China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Asante Mkuu!
Kipilipili nimekuwa nikifatilia hii mada toka 2015, nimeishajipanga kimtaji nahitaji msaada wako, kwa kuanzia naomba unipatie no yako. Hongera sana kwa kutupatia maarifa.
 
Habar yako kaka, samahan kwa usumbufu mm ni msichana naitwa Sabrina,Naishi tz ila juz kat nimepata fursa ya biashara China, yan kuchukua madera tz kupeleka China kuuza ,shida yangu ni moja jinsi ya kupeleka mzigo China na changamoto zake zipoje,na je ktk pita pita zako ushawai ona biashara ya madera huko China ,na wanauza kwa yuan ngapi?
Da Sabrina unachukua madera Bongo na kupeleka China au kutoa China kuleta bongo. Ama ndo yametimia ya kuwauzia wao mitumba
 
Nimefrah San kuona hii pin
M naomba muongozo wa biashara ya viatu ndo nataka nianze na je hizi kampuni za alibaba ni waaminifu kweli kufanya nao biashara? Na Je ni kampuni gani ya shipping iko vizuri kuna hyo silence ocean naonaga watu wanacomplain San kuhus kucheleweshew mizigo, mtandao was taobao mzuri sema n kichina tuuu....
Msaada plz kama una link ya wauza viatu plz mkuu
 
kuhusu masoko ya viatu kama utasafiri kuja china utayapata guangzhou.Ila kama utataka kununua mtandaoni alibaba basi malipo ufanyie kwa platform yao ili kama supplier akisumbua uweza kulalamika.Usikubali supplier akwambie ufanye payment kwa wire transfer kwenda kwenye acc yake ya bank.Pia jitahid kununua kwa gold suppliers.
kuhusu kusafirisha kuna makampuni meng ukiachana na silent ocean.Kuna GNM,ZAZEME na zingine nyingi.Nadhan ukiukagua huu uzi utaona kuna sehemu nilishare contacts zao.Good luck mkuu
 
wadau, naitaji maelekezo ya wapi ntapata chupi za kike na boxer za kiume zenye ubora nje ya nchi hususani china.
 
Mkuu Kipilipili, naweza kupata plastic pollen traps baada ya muda gani kutoka kwa jamaa zako? Naomba namba yako ya simu tafadhali.
Sasa hivi ni mapumziko ya chinese spring festival, hakuna shipping line zinazofanya kazi na baadhi ya viwanda vimefunga. Kawaida kiuzoefu usafiri wa meli ni siku 45-60. atakaekwambia ni siku 25 muogope kama ukoma (makampuni mengi husema ni siku 25 ila utasubiri na zitapita na utaishia kulalamika tu).

Simu mara nyingi sitoi, niliwahi kuweka namba ya simu kwenye huu uzi halau baadae niliitoa, BAADHI ya watu si waungwana humu kabisaaaaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar yako kaka, samahan kwa usumbufu mm ni msichana naitwa Sabrina,Naishi tz ila juz kat nimepata fursa ya biashara China, yan kuchukua madera tz kupeleka China kuuza ,shida yangu ni moja jinsi ya kupeleka mzigo China na changamoto zake zipoje,na je ktk pita pita zako ushawai ona biashara ya madera huko China ,na wanauza kwa yuan ngapi?
Mkuu, hii NAHISI kama ni kinyumenyume, ni sawa na kutoa korosho DSM kupeleka mtwara kuuza.
Viwanda vya madera vipo China, hata yale madera ya muhindi au yale ya uturuki mengi huzalishwa china. Sijajua wewe unataka china umuuzie nani?
Binafsi naona kama hii imekaa kinyume nyume na kuwa makini usije ukapigwa na wajanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simu kwa kweli sitoi mara nyingi. Mwenye lolote aulize hapa hapa ili wengine wafaidike. Ikiwa ni lazima sana kuwasiliana na mimi basi PM nitakupa email na sio simu. Mara chache sana natoa simu
Kipilipili nimekuwa nikifatilia hii mada toka 2015, nimeishajipanga kimtaji nahitaji msaada wako, kwa kuanzia naomba unipatie no yako. Hongera sana kwa kutupatia maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefrah San kuona hii pin
M naomba muongozo wa biashara ya viatu ndo nataka nianze na je hizi kampuni za alibaba ni waaminifu kweli kufanya nao biashara? Na Je ni kampuni gani ya shipping iko vizuri kuna hyo silence ocean naonaga watu wanacomplain San kuhus kucheleweshew mizigo, mtandao was taobao mzuri sema n kichina tuuu....
Msaada plz kama una link ya wauza viatu plz mkuu
Kuhusu shipping, HAKUNA kampuni isiyo chelewesha mizigo. HAKUNA! Narudia tena HAKUNA. Unachotakiwa kufanya ni kama una mzigo mkubwa ugawanye na utume kwenye kampuni tofauti ili hawa wakichelewa, hawa wamewahi unakuwa hupotezi wateja . Don't put all your eggs in one basket. Kampuni zipo nyingi sasa hivi na kila siku zinaongezeka. Silent ocean, GNM, Mapembeleo Cargo, Mokha Agency, Hawaii nk nk.

