China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Kweli inafaa ukaanza kuangalia biashara kwa mtindo tofauti wakati wa muda wa mapumziko. Tembelea Amazon.com angalia jinsi wanavyouza vitu na kisha tembalea Alibaba.com uone wanavyozalisha. Kwa wale ambao wameishi Ulaya na Amerika wajua jinsi wanavyonunua kwenye soko la Amazon.com. Biashara inayofanyika ni kununua vitu Alibaba.com kwa bei ndogo na kuuza Amazon.com kwa bei ya juu. That's it. Ingawa inahitaji kujifunza na tricks kidogo hasa sisi tunaotoka Africa lakini inafanyika.

mkuu, hebu funguka kwa kirefu kwa faida ya wengine
 
mkuu, hebu funguka kwa kirefu kwa faida ya wengine

Mkuu kinachofanyika hapa ni sawa tu kununua vitu China na kuuza kwenye masoko makubwa hapa nchini kama Nakumatt, The Game, Pick and Pay, n.k. Tofauti ni kuwa badala ya kuuza hapa nchi unaviuuza kwenye masoko makubwa AmAZON AU eBAY duniani. Tofauti nyingine ni kuwa huendi China wala USA/UK kuuza. Amazon wana mfumo unaokuwezesha kusafirisha vitu kwako mpaka kwao unaitwa FBA-Fulfillment By Amazon. Ukishanunua vitu vyako China wanakusafirishia mpaka Amazon kisha wanavitunza kwenye store yao. Kazi yako wewe nikuvi list kwenye Amzano.com kuonyesha picha na maelezo yake nakuanza kufanya marketing. Kikubwa hapa ni kupata reviews za bidhaa zako ili ziweze ku rank higher na kuanza kupata wateja.

Vintage_Retro_Pu_Leather_Stand_mobile_phone.jpg_220x220.jpg
Mfano hii ni Iphone 6 cover, Alibaba wanauza US $1-5 / Piece( FOB Price) na min order ni 500 negotiable
21MCB6oHOWL.jpg
. Ukienda Amazon.com, cover ile ile
Phone 6 Case, Spigen [HEAVY DUTY] Tough ArmorCase for iPhone 6 (4.7-Inch) - Gunmetal (SGP11022) wanaiuza $ 17. Walichofanya hapa ni wamei brand tu


Unaweza kuona potential iliyopo kwenye masoko haya. Na ukifanya marketing vizuri unaweza kuuza hapa piece 20 kwa siku. Assume una biashara kama hizo 3 au nne hivi. Haya yanafanyika kwenye computer bila hata kunyanyuka nyumbani kwako.

Lakini kama nilivyosema inahitaji kujifunza na watu hasa watumiaji wa mitandao wasitumie kwa kutumiana vichekesho tu ila watumie kwa kufanya biashara za uhakika. Wanachuo na watu wenye muda wa ziada na mtaji kidogo say $ 200 wanaweza kuanza biashara hii.

P.S Watu wanadhani bidhaa za China zina quality ndogo lakini siyo kweli, China wanakuuzia quality unayotaka. Kwa USA na Ulaya huwezi ingiza kama hizi zinazokuja kwetu.

PPS. Watu watafikiri ni mtaji mkubwa, hata unaweza kujaribu kwa kuleta sample na kuuza katika masoko yetu hapa nchini, Nakumatt, The game n.k kuna fursa hiyo ili product yako uijue vizuri.

PPPS. Bandiko hili linaweza kusomwa pamoja na lingine lililoko humu ndani linalosema kununua vitu Amazon. Somo ni refu sana ila inawezekana hakuna pesa rahisi.

Samahani kwa mwandiko mbaya, I am not so much used to the writing stuff.

 
Duu mkuu umenitoa matongotongo kiukweri endelea kutuamsha tulio lala
 
Manake fursa zipo sema kuzifikia ndio inakushida kutokana kutojua mambo kiupana zaidi
 
Mkuu, hili bandiko aliweka mwenzetu humu ndani, ila linaelezea kununua tu Amazon, nimeziba mwanya kwa kuonesha unaponunua Amazon wao wanaokuuzia hununua Alibaba.com China. Hivyo tuwe makini na bidhaa hizi, tunaambiwa kuna ni za USA au Ulaya kumbe nao baadhi ya bidhaa zao hunuunua China. Unaweza kusoma kwa pamoja ili kupata uelewa zaidi.


Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)


Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo. Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni 1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address 2:Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania) 3:Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1:CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2:KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3:KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4:KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?
hii iko hivi.... 1:Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted. 2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.comhii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao
Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2:COMGATEWAY
link-http://comgateway.com/ hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na uona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3:BORDERLINX
link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4:SHIPITO
link-USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5:STACKRY
link- Stackry - US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi. STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU please evaluate kindly.

nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi . maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila ithink there r limits.. help Mwl.RCT
Last edited by JZHOELO; 6th November 2014 at 23:17.​
 
Mkuu kinachofanyika hapa ni sawa tu kununua vitu China na kuuza kwenye masoko makubwa hapa nchini kama Nakumatt, The Game, Pick and Pay, n.k. Tofauti ni kuwa badala ya kuuza hapa nchi unaviuuza kwenye masoko makubwa AmAZON AU eBAY duniani. Tofauti nyingine ni kuwa huendi China wala USA/UK kuuza. Amazon wana mfumo unaokuwezesha kusafirisha vitu kwako mpaka kwao unaitwa FBA-Fulfillment By Amazon. Ukishanunua vitu vyako China wanakusafirishia mpaka Amazon kisha wanavitunza kwenye store yao. Kazi yako wewe nikuvi list kwenye Amzano.com kuonyesha picha na maelezo yake nakuanza kufanya marketing. Kikubwa hapa ni kupata reviews za bidhaa zako ili ziweze ku rank higher na kuanza kupata wateja.

Vintage_Retro_Pu_Leather_Stand_mobile_phone.jpg_220x220.jpg
Mfano hii ni Iphone 6 cover, Alibaba wanauza US $1-5 / Piece( FOB Price) na min order ni 500 negotiable
21MCB6oHOWL.jpg
. Ukienda Amazon.com, cover ile ile
Phone 6 Case, Spigen [HEAVY DUTY] Tough ArmorCase for iPhone 6 (4.7-Inch) - Gunmetal (SGP11022) wanaiuza $ 17. Walichofanya hapa ni wamei brand tu


Unaweza kuona potential iliyopo kwenye masoko haya. Na ukifanya marketing vizuri unaweza kuuza hapa piece 20 kwa siku. Assume una biashara kama hizo 3 au nne hivi. Haya yanafanyika kwenye computer bila hata kunyanyuka nyumbani kwako.

Lakini kama nilivyosema inahitaji kujifunza na watu hasa watumiaji wa mitandao wasitumie kwa kutumiana vichekesho tu ila watumie kwa kufanya biashara za uhakika. Wanachuo na watu wenye muda wa ziada na mtaji kidogo say $ 200 wanaweza kuanza biashara hii.

P.S Watu wanadhani bidhaa za China zina quality ndogo lakini siyo kweli, China wanakuuzia quality unayotaka. Kwa USA na Ulaya huwezi ingiza kama hizi zinazokuja kwetu.

PPS. Watu watafikiri ni mtaji mkubwa, hata unaweza kujaribu kwa kuleta sample na kuuza katika masoko yetu hapa nchini, Nakumatt, The game n.k kuna fursa hiyo ili product yako uijue vizuri.

PPPS. Bandiko hili linaweza kusomwa pamoja na lingine lililoko humu ndani linalosema kununua vitu Amazon. Somo ni refu sana ila inawezekana hakuna pesa rahisi.

Samahani kwa mwandiko mbaya, I am not so much used to the writing stuff.


mim naomba tuu no.yako mkuu au email niwasiliane nawe zaidi
 
Ebwa ee let 2 ask ma quention kidogo nataka kufaham kuhusu manunuzi ya phone kule china yamekaaje ama uwe la kamtaji ka uwezo gani kwa watu wa hali ya chini namanisha kianzio cha mtaji
 
Ebwa ee let 2 ask ma quention kidogo nataka kufaham kuhusu manunuzi ya phone kule china yamekaaje ama uwe la kamtaji ka uwezo gani kwa watu wa hali ya chini namanisha kianzio cha mtaji

Mkuu, asante kwa swali ila swali hili limeshajibiwa, naomba fuatilia post za nyuma kwenye thread hii.
Karibu tena
 
Duu sasa ndugu uwezi kunishibisha hatakama sijauzulia kwenye msiba lkn kwenye mazishi nipo mdau
 
Poa mdau nimekusoma kwa mfano wagiza mzigo na kama tunavofaham dunia kama kijiji na kuhusu swala la wizi jamaa wajipanga Boraa manake kuna jamii nyingine ipo ki wizieizi zaidi
 
Poa mdau nimekusoma kwa mfano wagiza mzigo na kama tunavofaham dunia kama kijiji na kuhusu swala la wizi jamaa wajipanga Boraa manake kuna jamii nyingine ipo ki wizieizi zaidi

a Comment or question?sijakuelewa
 
Habari wana jukwaa,

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabishara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki, vifaa vya electronics nk. Najua kuna thread nyingi zimewahi kuzungumzia biashara za China, lakini nimuombe mkuu Invisible aifanye hii iwe sticky thread ili iwe refernce point kwa kila anaehitaji kufanya biashara China.

Nitaeleza KIDOGO Kuhusu biashara za China.
BIASHARA YA NGUO: hii inapendwa sana kufanywa na kina dada japo wanaume pia wapo. Wengi walio wageni na biashara hii wamejikuta wakipata hasara hasa wanapofika tu miji kama Guanzhou na kuanza kununua nguo bila kuangalia hali ya soko Tanzania ikoje.

Hujikuta wakinunua nguo on their perspective and not customers perspective! Kinachowavutia machoni mwao ndicho wanachonunua kwa matarajio watauza tu. Wengine wananunua na wanapofika na mzigo kariakoo wanakuta mzigo kama huo uloshaingia a week/month before hivyo kujikuta wanauza kwa bei ya hasara.

Ushauri: jaribu kutafuta wateja kabla Tanzania , wakupe order na sample kisha ukifika China nunua kile walichokuagiza.Pia jitahidi ujue ni fashion gani bongo iko sokoni na mpaka mzigo umefika bongo,je bado hiyo fashion ulionunua itakuwa inauza? Mind you kwamba biashara ya nguo hasa za WANAWAKE zinaendeshwa kwa nguvu ya soko na fashion hubadilika mara kwa mara!Biashara ya nguo za watoto au wanaume kidogo fashion zake zinakaa muda mrefu ukilinganisha na za wanawake.

BIASHARA YA VIFAA VYA ELEKTRONIKI kama simu na accessories zake, music system n.k
Miji mizuri ya kununua mzigo kwa biashara hii ni Shenzhen na Honkong ,japo mji wa Guanzhou pia ni maarufu isipokuwa fake products kwa Guanzhou ni kubwa zaidi. Changamoto kubwa ya biashara hii ni FAKE PRODUCTS. Angalia wateja wako ni watu wa namna gani. Most low income earners ambao kwa Tanzania ndio wengi, wanapenda cheap price.

Kwahiyo, ukinunua genuine products huwezi kuuza bongo kwa sababu bei itakuwa iko juu na wao watashindwa. Kwa hiyo jua needs and wants za customers wako kabla hujaamua kununua mzigo.Kwa mtu mwenye mtaji mdogo unaweza kuanza na kununua phone acssesories na simu chache tu za bei ya chini, utakuwa unaongeza idadi ya simu kidogo kidogo kadri mtaji unavyokua.Pia kama una mtaji mkubwa unaweza kuingiza used products kama photocopier machines ila jitahidi uwe na orders kabla hujaleta kwa sababu ukija nazo nyingi bila order zinaweza kukaa muda mrefu ukajikuta unaanza kula mtaji.

Wakati unasafirisha photocopier machines jitahidi ununue vitu vidogo vidogo kama vile memory cards, USB cards, power banks nk na uviweke pamoja ndani ili ukija bongo wakati unasubiri kuuza photocopier machines unauza hivyo vitu vidogo vidogo ili kupata faida kidogo kidogo na kuhakikisha huli mtaji.

Kumbuka hapa utasafirisha kwa meli na huwa wanapima CBM na sio uzito kwa hiyo hivyo vitu vidogo vidogo cost yake ya kusafirisha itakuwa imemezwa na hizo machines.Photocopier machines nimetoa kama mfano wa moja ya bidhaa lakini vipo vimashine vingi tu ambavyo unaweza kusafirisha kama:Mashine za juice ya miwa, hizi zimekuwa na demand kubwa sana kwa sasa Tanzania. Wateja wake wapo , kama utakuwa na mtaji mzuri unaweza kununua hizi na kuleta. Nyingi ni portable na modern. Ni kiasi cha kutafuta orders na kisha kuleta.
Kuangalia bei mbalimbali za bidhaa tembelea:
http://www.alibaba.com/

http://m.made-in-china.com/

www.taobao.com (hii ni ua kichina, tumia browser ya google chrome na tumia kitufe cha translation ili ije kwa kingereza)

USAFIRI: Zipo kampuni nyingi zinazosafirisha mizigo kwa njia ya ndege na meli. Kampuni kama THE LAND, SILENT OCEAN ni baadhi tu na hizi zina ofisi zao pale pale Guanzhou na bei zake zinatofautiana kutegemeana unasafirisha kwa njia gani yaani ndege au meli. Na unapolipia wao ndio huhusika na clearance na kila kitu, wewe ukifika bongo unachukua tu mzigo wako kwenye Ghala lao.
Website ya baadhi ya makampuni ni:
http://www.silentoceanlimited.com/

