China itapata wakati mgumu sana kwa Taiwan kuliko Russia kwa Ukraine

wape somo vijana wa humu jf.
 
Hizo Mbwembwe na propaganda za USA, Taiwani itapigwa tu..Jana Biden kapewa onyo na Rais wa China
kwamba asichezee moto.
Mwenzako ameongea kwa weledi wewe unaongea tayari bangi imeshakutosha kichwani, jihadists ni shida sana. Itabidi tu muikubali elimu dunia mpende msipende.
 

Kuivamia Taiwan, China atalazimika kufanya military buildup ambayo lazima itakuwa detectable tu, na onyo litatolewa kama ambavyo onyo lilitolewa kabla ya Urusi kuivamia Ukraine.
 
Duuu apa kuna madini ya kutosha ngoja kwanza uzi usonge mbele
 
Hili uliloandika kwamba, [Na sababu pekee Marekani inaitetea Taiwan ni ili kuibana China na kuinyima access ya bahari ili kuidhibiti kiuchumi. Hakuna lingine] sio kweli kwani China bado ina access kubwa sana na bahari hata ukiangalia hiyo ramani yako.

Sababu alizozitoa mleta mada ni za ukweli kabisa. China kuivamia Taiwan ina hasara kuliko faida na wangekuwa wa kujaribu wangeisha jaribu ila wamebaki na vitisho tu.
 
Ni kweli walilonga masaa meng ila sidhani kama walikua wanatukanana au kutifuana ,ni mazungumzo ambayo yaliishia kwa kutoelewana kwa kila mmoja ,unajua kwenye kutoelewana kutokana na hasira upande mmoja ukizidiwa unaweza to a matamshi ambayo kiuhalisia hayawezekani ,mfano unaweza mwambia mtu ntakuua lakin hasira zikiisha huwez fanya hivyo ,mchina alikasirika ila sasa hivi ile kauli anatamani aifute ,maana kiuhalisia hawez Fanya chochote zaid alikua kakasirika tuu
 
Ramani niliyo weka hii hapa. Niambie Marekani wakiweka base Taiwan, access kubwa ipi unayosema China inayo?

Kumbuka, Marekani ina kambi za Jeshi 73 hapo South Korea, inazo 119 hapo Japan.

Pia ukiangalia vizuri hiyo ramani, hapo mbele ya East China Sea kuna kisiwa hapo akija andikwa jina, ni Okinawa ambapo Marekani ana kambi za Jeshi pia.

Huku Philippines ana kambi za jeshi, pembeni ya Hong Kong kuna Thailand anayo Pia, ukisogea pembeni ya Philippines kuna Malaysia anayo pia. Hiyo access kubwa ya bahari unayosema ni ipi?

Marekani akifanikiwa kuweka kambi Taiwan, atakuwa amemkaba sana China kwenye access ya Bahari.

Na tunavyo zungumzia access ya bahari kwenye hii post, tuna maanisha access za kupitisha meli kusafirisha mizigo siyo kuwa na pwani.

 
China ni massive na jeshi lake ni massive pia pia Marekani hawezi ku wage war maelfu ya km away halafu aishinde taiwan iliyoko 170 tu .
Brilliant!! Mkuu thanks a lot kwa hoja yako yenye mshiko - kinacho nishangaza mimi ni watu kushindwa au kupuuzia kuangalia ramani wakatafakari umbali wa kutoka mashariki au magharibi ya pwani ya Merikani kuja kwenye bahari ya Uchina kuna umbali gani? Tukiwekea maanani kwamba Uchina ya sasa sio ya mwaka 47 Wachina siku hizi wamejizatiti sana katika masuala ya Navy, hasa hasa their formidable anti ship missiles especially: air craft carrier killer missiles type DF-36 zenye uwezo mkubwa wa kuzamisha aircraft carriers hata zikiwa in mid Pacific or Atlantic oceans, hapo hatujazungumzia MACH 15/20 Hypersonic Missiles ambazo US na UK hawana kinga dhidi ya makombora hayo hatari yenye uwezo vile vile wa kuzamisha aina zote za meli za kivita-sasa swali hapa ni: hivi US/UK watapitisha wapi meli za kuwezesha kuiwekekea blockade Uchina kwenye eneo la Taiwan Strait au strait of Malacca-kwa maneno mengine meli za NATO specifically US zitapitia wapi kabla hazijazamishwa na Uchina wakati teknolojia ya siku hizi ni rahisi kuiwezesha Uchina ku-track nyenendo za Meli za kijeshi za USA in real time kwa kutumia satellites za aidha Uchina au Urusi au Iran au zote kwa pamoja zikawezesha missiles ku-zero on US/UK Naval ships na kuzizamiswa katikati ya Bahari za Pacific au Atlantic kabla hazijafika Uchina.

