China kupeleka chombo Mars na kuanzisha space station inawauma sana Marekani na washirika wake



Waamerika wataunda kirusi kingine cha mafua na safari hii watakitupa Beijing sio Wuhan.
 
Mkuu unajua chombo cha kwanza cha US kilitua mwaka gani Mars?
Kumbuka pia mwaka huu chombo cha Wamarekani kingine kiko Mars ikiwemo mink helcopter.
Elon Musk yeye anachotaka kufanya ni kufanya usafiri wa anga za mbali uwe kama utalii na affordable.

Ila hata mimi ninakubaliana na wewe kuwa Wachina ni noma. US na wivu wake akishirikiana na nchi za ulaya walimshinda kauli mrusi eti mchina asishiriki nao kwenye matumizi ya space station. Mchina now one man show anatengeneza yake, na bado chombo chake alichotuma mwezini kimefika sehemu ya mbali zaidi ambayo haikuwahi kuchunguzwa kabla.
 
Kataa ukubali, haijalishi nini America imefanya lakini nchi iliyokuwa almost na uchumi unalingana na Tanganyika leo kuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani ni jambo ambalo linastahili pongezi.

Pia wawe wnaiba technology au hawaibi nako kuiba kunahitaji maarifa, sisi hata tupewe formula bado tutafail.
 
Mleta mada anavyowapamba wachina kana kwamba wamekuja kutuokoa kutoka kwa mmarekani wakati ni washenzi tu.

mkuu hatukuwahi kuwakaribia china kiuchumi. Huo ni uongo ambao umerudiwa sana sasa unaonekana kama ukweli.
 
Ok
 
Asante kwa darasa ulilotupa.
 
Mkuu wewe umeniathiri sana!
Nilianza kukufuatilia 2010 au na 11 natumia simu ya mzazi. Nipo kidato cha 4. Safari inaendelea mpaka nafika Chuo nakufuatilia tu ikafika mahala Nikaanza kumfuatilia Prof. Stephen Cohen (ambaye ni marehemu kwa sasa). Nikaanza kufuatilia haya mambo kwa kadri nilivyoweza.

Athari niliyopata mambo mengi ya ujana yamenipita. Sijui mambo mengi sana ya ujana mpaka wezangu wananishangaa! Nikichangia WhatsApp wenzangu wananishangaa nashindwa kifupisha maneno. Kingine kufuatilia hizi mada zimenifanya nafikiri na nazungumza kiutuuzima kuliko umri wangu. Sikuligundua ila nimemabiwa!

Kingine kwa kile nilichokijua kwa kujifunza kupitia kwako na kwa wa mfano wako naona kama nimejitwisha mzigo mzito sana! Mfano kama ulichochangia kwenye Uzi wa Chige huwa najiuliza unawezaje kuhimili mambo makubwa mnoo kwenye moyo!Samahani kwa kutoka nje ya mada!

Kwa sasa nahangaika kurudisha ujana wangu.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU!
 
Halafu watu bado wanamkataa mchina
 
Hahaha Ustaadh umezingua sana, hizi ni mbwembwe tu jamaa yangu!
Unafikiri!

Vuta picha niliacha kusikiliza mziki, radio na vipindi vingi vya local channels tangu nina miaka 19. Nikawa nasoma mambo yenu na kujishughulisha nayo mpaka nafika miaka 26. Ikipita siku bila kusoma sipati raha kabisa! Umri huo nasoma gazeti kwa sana nafuatilia taarifa za habari plus makala tofauti tofauti. Namkubali sana Nikola Tesla nikawa namsoma na kusikiliza documentary zake. Nikahamia kwa wazee wa dunia flat huko nikakesha mpaka basi!

Sasa nina miaka 28 kila vijana wenzangu wanachozungumza sikielewi!

Waliniambia unasikikiza singeli? Masikini ya Mungu hata maana yake sikuwa najua! Wakasema ngoja tukutoe ushamba wakanipeleka viwanja, loooh! Kumenishinda! Ni hatari mnoo! Kwangu kasi waliyonipeleka niliiona ni kubwa mnoo!

Nimemeamua kurudi tu kuanza kutafuta vitabu vya wanafalsafa wa west na wa east. Pembeni namsikilza Mex Cortez.
 
aache kujisaidia mwenyewe aisaidie dunia ili iweje

us atoe mambo yake ili UCHINA ianguke na kila mmoja ajisaidie mwenyewe

mbna UCHINA inawatesa[emoji38][emoji38]
 
Wewe umejijuaje kwamba unayozungumza ni makunwa zaid ya umri wako
 
sasa nini amekifanya Marekani hadi ukajua kuwa roho inamuuma?
 
tunamshukuru kaleta tecno
Simu hizi za kujiwasha tochi ukiweka mfukoni? Hizi hizi ambazo hazina update? Km unatumia Lolipop ni hiyo hiyo hakuna update? Watu wapo android version 11 nawe upo 5.
Acha kumshirikisha Mungu kwenye vitu vya kijinga.
 
sasa nini amekifanya Marekani hadi ukajua kuwa roho inamuuma?
Sijaona hata makala inayoongelea kuwa wamerakani wamekereka.
Hao ni askari wa Jihad, wala usishangae maana muda wote wamejaa sumu kama wale wa Msumbiji.
Huko kwenye nyumba zao wameambiwa Marekani ni mbaya wao. Kwahiyo wanapoteza machungu
 
Sioni lolote la kipekee kwenye hili.. Watu wanapeleka orbiters na landers Mars kwa miongo kadhaa sasa..

Voyager 1&2 zipo nje ya solar system.. Kupeleka orbiter/lander kwa sayari iliyopo karibu zaidi na dunia haiwezi kuwa agenda kuu..

Kuhusu station yao; kwa namna ilivyo expensive ku-run ISS, nahisi hiyo itakuwa satellite ya kawaida tu kama zilivyo zingine.

Ngoja tuisome hiyo habari kwa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…