Kwenye speed basi zote ni sawa hakuna mchina wala mzungu tofauti ni vitu technical ya kumpa unafuu dereva abiria na mmiliki.
Tofauti ya mchina na mzungu kwenye basi ni mfumo wa Suspension system (mchina anatumia leaf spring na Europe wao ni airbag suspension)
Gari za kichina kwenye engine wanatumia bado sio electronic controlled zina mechanical pump, wakati Scania wapo na Electric pump. Na Scania engine saizi wapo kwenye Euro 5,6 Emission Standard wakati mchina ni Euro 2,3 standards. Kwenye gear shifting Tofauti ni Europe gear ni very soft na kwenye automatic kama Scania ina opticruise (10 speed gearbox) mchina hata Higer Bus ambazo kaweka auto ni ile gearbox ya kawaida Ukiweka D,R,P haina manoeuvre ya kuruka gear au kuzipangua kwa emergency.
Kwenye retarder, hapa tofauti ni kubwa sana. Kwenye gari za mchina zinazoingia nchini kwetu retarder ni option kuna basi zinakuja na retarder na nyingine hazina.
Mchina anatumia Eddy Current Retarder kwenye basi zake na hii ndio chanzo cha ajali nyingi sehemu zenye mvua au maji maji yakigusa sehemu ya retarder na madereva wengi baada ya kutoka mfumo engine brake(stopper) wao wanajiachia wanajua retarder ndio kila kitu.
Gari za ulaya wanatumia hydraulic retarder wakina Volvo,Benz,Scania hii inakupa ufanisi hasa na kupunguza matumizi ya brake ya mguuni. Kwa madereva wazuri hii inampa maisha marefu ya brake pass,shoes na akiwa speed ndogo au anapotaka kusimama haraka akitumia unaona uharaka wa gari kupungua speed.
Kuhusu muonekano wa Body kila mtengenezaji ana design yake nzuri ya kuvutia mtu yeyote.