CHINA: BYD waweka rekodi mpya wazindua gari linaloweza kwenda zaidi ya km 2000 bila kuongeza mafuta wala kuchaji na matumizi kidogo sana ya mafuta

Wenzetu wana serikali za wazalendo halisi wanaowaza Nchi yao ya China ,mila zao ,dini zao , utaifa wao, uchina wao na vizazi vyao kwa karne zijazo ,sisi tunawaza Uchaguzi ujao mitano tena na kutafuta misaada ya kushinda uchaguzi kwa kuuza mpaka vyanzo vya kukusanya mapato ya bure kama bandari na mbuga za wanyama na misitu.

Wenzetu wanawekeza katika Elimu kwa kiwango cha juu sana sisi tunawaza kuwalipa wenza wa wa watawala walioshiba na kusaza nao walipwe bila kufanya kazi.

Je, wenza wa wanajeshi waolala maporini na mbali ya familia zao wao wanalipwa nini na mishahara yao ikoje, hilo hawalijali . Wanakimbilia kwa shemeji zao na wajomba zao uarabuni kuwaleta waje wamiliki ardhi na mali za watanganyika kwa sababu wanajua miaka 50 ijayo mafuta yatakua ni chaguo la pili katika nishati na hawana rasilimali nyingine .

Shame on you African Leaders!!
 
Chama Cha Mambuzi

Dawa yao ni moja tu !
Wakisema Katiba mpya ni mpaka 2026 basi na Sisi tuwaambie uchaguzi uwe 2027 na sio 2025 bila katiba mpya.
Hakuna kuwachagua bila katiba ya kutupa uhuru wa kupata viongozi bara na siasa safi .

Ardhi tunayo
watu tunao
Siasa safi hatuna mana hatuna katiba inayozalisha sheria na kanuni bora za kupata siasa safi na sera nzuri.
Uongozi bora hatuna kwa sababu hatuna katiba bora inayotupa viongozi wa serikali ,bunge na hata kuwapata majaji wenye kusimamia haki bila kiyumbishwa na watawala kwa manufaa yao.

Hakuna haja ya kuendelea,kufanya uchaguzi wa hadaa na ujanja ujanja na kuwasimika viongozi wasiofaa na wasio na uzalendo kwenye utawala huku Taifa letu likiwa linaendelea kutegemea Wazungu na misaada ya masharti ya hovyo huku wachache wakitumia chama cha mapinduzi kusimika watu wao kwa manufaa ya wezi ,walevi na wahuni wachache.
 
50% ya watanzania tungekuwa na misimamo ya aina hii hata hapa tulipo tusingewahi kufika.
 
Sisi tukipata nafasi badala ya kufikiria ubunifu cha kwwnza tunafikiria nitaibaje hapa nisijukikane
 
Hii mentality ya kulaumu serikali kila saa nayo wachina hawana aisee,
Hio BYD ilianzishwa serikali ikaja unga mkono mbele kabisa huko
 
Hii mentality ya kulaumu serikali kila saa nayo wachina hawana aisee,
Hio BYD ilianzishwa serikali ikaja unga mkono mbele kabisa huko
Kama unaona hakuna haja ya kuilaumu serikali lakini unadhani kuna ulazima wa kuwa na serikali ,katiba mifumo ya sheria , usalama ,mifumo ya Elimu ,mifumo ya Kodi ,mifumo ya kifedha ,mifumo ya kisiasa,mifumo ya kusimamia Rasilmali za asili zinazotoka na asili na uumbaji wa Mungu . Basi utakua ni miongoni mwa wapotoshaji na watu wabinafsi kama wananyama wa mwituni hasa nyani!
 
Kazuri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…