1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Wenzetu wana serikali za wazalendo halisi wanaowaza Nchi yao ya China ,mila zao ,dini zao , utaifa wao, uchina wao na vizazi vyao kwa karne zijazo ,sisi tunawaza Uchaguzi ujao mitano tena na kutafuta misaada ya kushinda uchaguzi kwa kuuza mpaka vyanzo vya kukusanya mapato ya bure kama bandari na mbuga za wanyama na misitu.Kampuni ya kutengeneza magari ya BYD imezindua gari la mfumo wa Plug-in Hybrid Electric Vehicle (PHEV) PHEV ni magari ambayo yana mifumo miwili umeme na mafuta.
Kwa maneno rahisi kama chaji kwenye battery imeisha unatumia mafuta and vice versa. Model hiyo imepewa jina la BYD Qin L.
Ukijaza full tank na ukachaji mara moja tu battery (single charge) chuma inatembea zaidi ya km 2000.
Ilipofanyiwa majaribio ilitembea umbali wa km 2409 kutoka Xian mpaka Changchun.
Km 2400 ni sawa na umbali wa kutoka Dar mpaka Harare, Zimbabwe non-stop.
Rekodi nyingine ya gari hillo ni matumizi kidogo ya mafuta. Linatumia lita 2.9 za mafuta kwa umbali wa km 100 (2.9/100km)
Bei yake ni 14,000 USD (Tsh 36 milioni) hadi 19,000 USD (Tsh 49 milioni) unaanza nayo 0 km.
BYD Qin L imevunja rekodi iliyowekwa na gari lingine la mfumo wa PHEV iliyotembea km 1100.
View attachment 3003231
View attachment 3003234View attachment 3003235
Wenzetu wanawekeza katika Elimu kwa kiwango cha juu sana sisi tunawaza kuwalipa wenza wa wa watawala walioshiba na kusaza nao walipwe bila kufanya kazi.
Je, wenza wa wanajeshi waolala maporini na mbali ya familia zao wao wanalipwa nini na mishahara yao ikoje, hilo hawalijali . Wanakimbilia kwa shemeji zao na wajomba zao uarabuni kuwaleta waje wamiliki ardhi na mali za watanganyika kwa sababu wanajua miaka 50 ijayo mafuta yatakua ni chaguo la pili katika nishati na hawana rasilimali nyingine .
Shame on you African Leaders!!