China yatuma ndege 38 za kijeshi mpakani mwa Taiwan

China yatuma ndege 38 za kijeshi mpakani mwa Taiwan

[emoji38][emoji38][emoji38]
Kama unategemea kwamba US ata wage a totally war na UCHINA kisa Taiwan unakosea sana yaan
Kubwa jamaa akianza kula kipigo hapo tutaanza kusikia kuhusiana na sanctions no more yaan
Hicho kitendo cha jana cjui juzi kilikua tangazo rasmi la vita yaan
Kuona vita yajumla ya UCHINA na US kwamgongo wa TAIWAN bado sana yaan na TAIWAN nisuala la muda tu itakua sehem ya UCHINA
Bro hawa pro America wanachekesha Sana 🤣🤣
 
Hata Ukraine jimbo la luhansk na donestk marekan anatoa sapot ya kila aina na bado ngoma ngumu kutegemea msaada hakuwez dhamin usalama wako unatakiwa uwezo binafs msaada iwe ziada tu
Asante sana.

Marekani kwenye maneno anakupamba atakusaidia kikamilifu ila mwenye nguvu akikuvamia usitegemee Amerika akusaidie moja kwa moja labda kwenye vikwazo uchwara na kukuuzia silaha nyepesinyepesi
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
Kama unategemea kwamba US ata wage a totally war na UCHINA kisa Taiwan unakosea sana yaan
Kubwa jamaa akianza kula kipigo hapo tutaanza kusikia kuhusiana na sanctions no more yaan
Hicho kitendo cha jana cjui juzi kilikua tangazo rasmi la vita yaan
Kuona vita yajumla ya UCHINA na US kwamgongo wa TAIWAN bado sana yaan na TAIWAN nisuala la muda tu itakua sehem ya UCHINA
Ndicho tutakachokishuhudia kwa Taiwan endapo China alikamilisha hesabu zake
 
Siyo rahisi tena kwa china kuichukuwa taiwan na kuwa sehemu yake patawaka moto hapo asia maana marekani yuko upande wa taiwan na ana maslahi yake ya kijeshi
Kwan marekani hakua na maslahi US
 
China atumie njia aliyotumia Putin kuikamata Crimea, lakini hizi za kupeleka ndege ndani ya Taiwan italeta taharuki sana na sio njia yenye manufaa zaidi, itakuwa na hasara zaidi japo watafanikisha...

Watengeneze waasi wanaoikataa Taiwan, then Taiwan ikitumia nguvu, China iingilie kati, waasi wapewe vifaa vyote vya kivita kimya kimya, pia China iingize special force commandos kama Russia ilivyofanya Crimea...

Russia kwenye intelejensia ni mwisho wa reli, raisi tu mwenyewe ni former KGB...
 
China atumie njia aliyotumia Putin kuikamata Crimea, lakini hizi za kupeleka ndege ndani ya Taiwan italeta taharuki sana na sio njia yenye manufaa zaidi, itakuwa na hasara zaidi japo watafanikisha...

Watengeneze waasi wanaoikataa Taiwan, then Taiwan ikitumia nguvu, China iingilie kati, waasi wapewe vifaa vyote vya kivita kimya kimya, pia China iingize special force commandos kama Russia ilivyofanya Crimea...

Russia kwenye intelejensia ni mwisho wa reli, raisi tu mwenyewe ni former KGB...
tunawapa muda MKUU kote kutafikia huku TAIWAN haiwezi kutenganishwa na UCHINA yaani
 
Shida hao watu wenu wakianza kupigika mtasema marekani inavamia nchi za watu
 
Wenye hela zao wanajambajamba sembuse sisi???

“We’re all worried, very much, by a looming Cold War,” UAE presidential diplomatic adviser Anwar Gargash said Saturday at a conference in the capital, Abu Dhabi. “That is bad news for all of us because the idea of choosing is problematic in the international system, and I think this is not going to be an easy ride.”
 
Taiwan’s Foreign Minister Joseph Wu on Monday said Taiwan was preparing for conflict and would “fight to the end” if China was to attack its neighbour.

“I’m sure that if China is going to launch an attack against Taiwan,” he told the ABC. “I think they are going to suffer tremendously as well.”
 

Taiwan inasema imeshuhudia ndege 38 zikiingia kwenye eneo lake la ulinzi​

2 Oktoba 2021
A Chinese J-16 fighter jet. File photo

Uvamizi huo wa Ijumaa uluihusisha ndege za kivita aina ya jet J-16 jets (kama zinavyoonekana kwenye picha hii ya maktaba), Taiwan imesema

Taiwan imeripoti kuwa ndege za kijeshi za Uchina 38 zimepaa na kuingia eneo lake la ulinzi la anga siku ya Ijumaa- ukiwa ni uvamizi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Beijing hadi leo.
Wizara ya ulinzi ilisema kuwa ndege hizo, ikiwa ni pamoja na zana zenye uwezo wa kulipua mabomu, ziliingia katika eneo hilo kwa awamu mbili.
Taiwan ilijibu kwa kuzuwia haraka uvamizi huo kwa jeti zake na kutuma mifumo yake ya makombora angani.
China inaiona Taiwan yenye demokrasia kama jimbo lililojitenga, lakini Taiwan inajiona kama taifa huru.

