giant, China lazima iwape competition Wamarekani ila haimaanishi kwamba wamarekani wamelala. Sioni China akiipita USA leo wala kesho
 
Amejitahidi kwa kiasi chake
Mimi sisemi kuwa Mchina ni mbovu, najaribu kupinga hiyo "FALL OF USA"
Of course as a tech giant, China lazima iwape competition Wamarekani ila haimaanishi kwamba wamarekani wamelala. Sioni China akiipita USA leo wala kesho
Mkuu kama ulikuwa unafuatilia teknolojia miaka 10 iliyopita kipindi Us alipokuwa relactant, usingeweza kuamini leo tungekuwa tuna compare US na China.

Kama tutakuwa hai tutazidi kukumbushana
 
Android sijui iliweza kusurvive vipi na kuizidi windows phone. Hii ni bahati tu na labda windows alikua hana nyota ya soko la simu.

Mm nmeanza kuandika apps za android zamani sana, lkn android kabla ya version ya KitKat (4.4.2) was trash kiukweli.

Yaan kufanya frauding ilikua rahisi sana. Haikua secure, kuiba data za mtu ilikua kugusa tu, app za kudanganya danganya zilikua kibao.

Na sasa android ikawa adopted kila koma, sio kwenye TV, multmedia sets za kwenye magari, tabs, diagnosis tools, hadi hospital equipments kuna baadhi zinatumia android.
 
Nadhani kuifanya open source na kila mtengeneza simu akawepo kutumia kwenye device zake ikawa kwenye devices nyingi iliwafanya nyie developers mvutiwe nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…