China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

China: Marufuku kwa walio chini ya Miaka 18 kushiriki Mambo ya Dini

Unaiongelea China badala ya CCM iliyo wafanya wananchi wabakie masikini wa kutupwa ndani ya nchi yao, kuwageuza wajinga kuwa machawa na misukule ya watawala!
 
Dini zilikuwepo kitambo mno, na wajinga dini pia walikuwepo

Ulaya, American na mataifa mengine wanazo dini, wameziishi na wanaziishi, na bado wanazo akili

Na taifa lenye watu wenye IQ kubwa siyo China, ni mataifa ambayo wanaamini uwepo wa Mungu
Tunazungumzia maendeleo kwa kuvuna nguvu kazi watu sio IQ za Ulaya na American wanaowanyonya wengine ili kujenga uchumi.
 
Dini zilikuwepo kitambo mno, na wajinga dini pia walikuwepo

Ulaya, American na mataifa mengine wanazo dini, wameziishi na wanaziishi, na bado wanazo akili

Na taifa lenye watu wenye IQ kubwa siyo China, ni mataifa ambayo wanaamini uwepo wa Mungu
Ulaya na Marekani walipiga hatua kubwa za maendeleo kwa harka baada ya kuziweka dini siti ya nyuma badala ya kwenye usukani na kuchora mstari mkubwa kati ya dini na state (Age of enlightenment Karne ya 17 na 18). Hapo ndipo haya mambo yote mazuri unayoayoana Ulaya na Marekani yalipoibuka na kustawi.
 
Haya mambo ya dini yanatuharibu ubongo tuu mtu anachepuka mara ya kwanza unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe kisa tu umekariri SAMEHE 7 MARA 70 mwisho ukimwi unakuchukuliza
 
Mkuu unaweza kufanya social engineering kubwa sana ukiwa na absolute power, angalia MBS anavyowaburuza Wahafidhina Saudi Arabia, anaruhusu kila kitu (sijui ndio wanasema kufungua nchi). Hapa Tanzania kwa mamlaka aliyo nayo rais na uwepo dini mbili tofauti (unazoeweza kuzifanya zisigane) hili wala sio jambo gumu sana na ukizingatia raia pia hata hawamuweki mtawala madarakani.
Alishindwa Karume na Nyerere wake huku Zanzibar watakuja kuwezä hawa wanaosumbuliwa na njaa ?
 
Mkuu, kama dini ni chanzo cha umaskini mbona waliotuletea maendeleo sisi wenyewe ndo hao waliotuletea dini,ingekuwa dini ni kikwazo ilitakiwa wazungu kabla hawajaja huku kwetu sisi tuwe na maendeleo ya juu zaidi yao. Cha kushangaza hata hospital na shule tulijengewa na hao hao wamisionari.

Halafu China kwenye suala la dini iko tofauti na nchi nyingine. China walikuwa na imani zao na wanazo lakini hazikuwa zimekaa kwenye mfumo wa kitaasisi kama Islam au Christianity na hadi leo ndio imani zao zipo hivyo hivyo.

Ndio maana hata CCP wanaweza kuzuia ushawishi wa kidini kwa sababu dini za kichina hazijakaa kwenye mfumo wa kama kiislam au kiiristo. Lakini sio kila nchi duniani ni China ,huwezi kuiga kila kitu wanachofanya China ukaleta nchini mwako ilihali wewe hauna utamaduni au historia kama ya China.

Ingekuwa dini ni chanzo cha umaskini basi Qatar na Saudia walipaswa kuwa maskini wa kutupwa. Kama dini ingekuwa inaua uwezo wa kufikiri basi Iran wasingekuwa na uwezo wa kutengeneza yale makombora,kama dini inakufanya kuwa mjinga basi mgunduzi wa Fallopian tubes asingekuwa Padri wa Kanisa Katoliki.

Kama dini inashusha IQ basi Gregory Mendel mtawa aliyekuwa anatumia muda mwingi kusali asingekuwa amegundua masuala ya vinasaba yaliyofanya leo hii tunawaambia watu" kapime DNA".
 
Alishindwa Karume na Nyerere wake huku Zanzibar watakuja kuwezä hawa wanaosumbuliwa na njaa ?
Nyerere na Karume walikuwa wanadini haswa, hawakuwa Wajamaa au Wakomunisti halisi.
 
Kama dini inashusha IQ basi Gregory Mendel mtawa aliyekuwa anatumia muda mwingi kusali asingekuwa amegundua masuala ya vinasaba yaliyofanya leo hii tunawaambia watu" kapime DNA".
Waliotuletea maendeleo walianza kuendelea katika "age of enlightenment", fuatilia hiko kilikuwa ni kipindi cha aina gani.
 
Haya mambo ya dini yanatuharibu ubongo tuu mtu anachepuka mara ya kwanza unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe anachepuka tena unamsamehe kisa tu umekariri SAMEHE 7 MARA 70 mwisho ukimwi unakuchukuliza
Hao hawajaisoma biblia vizuri kwani Bwana Yesu alisema unapomtizama tu mwanamke kwa matamanio basi bora jicho lako ulitowe kuliko ukafa nalo ukalichukuwa nalo kwani adhabu ya huko mbele ya Mungu haisemeki. Jee uliwahi kusikia mkristo amelitoa jicho lake ?
 
Waanze kuondoa vipindi vya dini mashuleni, watoto wafundishwe vitu vya maana vyenje tija kwenye maisha yao.
Mkuu,kwani sasahivi watoto hawafundishwi vitu vya maana na vyenye tija huko shuleni? Au wakienda shule ni dini asubuhi hadi jioni?

Kwanza shule za serikali vipindi vya dini hata havitiliwi mkazo na bado zinaongoza kwa matokeo mabovu. Shule za dini ambazo kuna hadi makanisa shuleni ndo shule zenye ufaulu.

Mtoto kusoma au kutokusoma dini hakumfanyi afaul,tutafute kichaka kingine.
 
Back
Top Bottom