China kazi anayo dhidi ya Mmarekani, Biden aweka vikwazo maradufu

China kazi anayo dhidi ya Mmarekani, Biden aweka vikwazo maradufu

Ushindani umekuwa mkubwa na marekani ni kama ushindani unamuelemea hivi ukifuatiza toka matokeo ya trade war wakati wa trump masuala ya Huawei na matokeo yake sasa.

Masuala ya Chips na inavyo backfire wao wenyewe U.S na washirika wake Netherlands, Japan na SK nafikiri U.S anapaswa kuja na mbinu mpya za kumkabili mchina.
Fair ground hamuwezi,wazungu wote hawamiwezi mchina,na walimuhofia kale
 
Hawawezi wakishusha hawatapata faida

China ina advantages nyingi sana inapohusu manufacturing kuanzia upatikanaji wa materials, R&D centres, skilled personel, supply chain n.k

Mfano magari ya Tesla 95% ya components zimetengenezwa China. Well Marekani amepiga ban China-based EVs, ila EVs za Tesla kutoka China zinaingia Marekani zikiwa zimetengenezwa kwa vifaa 95% kutoka China sio mbaya kwa uchumi wa China

Ilikuwa Tesla wafungue kiwanda India ila Elon Musk baada ya kupima kaona bora aongeze cha pili China. Kashapewa eneo lingine Shanghai aanze ujenzi mara moja
Aiseeh! Hatari
 
Huyo babu anasemaje? Eti Marekani ije kuongoza kwenye hizo sekta. Anaota ndoto za mchana

Kwa gap hili ni lini Marekani atampiga gap China? kama ameongea kisiasa sawa

●Steel:
China 54% global market share, vs US 4.3%

●Aluminum:
China 55%
share, vs US 1.5%

●EVs:
China 60%
share, vs US 8%

●Solar panels:
China 78%
share, vs US 2%
 
Miaka yote niliamini USA ni champion wa free markert economy na ni leader wa Free world kwa sasa naanza kupata mashaka.

Ni kama vile USA inakuwa Socialist/neo-communist na China ni purely capitalist.
Nakwambia hivi wazungu wanakuchapa ukijibu unaitwa gaidi
Sasa miaka yote wanahubiri free market, waliishimikiza sana China ifungue nchi wakapate cheap labour na material, sasa kiazi cha moto kimenasa kwenye koo.
 
Huku Tanganyika , viongozi wanapambana kuhakikisha hakuna kiongozi anayepewa sifa nyingi kuzidi Samia Hassan.

Sijui kwanini hili bara lina majitu ya hovyo hovyo duniani with zero focus.
Hv umesoma kilichoandikwa au umekimbilia tu ku comments hili jukwaa sasa hv naona mpk wenye matatizo ya akili wanajiunga
 
Tuchukulie mfano kwenye EVs unaonaje uhai wa makampuni yao ya magari katika soko la ushindani na makampuni ya China. Je, EU wataacha hivi hivi lipite ?
Sijajua watachukua hatua ipi ila sidhani kama watachukua au wana mpango wa kuchukua hatua kandamivu kama za US,maana mwaka huu viongozi wa Ulaya wamemiminika sana Beijing kwaajili ya ushirikiano wa kidiplomasia na kibiashara.
 
Umeangalia market size tu ,jaribu kuangalia power na influence yake worldwide.
Eti Africa!!! Biashara kubwa za dunia hazioni Africa kama targeted market kwao.
China akipewa option achague Kati ya Brazil na Africa atachagua Brazil.
China ni taifa lenye influence kibiashara na kidiplomasia.
USA alishaachwa mbali sana.
Pia China ina purchasing power kubwa.
Pia Afrika ni miongoni mwa masoko makubwa na muhimu duniani maana unao uwezo wa kupata wateja aina zote.
Hukukaa ufuatilie mkuu,China is giant in every aspect surpassing USA.
 
Market size ya marekani ni ndogo sana 300m population, 1 8bn pple china 2bn pple Africa 1bn pple, kwahiyo hilo ni dogo sanaa aliwezi ku affect uchumi wake.
GDP-PPP per capita ya wamerekani ni kubwa mara 100 ya wachina na mara 1000 ya waafrika. Kwa hiyo mchina kukosa soka la US ni pigo kubwa kwa uchumi wa china.
 
Haya ni matokeo ya USA ku invest kwenye vita kwa muda mrefu.

Wakati USA yeye yupo kwenye forever wars (na ku invest kwenye bidhaa za silaha), China wao walikuwa Wana invest kwenye viwanda/uzalishaji wa bidhaa za viwanda.

Haya ndio matokeo Sasa.
 
Market size ya marekani ni ndogo sana 300m population, 1 8bn pple china 2bn pple Africa 1bn pple, kwahiyo hilo ni dogo sanaa aliwezi ku affect uchumi wake.
Si sahihi. Ulaya na Marekani kuna watu wachache lakini wenye nguvu kubwa kiuchumi. Unaweza ukawa na watu wengi lakini nguvu yao ya manunuzi ni ndogo mfano India na Afrika.
 
Si sahihi. Ulaya na Marekani kuna watu wachache lakini wenye nguvu kubwa kiuchumi. Unaweza ukawa na watu wengi lakini nguvu yao ya manunuzi ni ndogo mfano India na Afrika.
Mnasahau jambo moja kwamba hata Marekani hutegemea soko la LDCs kwa bidhaa zake, umasikini wa Africa haumanishe kwamba hamna good quality income earners hata kupita baadhi ya watu katika nchi za Ulaya na Marekani out of 1 2bn African kuna population ya zaidi ya watu 300m ambao wana high annual disposable income ambao ni market target ya bidhaa kutoka marekani au China, kwahiyo kusema kwamba Africa wote masikini hapana
 
Hayo mambo ya vikwazo tayari yameshaonesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa dunia ya sasa hususani kwa mataifa kama Russia na China yenyewe.
China ni tofauti sana na Russia,
China ni global economy wakati Russia ni regional economy.
Na kuna tofauti pia ya sanctions na tarrifs, msikaririr mambo kama Kasuku.
 
Pale bingwa wa ubepari anapoomba pooh kupitia vikwazo.

Miaka yote niliamini USA ni champion wa free markert economy na ni leader wa Free world kwa sasa naanza kupata mashaka.

Ni kama vile USA inakuwa Socialist/neo-communist na China ni purely capitalist.
Kuna tofauti ya soko huria na soko holela.
Free market economy ni ndani ya nchi ila unapotoka kushindana na wengine lazima ulinde maslahi ya nchi yako kwanza ndio maana miaka yote Marekani inatoa ruzuku za mabilioni kwa wakulima wake na kuwafanya kuwa na ushindani zaidi kuliko wakulima wengine duniani.
 
Back
Top Bottom