NAULI:nauli zinategemea season na pia unataka kusafiri lini. Kipindi cha high season kama ,july, august bei zinakuwa juu. Kama kwa mfano unatarajia kusafiri July basi ikifika april kata tiketi mapema . Mara nyingi kunakuwa na offer kwenye mashirika ya ndege kwa hiyo pendelea kutembelea website zao.
Pia nauli inategemea na shirika la ndege unalotaka kusafiria na pia daraja unalotaka kukaa.
Kwa wafanyabiashara wengi hutumia ethiopian airline kwa sababu huwa wanatoa kg nyingi kuliko wengine.
Pita kwa mawakala posta na kariakoo au search google kupata bei mbalimbali za nauli. Unaweza kutenga bajeti ya USD 900-1200 Kwa nauli kwa economy class
Angalia bei za NAULI hapa:
http://www.ethiopianairlines.com/en/default.aspx

http://www.qatarairways.com/global/en/homepage.page

https://www.klm.com/?_e_pi_=7,PAGE_ID10,8626374365


MALAZI: Hapa nitazungumzia mji wa Guanzhou ambao ndio wenye wafanyabiashara wengi wa mataifa mbalimbali hasa Afrika. Zipo hoteli za hadhi tofauti, bei kutoka 120 yuan(36,000 Tsh) ikiwa ni bei ya chini labisa na kuendelea kutegemeana na mfuko wako. Maeneo kama "shaobei lu" ni maarufu kwa watu weusi na utakisikia kiswahili kila baada ya hatua kadhaa. Hoteli za pembeni ya mji bei huweza kuwa chini mpaka yuan 100.
Angalia range ya bei za hoteli hapa:
http://www.chinahotelsreservation.com/GuangZhou/


CHAKULA: zipo hoteli nyingi Guanzhou na shenzen zinazomilikiwa na foreigners na wanauza chakula kizuri japo kiko ghali kidogo, ila kama unahitaji chakula cha bei ya chini na ambacho ni HALAL (wengi huhofia kulishwa mbwa,kitimoto,nk) unaweza kula kwenye sehemu nyingi ambazo huuza wachina waislamu wenye asili ya Xinjiang ambao huuza HALAL food kwa bei poa kuanzia Yuan 15(4500 Tsh) na kuendelea kutegemea na aina ya chakula ulichoagiza. Kuwa makini na vyakula mana wale wenzetu huwa wanakula vyakula vingi vya "ajabu ajabu".

LUGHA: wachina hutumia lugha yao kwa kila kitu. Katika miji ya biashara kama Guangzhou wachina wafanyabiashara huongea kingereza cha mawasiliano(kibovu) ila mnawasiliana na kuelewana. Pia lugha ya ishara inatumika pale panapokuwa na language barrier . Hata kama hujui kabisa kingereza unaweza kuchagua bidhaa na kisha mkapatana bei. Wenzetu wana utaratibu wa kutumia calculator kukuandikia bei, hivyo na wewe utaandika ya kwako mpaka mtafikia makubaliano. Nashauri download application yoyote ya TRANSLATION kama pleco nk ili ikusaidie kwenye mawasiliano unapokwama andika neno unslohitaji kwa kingereza kisha tafsiri kwa kichina na muoneshe mchina hilo neno, itasaidia kurahisisha mawasiliano

Nimegusa juu juu vitu vichache mno kuchokoza mada ili wengine waongezee uzoefu na iwe msaada kwa kila anaetaka kufanya biashara China.

Karibuni tujadili na kusaidia wengine

upuuzi mtupu.miaka 50 hamsini ya Uhuru bado tunaenda kuchukua nguo.vyombo ,chupi,soksi.hivi watanzania ni vilema hatuwezi kutengeneza hivi vitu.huko China wataolewa wengi sana.nakumkumbuka sana nyerere
 
Last edited by a moderator:
upuuzi mtupu.miaka 50 hamsini ya Uhuru bado tunaenda kuchukua nguo.vyombo ,chupi,soksi.hivi watanzania ni vilema hatuwezi kutengeneza hivi vitu.huko China wataolewa wengi sana.nakumkumbuka sana nyerere

Mkuu labda tuanze na wewe, umeshatengeneza kipi labda?umewahi kutengeneza japo SINDANO tu ya kushonea nguo ili watanzania wenzio tutumie?....
MY TAKE: usituharibie uzi, kama huu ni "upuuzi" basi wewe pita kimya tu. Tuache tujadili "upuuzi" wetu. Wewe baki na ujanja wako.
 
Back
Top Bottom