China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

ChawaVariable chama chenu cha CCM si ndio mnasema CCP ndio mlezi wenu kisiasa hadi chuo amewajengea huwa wanatoa mafunzo ya udikteta vipi tena kwanini hutaki kufuata kila CCP wanachofanya maana ndio benchmark ya CCM.
... za kuambiwa changanya na zako! ........................................................... MKWERE
 
Dini zilikuwepo kitambo mno, na wajinga dini pia walikuwepo

Ulaya, American na mataifa mengine wanazo dini, wameziishi na wanaziishi, na bado wanazo akili

Na taifa lenye watu wenye IQ kubwa siyo China, ni mataifa ambayo wanaamini uwepo wa Mungu
 
Pia na CCM wafuate uzazi wa mipango , watoto 2 TU, wanatosha , kila mwaka serikali kujenga vituo vya ( Afya uzazi) , madarasa, madawati , Nchii hii itashindwa kuendelea , jamani ,


Walipa Kodi ni wachache mara 7 ya wasio kuwa na shughuli zinazo zalisha kipato na kukusanya Kodi
 
Kijana , hoja yako ina mambo ya kufikirisha kuhusu umuhimu wa elimu, sayansi na uwezo wa kufikiri kwa kina. Uislamu haupingi mambo hayo; kwa kweli Qur'an mara nyingi inawaalika watu kutumia akili zao, kutafakari na kuchunguza ulimwengu. Aya ya kwanza iliyoteremshwa ilikuwa "Soma", jambo linaloonyesha thamani ya elimu.

Hata hivyo, kusema kwamba dini huwafanya watu wote kuwa wajinga si sahihi kihistoria wala kimantiki. Wanasayansi wengi walioweka misingi ya hisabati, tiba, astronomia na kemia katika ustaarabu wa Kiislamu walikuwa waumini. Mfano ni Ibn Sina, Al-Khwarizmi na Ibn al-Haytham. Hawakuona imani na akili kuwa maadui bali washirika.

Pia, hoja kwamba watoto wasifundishwe dini hadi wawe watu wazima ina changamoto yake. Watoto hufundishwa maadili, tamaduni, lugha na mitazamo mbalimbali tangu utotoni. Ikiwa kufundisha dini ni "indoctrination", basi kufundisha falsafa ya kutokuamini Mungu au mtazamo wa serikali pia kunaweza kuitwa hivyo. Swali si kama watoto wafundishwe maadili au la, bali ni maadili gani wafundishwe na kwa namna gani.

Kuhusu China, maendeleo ya sayansi na teknolojia hayatokani na kuzuia dini pekee. Kuna nchi nyingi zilizoendelea ambazo zina uhuru mkubwa wa dini, na pia kuna nchi zisizo na maendeleo licha ya kudhibiti dini. Sababu za maendeleo ni nyingi: elimu bora, utawala mzuri, sheria, uwekezaji katika sayansi na uwajibikaji.

Uislamu haufundishi mtu akae akisubiri miujiza bila kufanya kazi. Mtume Muhammad alisema kwamba mtu amfunge ngamia wake kwanza kisha amtegemee Mungu. Hii inaonyesha kuchukua sababu na hatua za vitendo kabla ya kutegemea msaada wa Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo, tatizo si dini yenyewe bali namna watu wanavyoitumia. Dini inaweza kutumiwa vibaya kama vile siasa, elimu au teknolojia zinavyoweza kutumiwa vibaya. Suluhisho si kupiga marufuku dini, bali kujenga jamii yenye elimu, fikra huru, maadili na heshima kwa uhuru wa watu kuamini au kutokuamini.
... Tatizo sio dini ila ni jamii zenye dini mseto ambazo kila moja inataka imiliki serikali kwa maslahi yake! ... hii inazaa uhasama na upinzani kwenye mpaka mikakati yenye tija ilimradi tu imependekezwa na mtu wa imani kinzani!
HII HUTUFANYA TULIO WENGI KUONA DINI NI KIKWAZO!
 
Haiwezekani. Wananchi ni watu wa imani. Watapoteza mamlaka. Ili iwezekane inabidi wananchi kwa idadi ya kutosha wawe wapagani kwanza.
Inawezekana na wala hatapoteza mamlaka, nchi kama Tanzania ni rahisi zaidi katika mazingira sasa, anachotakiwa ni ku play smart tu long game, unaanza kidogokidogo kuondoa ushwawishi wa dini kwenye mambo ya kitaifa mfano kutohudhuria makongamano ya dini yoyote.

Kutoalika viongozi wa dini kwenye ishu za kitaifa, kuondoa misamaha ya kodi kwa biashara za dini n.k Halafu pembeni hakikisha una attack dogs wako aina ya Cyprian Musiba na pia play one religion dhidi ya nyingine from time to time.

Sema sasa kwanza kupata tu huyo kiongozi asiyehusudu dini kwa nchi hii ni sawa na kuokota pesa Kariakoo.
 
Jana huko IG nimemuona Mzungu Koko mmoja na yeye anasema mwanae akifikisha miaka 18 atakuwa tayari kashajua dini ni uongo na utapeli.Namnukuu mwanangu atakuwa kashajua nyoka hawezi kuongea na Wala mwanamke hatoki kwenye ubavu wa mwanaume .Hivyo hizo zote anadai ni porojo tu mwisho wa kumnukuu.
 
... Tatizo sio dini ila ni jamii zenye dini mseto ambazo kila moja inataka imiliki serikali kwa maslahi yake! ... hii inazaa uhasama na upinzani kwenye mpaka mikakati yenye tija ilimradi tu imipendekezwa na mtu wa imani kinzani!
HII HUTUFANYA TULIO WENGI KUONA DINI NI KIKWAZO!

Ninakubaliana kwamba wakati mwingine migogoro ya kidini inaweza kuleta migawanyiko katika jamii. Lakini tatizo la msingi si dini yenyewe, bali tamaa ya madaraka, ubinafsi na kutovumiliana kwa baadhi ya watu. Hata katika nchi ambazo dini si sehemu kubwa ya maisha ya watu, bado kuna migogoro ya kikabila, kisiasa, kiitikadi na kiuchumi. Hii inaonyesha kuwa chanzo cha migogoro si dini pekee.

Kwa mtazamo wa Uislamu, tofauti za dini na makabila ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Qur'an inafundisha watu wafahamiane na washirikiane katika mema, si kupigana kwa sababu ya tofauti zao. Historia inaonyesha kwamba Muhammad aliishi na kushirikiana na Wayahudi, Wakristo na makundi mengine katika mji wa Madina chini ya mfumo uliotambua haki za kila kundi.

Pia, si sahihi kuhitimisha kwamba kwa sababu baadhi ya watu wanatumia dini kutafuta ushawishi wa kisiasa basi dini yenyewe ni kikwazo. Kwa mantiki hiyo hiyo, tungeweza kusema demokrasia ni mbaya kwa sababu baadhi ya wanasiasa huitumia vibaya, au sayansi ni mbaya kwa sababu imetumika kutengeneza silaha. Ukweli ni kwamba tatizo liko kwa watumiaji, si kwa msingi wa kitu chenyewe.

Dini inapofundishwa kwa usahihi, inapaswa kuwafanya watu wawe waadilifu, waaminifu, wenye huruma na wenye kuheshimu haki za wengine. Kinachozalisha uhasama si imani ya mtu kwa Mungu, bali pale watu wanapoweka maslahi yao binafsi juu ya haki na ukweli.

Kwa hiyo, suluhisho si kuondoa dini katika jamii, bali kujenga utamaduni wa haki, elimu, uvumilivu na kuheshimiana kati ya watu wa imani tofauti. Jamii inaweza kuwa na dini nyingi na bado ikaishi kwa amani ikiwa watu wataongozwa na uadilifu badala ya ubaguzi.
 
... Tatizo sio dini ila ni jamii zenye dini mseto ambazo kila moja inataka imiliki serikali kwa maslahi yake! ... hii inazaa uhasama na upinzani kwenye mpaka mikakati yenye tija ilimradi tu imipendekezwa na mtu wa imani kinzani!
HII HUTUFANYA TULIO WENGI KUONA DINI NI KIKWAZO!
Hili nalo ni tatizo pia pamoja viongozi kuteuliwa kwa kuangalia dini zao zaidi ili ku balance badala ya kutanguliza merits mbele.
 
Dini zinazchelewa maendeleo, mojawapo ya sababu kubwa ya China na Tiger economies kuendelea kwa haraka sana ndani ya miongo michache ni kupuuza dini na miongozo yake.

Kusema China na Tiger Economies zimeendelea kwa sababu zilipuuza dini ni kurahisisha jambo lenye sababu nyingi. Maendeleo yao yalitokana zaidi na elimu bora, nidhamu, uwekezaji katika sayansi, teknolojia, viwanda na utawala madhubuti.

Kama dini ndiyo chanzo cha umaskini, basi nchi zote zenye dini zingekuwa maskini na zote zisizo na dini zingekuwa tajiri, jambo ambalo si kweli.

Kwa mtazamo wa Uislamu, dini haipingani na maendeleo. Uislamu unahimiza elimu, kazi, biashara, utafiti na matumizi ya akili. Tatizo si dini, bali uvivu, ujinga, rushwa na uongozi mbovu.

Kwa hiyo, maendeleo huletwa na maarifa na utendaji mzuri, si kwa kuondoa dini.
 
Inawezekana na wala hatapoteza mamlaka, nchi kama Tanzania ni rahisi zaidi katika mazingira sasa, anachotakiwa ni ku play smart tu long game, unaanza kidogokidogo kuondoa ushwawishi wa dini kwenye mambo ya kitaifa mfano kutohudhuria makongamano ya dini yoyote, kutoalika viongozi wa dini kwenye ishu za kitaifa, kuondoa misamaha ya kodi kwa biashara za dini n.k Halafu pembeni hakikisha una attack dogs wako aina ya Cyprian Musiba na pia play one religion dhidi ya nyingine from time to time.

Sema sasa kwanza kupata tu huyo kiongozi asiyehusudu dini kwa nchi hii ni sawa na kuokota pesa Kariakoo.
Mkuu jiji kama Dar itawezekana kwa tabu mno, ila huko mikoani kusipo na exposure, si kazi rahisi.
 
Mkuu jiji kama Dar itawezekana kwa tabu mno, ila huko mikoani kusipo na exposure, si kazi rahisi.
Mkuu unaweza kufanya social engineering kubwa sana ukiwa na absolute power, angalia MBS anavyowaburuza na kuwapelekea moto Wahafidhina Saudi Arabia, anaruhusu kila kitu (sijui ndio wanasema kufungua nchi).

Hapa Tanzania kwa mamlaka aliyo nayo rais na uwepo dini mbili tofauti (unazoweza kuzifanya zisigane) hili wala sio jambo gumu sana na ukizingatia raia pia hata hawamuweki mtawala madarakani.
 
Haiwezekani. Wananchi ni watu wa imani. Watapoteza mamlaka. Ili iwezekane inabidi wananchi kwa idadi ya kutosha wawe wapagani kwanza.
Ni kuwapa Elimu ya ufahamu kwamba huko wanakodhani dini zilianzia hasa Kwa Wazungu walishaacha kwenda hata makanisani
 
Ni kuwapa Elimu ya ufahamu kwamba huko wanakodhani dini zilianzia hasa Kwa Wazungu walishaacha kwenda hata makanisani
Elimu haifanyi kazi sana kwa watu wa dini, dini ni jambo la hisia zaidi kuliko logic na critical thinking.

Halafu mbona Gwajima na kanisa lake lote walifungiwa tena kwa uonevu tu lakini hawakufanya chochote kikubwa. Hakuna chochote kikubwa kitatokea mfano serikali ikiondoa vipindi vya dini mashuleni au ikiacha kuwashirikisha na kuwapa kipaumbe kipekee viongozi wa kidini katika masuala ya kitaifa.
 
Dini ni sawa na Pombe, madawa au bangi au Porno, zote hizo kwa Under age zinaharibu malengo kama vile tu Mimba au Ndoa kwa watoto wa Shule.

Dini aianze mtu akiwa tayar anacarrier na Uchumi wake binafs ili atumie akili zake kuchagua sio influence ya wazazi. Ili aone ilivo ngum kutoa 20% ya mshahara kila mwezi kumpea mchungaji kwa kile wanachoita Zaka na Sadaka.
 
Back
Top Bottom