Nimefrah San kuona hii pin
M naomba muongozo wa biashara ya viatu ndo nataka nianze na je hizi kampuni za alibaba ni waaminifu kweli kufanya nao biashara? Na Je ni kampuni gani ya shipping iko vizuri kuna hyo silence ocean naonaga watu wanacomplain San kuhus kucheleweshew mizigo, mtandao was taobao mzuri sema n kichina tuuu....
Msaada plz kama una link ya wauza viatu plz mkuu
Kuhusu shipping, HAKUNA kampuni isiyo chelewesha mizigo. HAKUNA! Narudia tena HAKUNA. Unachotakiwa kufanya ni kama una mzigo mkubwa ugawanye na utume kwenye kampuni tofauti ili hawa wakichelewa, hawa wamewahi unakuwa hupotezi wateja . Don't put all your eggs in one basket. Kampuni zipo nyingi sasa hivi na kila siku zinaongezeka. Silent ocean, GNM, Mapembeleo Cargo, Mokha Agency, Hawaii nk nk.
Kuhusu Taobao, Hii huwezi mkuu kununua ukiwa uko bongo kwa sababu hii ni maalumu kwa ajili ya soko la NDANI la china na ni rejareja. Hii utatakiwa kwanza ujisajili, na uwe na bank account ya kichina na sio bank account ya nje kama CRDB au NMB. Pia utahitajika uwe umejiunga na Alipay ambayo itaunganishwa na akaunti yako ya bank ya china. Pia utatakiwa uwe na namba ya simu ya china na hii ndio wasafirishaji wa ndani wa mzigo watawasiliana na wewe wakati wanapokuletea mzigo wako. Mwisho utatakiwa uwe na local chinese address ambapo mzigo ulionunua utafikishwa moja kwa moja. Hivyo ni lazima kuwe na mtu wa kuupokea mzigo wako hapa china. Na wakati mwingine mzigo wanakuwekea kwenye makabati ya kupokea mizigo ambayo yanapatikana kwenye majengo mengi china kulingana na lipi lipo karibu na address yako, kisha unatumiwa code number ya kupokea kupitia namba ya simu. Sasa kama upo TZ nani atapomea? Hivyo kama hujawahi kuishi/kuja China basi Taobao huwezi kuitumia. Pia kuna changamoto ya lugha na inahitaji angalau ujue maneno machache ya kichina au uzoefu wa kudeal na wachina mana si kila wakati apps za translation zitakusaidia. Naandika kwa uzoefu binafsi wa kuitumia taobao kwa zaidi ya miaka 6 sasa.
Kuhusu kununua Alibaba na mitandao mengine, nilishaeleza sana hili. Ila nasisitiza tena na tena, unaweza kununua Alibaba, ila nunua kwa GOLD SUPPLIERS au suppliers ambao WAMEKAGULIWA na alibaba wenyewe na wako VERIFIED. Pia hakikisha malipo na mawasiliano yote unayafanya NDANI ya alibaba. Hii ndio njia salama, na seller akikuzingua unafungua kesi na hela yako inarudi bila presha.
Unaponunua kitu online, usinunue mzigo mkubwa kwanza,nunua sample 1 tu kwanza ije uione, na ukiiridhia ndio uagize mzigo mkubwa, vinginevyo utalia kwa lugha ya kwenu.
Sent using
Jamii Forums mobile app