Kuhusu Taobao, Hii huwezi mkuu kununua ukiwa uko bongo kwa sababu hii ni maalumu kwa ajili ya soko la NDANI la china na ni rejareja. Hii utatakiwa kwanza ujisajili, na uwe na bank account ya kichina na sio bank account ya nje kama CRDB au NMB. Pia utahitajika uwe umejiunga na Alipay ambayo itaunganishwa na akaunti yako ya bank ya china. Pia utatakiwa uwe na namba ya simu ya china na hii ndio wasafirishaji wa ndani wa mzigo watawasiliana na wewe wakati wanapokuletea mzigo wako. Mwisho utatakiwa uwe na local chinese address ambapo mzigo ulionunua utafikishwa moja kwa moja. Hivyo ni lazima kuwe na mtu wa kuupokea mzigo wako hapa china. Na wakati mwingine mzigo wanakuwekea kwenye makabati ya kupokea mizigo ambayo yanapatikana kwenye majengo mengi china kulingana na lipi lipo karibu na address yako, kisha unatumiwa code number ya kupokea kupitia namba ya simu. Sasa kama upo TZ nani atapomea? Hivyo kama hujawahi kuishi/kuja China basi Taobao huwezi kuitumia. Pia kuna changamoto ya lugha na inahitaji angalau ujue maneno machache ya kichina au uzoefu wa kudeal na wachina mana si kila wakati apps za translation zitakusaidia. Naandika kwa uzoefu binafsi wa kuitumia taobao kwa zaidi ya miaka 6 sasa.

Kuhusu kununua Alibaba na mitandao mengine, nilishaeleza sana hili. Ila nasisitiza tena na tena, unaweza kununua Alibaba, ila nunua kwa GOLD SUPPLIERS au suppliers ambao WAMEKAGULIWA na alibaba wenyewe na wako VERIFIED. Pia hakikisha malipo na mawasiliano yote unayafanya NDANI ya alibaba. Hii ndio njia salama, na seller akikuzingua unafungua kesi na hela yako inarudi bila presha.
Unaponunua kitu online, usinunue mzigo mkubwa kwanza,nunua sample 1 tu kwanza ije uione, na ukiiridhia ndio uagize mzigo mkubwa, vinginevyo utalia kwa lugha ya kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri wa BURE. Kama unataka china na uzipate kwa bei rahisi basi jipange kuchukua mzigo mkubwa. Ntakupa mfano hai. Kiwandani ili wakuuzie kwa bei ya kiwanda chupi ya Aina moja Basi wanataka kwa kila aina ununue kuanzia 6000pcs na bei yao inakuwa poa around 1yuan-2yuan kwa kila chupi kulingana na aina na ubora unaotaka. Chini ya hapo hawataki mana hujafikia MOQ(Minimum oder quantity).
Kama unataka chini ya hapo inabidi sasa uingie mtaani maduka ya wachuuzi wa jumla ambao wao wamenunua viwandani. Hawa bei zao sio rafiki.
Bongo unaweza kukuta chupi inauzwa 2000 usitarajie kwa mfano ukiagiza china pc100 basi utazipata kwa bei rahisi. Wengi tumezoea Tanzania pc5 au 10 ni jumla, hiyo kwa mchina ni rejareja tu . Kila kiwanda kinakuwa na MOQ yake ila kama unataka kufanya serious businesa basi jipange kuchukua mzigo mkubwa.
Kama huna uwezo wa kuja mwenyewe china, basi agiza wafanyabiashara wakubwa wanaokuja china ambao wana kampuni zao Tanzania au wana maduka Tanzania. Kama pia hujawa na uzoefu wa kuagiza online basi agiza kupitia hao wafanyabiashara wakubwa na ingia nao mkataba wa kisheria ili incase of anything uwe na pakusimamia. Kama unataka kuagiza online basi agiza sample kwqnza ije uione kisha ukiridhika ndio uagize mzigo mkubwa.
Siwezi kusema exactly wapi bongo utawapata hao wafanyabiashara wakubwa ila naamini ukifanya utafiti hasa kariakoo utawapata. kila la heri
wadau, naitaji maelekezo ya wapi ntapata chupi za kike na boxer za kiume zenye ubora nje ya nchi hususani china.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom