China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

Waliotuletea maendeleo walianza kuendelea katika "age of enlightenment", fuatilia hiko kilikuwa ni kipindi cha aina gani.
Vipi kwa nchi zilizopata maendeleo hivi karibuni eg Singapore, Malaysia, UAE au waafrika wenzetu kama Botswana na Algeria? Kwanini na sisi tusiendelee kama wao?
 
Mkuu,kwani sasahivi watoto hawafundishwi vitu vya maana na vyenye tija huko shuleni? Au wakienda shule ni dini asubuhi hadi jioni?Kwanza shule za serikali vipindi vya dini hata havitiliwi mkazo na bado zinaongoza kwa matokeo mabovu. Shule za dini ambazo kuna hadi makanisa shuleni ndo shule zenye ufaulu. Mtoto kusoma au kutokusoma dini hakumfanyi afaul,tutafute kichaka kingine.
Siongelei matokeo mabovu tu, hata hao wanafunzi wanaofaulu hizo shule za dini kwa ufaulu mkubwa wengi wao wala hawana mchango mkubwa kwa taifa, Kuna waseminari wengi ni wezi na mafisadi tu.
 
Siongelei matokeo mabovu tu, hata hao wanafunzi wanaofaulu hizo shule za dini kwa ufaulu mkubwa wengi wao wala hawana mchango mkubwa kwa taifa, Kuna waseminari wengi ni wezi na mafisadi tu.
Huo mchango kwa taifa hauji kwa sababu ya dini au kwa sababu ya mifumo ya nchi? Mtaala wa elimu mbovu unaopima ufaulu kwa nadharia na si vitendo unatungwa na nani? Mifumo mibovu ya makazini inayolea wezi imewekwa na nani? Na huo wizi na ufisadi wanafundishwa wakiwa seminari?

Kwa marejeo yangu,imani zote za hapa Tz zinakataza wizi na ufisadi kwa hiyo huyo mseminari anaeiba na kufanya ufisadi ameenda kinyume na maadili yake ya kiseminari aliyopewa. Hakuna dini hapa Tz inayofundisha ukaibe,kwanza dini zinakataza.

Na kuhusu mchango wa hao wanafunzi wanaofaulu ni sisi mifumo yetu inaua vipaji vya watu hasa huko makazini. Watanzania tunataka watu wanaofanya kazi ili mradi walipwe na sio wabunifu.Ukiwa mbunifu kazini na unafanya extra hata bosi wako anakuchukia.

Sasa ni dini ndo zinatuambia tuwe na mifumo mibovu kazini au ni utamaduni wetu wa kijinga tuliogoma kuuachia? Ni dini ndo zinatuambia tuue vipaji vya watoto wetu toka wakiwa wadogo au ni sisi wenyewe? Ni dini ndo zinawaambia viongozi wateue watu kwa kujuana badala ya kuangalia ufanisi wa kazi?
 
Nyerere na Karume walikuwa wanadini haswa, hawakuwa Wajamaa au Wakomunisti halisi.
Walikuwa hawana dini , wakijifnya tu wana dini , wasingaliwachukuwa wakomunisti kwenye serikali na vile vile hawakuishi kidini
 
Ingekuwa dini ni chanzo cha umaskini basi Qatar na Saudia walipaswa kuwa maskini wa kutupwa. Kama dini ingekuwa inaua uwezo wa kufikiri basi Iran wasingekuwa na uwezo wa kutengeneza yale makombora,kama dini inakufanya kuwa mjinga basi mgunduzi wa Fallopian tubes asingekuwa Padri wa Kanisa Katoliki.
Kasome historia walikuletea dini kama mbinu ya kukutawala kiuchumi na Kijamii.

Dini ni vitangulizi vya ukoloni mkongwe na ukoloni mamboleo.
 
Vipi kwa nchi zilizopata maendeleo hivi karibuni eg Singapore, Malaysia, UAE au waafrika wenzetu kama Botswana na Algeria? Kwanini na sisi tusiendelee kama wao?
Ukichunguza wame priotise rational and critical thinking badala ya emotions za dini.

Huwezi pata maendeleo Kwa kuendekeza dini.
 
Kabla hatujaletewa hizo dini mbona tulikuwa hatuna maendeleo kuwazidi wao mkuu?
Ulidanganywa na nani kwamba tulikuwa hatuna maendeleo?

Kwani wewe hujui kwamba Wazungu wameiba treasures zote za Africa na wamefuta historia yetu Ili ionekane hivyo ulivyolishwa matangopori?

Wakati wanakuja walitukuta na Kila kitu tunafanya
 
Ukichunguza wame priotise rational and critical thinking badala ya emotions za dini.

Huwezi pata maendeleo Kwa kuendekeza dini.
Kabla ya kuletewa dini sisi tulikuwa tumeprioritize rational and critical thinking?

Si ni jamii zetu ambazo hadi watoto mapacha walikuwa wanauwawa kwamba ni mikosi?

Si ni jamii zetu ambazo watoto ambao weno yanaanza kuota ya chini walikuwa hadi wanauwawa?

Ukoma ulikuwa unaaminika ni ugonjwa wa kurithiwa na wanawake waliokuwa hawazai walikuwa wanatimuliwa kwenye ndoa zao kwamba hawana faida.

Ilitakiwa waliotuletea dini wasitukute na hizo imani maana kabla ya dini rational na critical thinking tulikuwa nayo
 
Kabla ya kuletewa dini sisi tulikuwa tumeprioritize rational and critical thinking? Si ni jamii zetu ambazo hadi watoto mapacha walikuwa wanauwawa kwamba ni mikosi? Si ni jamii zetu ambazo watoto ambao weno yanaanza kuota ya chini walikuwa hadi wanauwawa? Ukoma ulikuwa unaaminika ni ugonjwa wa kurithiwa na wanawake waliokuwa hawazai walikuwa wanatimuliwa kwenye ndoa zao kwamba hawana faida? Ilitakiwa waliotuletea dini wasitukute na hizo imani maana kabla ya dini rational na critical thinking tulikuwa nayo
Bila shaka ndicho tuliweka mbele,hatukuwa na kuzuia ya kuombewa sijui mapepo and such nonsense.

Ndio maana kwenye jamii zetu kulikuwa hakuna walemabu Wala albino maana ni shortcomings ambazo hazikukubalika kwenye jamii zetu ziliondolewa Kwa akili kubwa.
 
Elimu haifanyi kazi sana kwa watu wa dini, dini ni jambo la hisia zaidi kuliko logic na critical thinking.

Halafu mbona Gwajima na kanisa lake lote walifungiwa tena kwa uonevu tu lakini hawakufanya chochote kikubwa. Hakuna chochote kikubwa kitatokea mfano serikali ikiondoa vipindi vya dini mashuleni au ikiacha kuwashirikisha na kuwapa kipaumbe kipekee viongozi wa kidini katika masuala ya kitaifa.
Huwezi pata maendeleo Kwa kutumia emotions
 
Ulidanganywa na nani kwamba tulikuwa hatuna maendeleo?

Kwani wewe hujui kwamba Wazungu wameiba treasures zote za Africa na wamefuta historia yetu Ili ionekane hivyo ulivyolishwa matangopori?

Wakati wanakuja walitukuta na Kila kitu tunafanya
Mkuu, mfano hapa Tanzania tulikuwa na maendeleo gani kabla mzungu hajaja? Na kuhusu treasures kuibiwa mbona nyingine bado hazijaibwa? Ziwa Tanganyika limeibiwa? Ardhi yenye rutuba imeibiwa? Bahari ya Hindi imeibiwa? Mbona hizo ni treasures ambazo tunazo ni sisi wenyewe tumeshindwa kuzitumia. Mfano maji hadi leo ni shida,mzungu katuibia maji yote kaenda nayo Ulaya?
 
Bila shaka ndicho tuliweka mbele,hatukuwa na kuzuia ya kuombewa sijui mapepo and such nonsense.

Ndio maana kwenye jamii zetu kulikuwa hakuna walemabu Wala albino maana ni shortcomings ambazo hazikukubalika kwenye jamii zetu ziliondolewa Kwa akili kubwa.
Kuua maalbino na walemavu ni critical thinking kuliko kutengeneza vifaa vya kuwasaidia walemavu kuishi maisha kama wengine? Maana walemavu walikuwa wanauliwa . Hiyo ni sawa kwa watu wenye " critical thinking"?
 
Mkuu, mfano hapa Tanzania tulikuwa na maendeleo gani kabla mzungu hajaja? Na kuhusu treasures kuibiwa mbona nyingine bado hazijaibwa? Ziwa Tanganyika limeibiwa? Ardhi yenye rutuba imeibiwa? Bahari ya Hindi imeibiwa? Mbona hizo ni treasures ambazo tunazo ni sisi wenyewe tumeshindwa kuzitumia. Mfano maji hadi leo ni shida,mzungu katuibia maji yote kaenda nayo Ulaya?
Kabla ya mzungu hakukuwa na kitu inaitwa Tzn labda uulize kulikuwa na maendeleo gani kwenye himaya zetu za kikoo.Wewe ni mgeni n watemi wetu? Kina Isike,Mangi,Mkwawa nk? Tulikuwa na mipaka yetu na maendeleo yetu Wazungu wakaweka ya kwao na kuvuruga vya kwetu
 
Mkuu, taja eneo lolote ambalo kwa sasa ni Tanzania chagua lolote ambalo lilikuwa na maendeleo kuzidi Ulaya kabla wazungu hawajaja.
 
Kuua maalbino na walemavu ni critical thinking kuliko kutengeneza vifaa vya kuwasaidia walemavu kuishi maisha kama wengine? Maana walemavu walikuwa wanauliwa Hiyo ni sawa kwa watu wenye " critical thinking"?
Hatuhitaji kutumia Rasilimali kuhudumia walemabu wasio na Msaada kwenye jamii zetu ndio maana tulikuwa tunamalizana nao tukiwa wadogo kabisa.

Tulikuwa na maarifa na mbinu zetu za maana sana mfano ukiambiwa mmja mzigo usile mayai sana utazaa mtoto mwenye kipara tulikuwa tunamaanisha hatuko tayari kupoteza wanawake kwenye uzazi ila nyie wenye akili za kizungu Sasa mnauza dawa ,mnapasua watu hamna utu.
 
Mkuu, taja eneo lolote ambalo kwa sasa ni Tanzania chagua lolote ambalo lilikuwa na maendeleo kuzidi Ulaya kabla wazungu hawajaja.
Kwani standard ya maendeleo ni Ulaya? Mathalani Ulaya Wana michezo Yao ya mpira wa miguu ,Mimi nisipokuwa nao na sijajenga viwanja nitakuwa Sina maendeleo?
 
Hatuhitaji kutumia Rasilimali kuhudumia walemabu wasio na Msaada kwenye jamii zetu ndio maana tulikuwa tunamalizana nao tukiwa wadogo kabisa.

Tulikuwa na maarifa na mbinu zetu za maana sana mfano ukiambiwa mmja mzigo usile mayai sana utazaa mtoto mwenye kipara tulikuwa tunamaanisha hatuko tayari kupoteza wanawake kwenye uzazi ila nyie wenye akili za kizungu Sasa mnauza dawa ,mnapasua watu hamna utu.
Mkuu,kumuita mlemavu" mtu asiye na msaada kwenye jamii" ni critical thinking? . Hapo chini umesema" watu hamna utu", kuua walemavu sio " kukosa utu"?
 
Mkuu,kumuita mlemavu" mtu asiye na msaada kwenye jamii" ni critical thinking? . Hapo chini umesema" watu hamna utu", kuua walemavu sio " kukosa utu"?
Ndio ,kiafrica hatuhitaji walemavu kwenye jamii zetu sio mila Wala desturi zetu.

Ulemavu ambao ulikuwa tolerated kwetu ni wa baada ya kuwa mtu mzima na sio kabla.

Hili ni suala la Mila sio maendeleo
 
Kwani standard ya maendeleo ni Ulaya? Mathalani Ulaya Wana michezo Yao ya mpira wa miguu ,Mimi nisipokuwa nao na sijajenga viwanja nitakuwa Sina maendeleo?
Standard ya maendeleo sio Ulaya, ila kama tulikuwa tumeendelea ilitakiwa tuwe na teknolojia ambayo ingetuwezesha kuwashinda pale walipotaka kututawala kwa nguvu. Unasemaje umeendelea ilihali mtu anatoka huko anakuja kukufunga minyororo anakuweka kwenye meli ukawe mtumwa nchini mwake? Ilitakiwa tuwe na uwezo wa kupambana nao hadi tuwashinde.
 
Back
Top Bottom