China itapata wakati mgumu sana kwa Taiwan kuliko Russia kwa Ukraine

Mmmh hapana! Ninataka kumaanisha kuwa yaani China isionekane ya kinyonge mzee kwa dunia ya sasa
Sijakataa bwashee ,China ni taifa kubwa tena lenye uchumi mkubwa duniani kuliko nchi zote sijasema atashindwa Bali nazungumzia changamoto ngumu atakazokumbana nazo
 
Napingana na wewe kabisa.
Wapi umepata hiyo habari kuwa kuna kambi ya jeshi ya Marekani Taiwan na kuwa kuna wanajeshi wa Marekani 20,000?

Hakuna kambi ya jeshi ya Marekani Taiwan. Kuna wanajeshi 31 tu wa Marekani Taiwan. Waliongezeka mwaka jana toka 20.

Na sababu ya Marekani kutaka Taiwan isiwe sehemu ya China ni hili iweze kuweka base pale.

Na sababu pekee Marekani inaitetea Taiwan ni ili kuibana China na kuinyima access ya bahari ili kuidhibiti kiuchumi. Hakuna lingine.

Ukiangalia kwenye ramani, hapo Taiwan ndiyo sehemu pekee iliyobaki ambayo China ina control na kupitisha mizigo yake. Maana upande mwingine ni South Korea na Japan, upande mwingine ni Philippines na visiwa vyake. Taiwan ipo katikati.

Pia ndiyo sababu hiyohiyo Marekani inataka Hong Kong ijitenge Na China. Kwa kuwa ikitoka ina maana Guangzhou litakuwa hatarini kushuka sana kiuchumi.

Hakuna sijui kuitafutia uhuru Taiwan wala nini. Ni propaganda za kipuuzi tu.

Wabongo tutumie muda japo kuidogo kufungua ramani ili uweze kuelewa haya mambo.
 
Ni base gani ya marekani ipo Taiwan ? Na ipo Taiwan sehemu gani?🤔
 
Biti tuu hilo mama anaenda na hawamfany kitu,China alipigwa biti moja tu ole wake aisaidie Russia mpaka leo mkia makalion ,tuone biti lake,US anawaona kama walevi wa madaraka tuu. Mtu ukikaa sana madarakani unapungukiwa akili
China aisaidie Russia katika nini ? 🤔
 
Vita ni zaidi ya hayo uliyoandika mzee,
 
Wewe ndio umeongea kisomi zaidi . heko kwako👍
 
We nawe ,eti kuna wanajeshi 20 ,ila hakuna Base, nenda kachimbe zaid mzee ,base ziko mbili ambazo zinaendeshwa na base kubwa iliyo kisiwa cha Japan kinaitwa Okinawa, walianza na wanajeshi 39 sasa hivi ni zaid ya 2,0000 kaa na matango pori yako
 
Halafu hako kanorth korea ndo kanamtishia USA jamani....tuwe wapole tu
 
Unajua ni mara ngapi China ameingia katika Air defense identification zone ya Taiwan? Mwezi January pekee china imeingiza warplanes, including fighters na bombers zaidi ya 30 je unajua why wanafanya hvyo.


Taiwan wamezoea uchokozi huu wa China na siku ya Kushambuliwa wanaweza kujua ni kawaida ya China kupitisha ndege zake katika defense identification zone ya Taiwan kumbe siku hyo China ndo anavamia so wkt mnapambana angani huku kwingine watu wanaingia

Kingine inapotokea katika vita ww ukawa uko kwenye defense mode tofauti na attack mode mwenye defense mode anakuwa na wakt mgumu sana na katika vita nying mara nying alie ktk defense mode wanashandwa vita coz itakulazimu utumie silaha kubwa au gharama kubwa kuliko alie ktk attack mode yeye anatumia silaha kutokana na mahitaji au hali ya uwanja wa vita so ni kichekesho kusema kati ya Taiwan na China , Taiwan atampiga Mchina so automatic Taiwan atakuwa kwenye Defense mode na China Kwenye attack mode

Kingine Base zote za US zinajulikana zilipo pia unatakiwa kujua China ana the Biggest Navy in the world kumshinda US pia hypersonic missiles ambazo kwa technology iliyopo kwa sasa hakuna air defense yeyote yenye uhakika wa kuzizuia
 
We nawe ,eti kuna wanajeshi 20 ,ila hakuna Base, nenda kachimbe zaid mzee ,base ziko mbili ambazo zinaendeshwa na base kubwa iliyo kisiwa cha Japan kinaitwa Okinawa, walianza na wanajeshi 39 sasa hivi ni zaid ya 2,0000 kaa na matango pori yako
Leta link acha propaganda na story za vijiweni kijana. Leta link inayosema kuna kambi ya jeshi ya Marekani Taiwan na kuna wanajeshi 20,000 wa Marekani.

Embu waza hili kidogo, yaani China waruhusu Marekani wajenge kambi na kuwa na wanajeshi 20,000 Taiwan alafu waje kupiga kelele na kutishia vita kisa Speaker wa Bunge la Marekani anataka kutembelea Taiwan? Inaingia akilini kweli hiyo.

Mimi nakupa hizi link kudhibitisha kuwa kuna wanajeshi 31 tu wa Marekani Taiwan. Unaweza google we mwenyewe ujionee. Kawa danganye vijiweni kule siyo hapa.


 
Endelea kutoa somo kwa hawa vijana wa humu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…