China kuendesha TAZARA kwa miaka 27, Uwekezaji wa dola bilioni 1.4 kuanza

Miaka hiyo tupo Uchindile huko ndani ndani,unakwea zako Tazara,mwendo wa Ngiri,chuma inatembea mbayaaaa....

Kaja Mtu mweusi,ng'oa ng'o vitu....mamaeee,ndio black people life....

Kila kitu ukiwaza roho inaumaa
Na ukikumbuka tuliachiwa na hadi kiwanda Cha kukata Almasi - TANCUT Iringa, unachoka kabisa. Baadhi ya majengo yake ndio hiyo Mahakama Kuu Iringa.
 
Mimi nilidhani tungezungumza na Zambia kubadilli mfumo wa uendeshaji ili tuwe na sauti upande wetu,pia Reli hiyo ingewekwa chini ya TRC kwa Tanzania.Kuwapa wachina sio suluhisho pekee ni kufeli kunakoendelea.
 
Kiwango cha kujali vitu na uwajibikaji kwetu sisi kipo chini sana.
 
Hatukatai uwekezaji,tatizo letu ni usimamizi mbovu wa rasilimali zetu,itafika mahali watakuwa wanachukua pesa na hata ukarabati haufanywi mwisho wa siku tunaachiwa vyuma chakavu...
 
Mimi nilidhani tungezungumza na Zambia kubadilli mfumo wa uendeshaji ili tuwe na sauti upande wetu,pia Reli hiyo ingewekwa chini ya TRC kwa Tanzania.Kuwapa wachina sio suluhisho pekee ni kufeli kunakoendelea.
Sisi kazi yetu kuua mashirika. Kuwapa Wachina ndiyo suluhisho, sisi wazawa HATUWEZI.
 
Bora tu wangeitisha wawekezaji wa ndani kuliko hao wachina
Nitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?

Kuendesha TAZARA siyo sawa na kuendesha mabasi ya Kimbinyiko. Acheni mizaha
 
Hakuna watu watalia kama wafanyabiashara wa malori.kila siku wanaambiwa hii fursa wao wanakomaa na malori ya kutoka kwao..kifupi paka kapewa kulinda samakai.
 
Wangekuwa wanaitumia isingefika huko
 
Tazara na yenyewe itakua inafanya nini? Si bora ifungwe tu badala yakuendelea kutia hasara serikali zetu. Tena kama vigogo walafi wa zambia na tanzania hawataweza kuwapa wachima ushirikiano bora tu hiyo teli ifungwe maana kuiuza itakua usaliti mkubwa kwa nyerere na kaunda. Reli inahujumiwa kufanya biashara na malori ya vigogo. Wanahakikisha mizogo wa kubebwa na reli yanabeba malori yao. Uchumi unahujumiwa na gharama kubwa ambazo zingepungua kwa kutumika reli. Pia barabara zinakutikana na maisha mafupi bure kwa kubeba mizigo mizito kama madini ya vyuma na shaba ambayo yangestahili kubebwa ikibidi hata kwa sheria na reli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…