Haya tuje kwenye suala la idadi ya Military bases ambazo Merikani anamiliki mashariki ya mbali, binafsi naona hiyo si hoja ya kuzitia wasi wasi Uchina au Urusi kambi hizo zote zinaweza kushambuliwa na kuchakazwa vibaya kwa makombora hatari ya Kichina na Urusi hata Korea ya Kasikazini uwezo huo wanao sana,na kusema kweli ukichunguza kwa umakini military bases hizo za kimerikani wala hazina military assets/materiel nyingi kivile na idadi ya wanajeshi wanao ishi kwenye makambi hayo niya kawaida kabisa, hivyo maadui wake ni rahisi kuzi-contain bases hizo in no time.

Ebu sasa tuangalie mfano mmoja kuhusu umakini pamoja na Ulinzi in general wa Military bases za Wamerikani around the World: kama nakumbuka vizuri miaka miwili/mitatu iliyo pita kambi mbili za jeshi la Merikani zilishambuliwa na roketi za Wairan, zikaharibu majengo kadhaa ya kambi na kutifua runways za ndege - wanajeshi kadhaa wa Merikani walipata madhara licha ya kujichimbia/jificha kwenye mahandaki yaliyo imarishwa kwa zege, walipo tonywa mapema kwamba Iran hiko mbioni kushambulia military bases mbili za jeshi la Merikani, hilo alikusaidia kitu ndio maana wanajeshi wengi ilibidi wakimbizwe Kuwait, Ujerumani na Merikani kupewa matibabu,kutokana na kupata madhara ya ubongo kutikiswa na shockwave ya mlipuko, binafsi huwa najiuliza: hivi kama Iran ingerusha roketi zilizo sheheni thermobaric payloads si wanajeshi wote wangekufa kutokana kukosa hewa na mapafu kuwa punctured, kwa bahati nzuri kutokana na UTU Iran hakufanya ukatiri wa kurusha roketi zenye madhara mkubwa kwa binadamu wenzake, badala yake Wairan walirusha roketi zilizo sheheni conventional high explosives tu na sio fuel air bombs/termobaric bombs

Tukirudi kuzungumzia uwezo wa Wachina ku-track movement za meli za Vita na submarine za USA in real time kwa kutumia satellite na sonars, wala hilo halishangazi hata kidogo maana siku hizi nyaja ya sayansi na teknolojia ime-grow sana na haihodhiwi na Taifa moja tu, hilo likumbukeni sana - ukweli ni kwamba linapo kuja suala la silaha - Uchina na Urusi zimekwisha ipiku USA kwenye silaha za kisasa kabisa, mfano: Hypersonic missiles and glide Vehicles, Submarine Drones, Supercavitation torpedoes za kuzamisha meli na submarine at high speed huku ikiwa imezama ndani ya Bahari.
 
Huu ndiyo ukweli wenyewe, siku zote vita ni uchumi!!!Sijui kutaka kujitenga au kujiunga NATO huwa ni geresha tu!!!

Vita zote zinalenga KUKUZA UCHUMI!!!!!
 
China ni massive na jeshi lake ni massive pia pia Marekani hawezi ku wage war maelfu ya km away halafu aishinde taiwan iliyoko 170 tu .
Naona umesahau Korean War mwaka 1950. Wakati wa Vita vya Korea,Korea Kaskazini Chini ya Mkomunist Kim ILL Sung wakiungwa mkono na China na Usoviet(Russia) waliivamia Korea Kusini ambayo ilikataa kufuata Mifumo ya Kikomunist badala Yake ikafuata Mifumo ya Kibepari. Matokeo ya Vita Ni Vifo vya Wanajeshi 450,000 wa China,400 wa Usoviet ,4,500 wa Marekani,320,000 wa Korea Kusini na 730,000 wa Korea Kaskazini.

Licha ya Korea Kusini kuwa Mlangoni mwa China na Maelfu ya Kilometer Kutoka Marekani lakini China alishindwa kuikalia Korea Kusini mpaka Sasa. Marekani ikiamua kwenda Vitani China haiwezi kufua dafu. Shida Ni Wanasiasa wa Marekani kuliingilia Jeshi la Marekani ili kujitafutia Kura. Mfano Ni Biden kuamua kuondoa Jeshi la Marekani Chini Afghanistan na Taliban kuchukua Madaraka,Kila mtu anasema Eti Taliban waliifurusha Marekani Kitu ambacho sio sahihi kabisa.
 
China ya 1950 sio ya sasa 2022 china ya korean war ilikuwa sawa tu na nigeria ya leo na wakati USA alikuwa ni super power na ana nyuklia !
 
China hakupigana Korean war kwa misingi ya kuikalia Korea ya Kusini bali alipigana kumsaidia ndugu yake mjamaa Korea ya kaskazini dhidi ya marekani.
 
Usa hii hii iliyojaa mashoga kibao kwenye jeshi lake aingie na uchina kwenye vita halafu ashinde!!!???? , maviiiiiii ya kuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…