Naona watu wana comment kiushabiki na wanasahau uhalisia kwamba wa kwanza kuathirika ni sisi huku nchi zisizo "jielewa" hasa viongozi wetu.
Nikifikiria magonjwa yenye udhamini wa taifa la USA, TB, HIV na malaria sioni hawa ndugu zetu watapata wapi msaada wa madawa haya kwa urahisi na wakati sahihi.
Nikikumbuka mwaka jana nina ndugu namuuguza ana TB kuna kipindi dawa ziliadimika dozi ikawa haipatikani kwa ukamilifu hii ni baada ya mdhamini kumaliza muda wake wa kutoa huduma.
Kiukweli kama haujui changamoto za haya magonjwa ya muda mrefu na upatikanaji wa dawa ukojekwa nchi zetu hizi utajua ni nini kinafata kwa ndugu zetu.
Serikali pekee sidhani kama wataweza kikombe hiki ukizingatia janga la corona ndio kwanza linaanza kuchanganya.
Sioni mchina kama ataweza kuingiza hizo $m400 WHO ili kuendeleza huu ufadhili, tuache masihara baniani mbaya ila kiatu chake dawa.