Taiwan imekuwa ikilalamika kwa zaidi ya mwaka mmoja juu ya harakati za kijeshi za mara kwa mara za vikosi vya anga vya China karibu na kisiwa hicho.
"China imekuwa ikifanya uchokozi wa kijeshi, na kuharibu amani ya eneo ," Waziri mkuu wa Taiwan Premier Su Tseng-chang aliwaambia waandishi Jumamosi.
Serikali ya Beijing - ambayo inaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamuhuri ya watu wa China- hadi sasa haijatoa kauli yoyote kuhusu tukio hilo.
Lakini awali ilisema kwamba safari kama hizo za anga zilikuwa ni za kulinda nchi na pia yalilenga "njama "baina ya Taiwan na Marekani.
Katika taarifa yake, wizara ya ulinzi ya Taiwani ilisema kuwa ndege 25 za kikosi cha jeshi la People's Liberation Army (PLA) ziliingia katika eneo la kusini -magharibi kama sehemu ya vikosi vya ulinzi ya utambuzi wa eneo (ADIZ) wakati wa saa za mchana, na kupaa karibu na visiwa vya Pratas.
Eneo la utambuzi wa kijeshi ni eneo lililoko nje ya eneo la nchi na ni eneo la anga la kimataifa - lakini ni eneo ambalo ndege ya kigeni bado inatambuliwa, kufuatiliwa, na kudhibitiwa kwa maslahi ya usalama wa taifa.
Ni eneo linalojitangaza na kiufundi linasalia kuwa eno huru la anga la kimataifa.
hii ilifuatiwa na wimbi la pili la ndege 13 za China katika eneo hilo hilo Ijumaa jioni. Zilipaa juu ya maji kati ya Taiwan na Ufilipino
Presentational grey line

Wizara ilisema kuwa ndege ya Kichina zilikuwa pamoja na zana za mabomu nne aina ya H-6 , ambazo zina uwezo wa kufanya mashambulio ya silaha za nyuklia, pamoja na ndege ya kuzuwia mashambulio yanayotoka kwenye manuari za kijeshi.
Mara kwa mara Beijing hufanya uvamizi wa aina hiyo kuelezea kutofurahishwa kwake na kauli zilizotolewa na Taiwan.
Haijafahamika nini kilichopsababisha uvamizi wa hivi karibuni

Maelezo zaidi juu ya mzozo baina ya Taiwan na China​

  • Kwanini China na Taiwan zna uhusiano mbaya? China na Taiwan ziligawanyika tangu vilipotokea vita vya wenyewe kwa wanyewe katika miaka ya 1940, lakini Beijing inasisitiza kuwa kisiwa hicho kitarejeshwa kwake wakati mmoja, kwa nguvu iwapo itakuwa lazima.
  • Taiwan inatawaliwa vipi? Kisiwa hicho kina katiba yake, viongozi waliochaguliwa kidemokrasia, na takriban wanajeshi 300,000 na vikosi vya usalama.
  • Nani anaitambua Taiwan? Ni nchi chache tu zinazoitambua Taiwan. Wengi wanaitambua serikali ya Beijing badala yake. Marekani haina uhusiano rasmi na Taiwan lakini ina sheria inayoipasa kuipatia uwezo wa kujilinda
Yapi maoni yako?
Dah asee humu ndani watu wanachekesha sana.
Eti China haina nguvu ya kuichukua Taiwan.
Wengine wanakwambia Hong Kong imeporomoka kiuchumi kisa udikteta wa Jin Ping.
1)China kwa sasa ni taifa lenye nguvu kuliko watu wanavyofikiria.Kuna makala imewahi kuzungumziwa ya (Coming war in China with USA),ilizungumziwa na BBC pamoja na Aljazeera.USA zaidi ya miaka 60 amekua akijaribu kutengeneza washirika watakaomsaidia endapo atapigana na China na bado wamepiga mahesabu wameona bado hawana uhakika wa kuiangusha China wanahitaji washirika zaidi.
Kitaften kisiwa kinaitwa marshall islands kuna nukes USA imehifadhi pale kwaajili ya vita itakayotokea km endapo itatokea baina ya China na USA.
Rudini miaka ya 1950s China ilipoisaidia North Korea dhidi ya South Korea USA alivyoaibika mpk kutaka reconciliation baada ya kuona vita inamuelemea yeye na mshirika wake South korea.
Rudini hapo hapo kuna confrontation ya Jangsari ambapo wakorea kusini wengi walikufa na navy seal wengi wa USA kufa North korea ilisaidiwa kisilaha na kijeshi na China.
MSIICHUKULIE CHINA MANDEZI NYIE WATU.
SOMENI DOCUMENTARIES MFAHAMU.
Hiyo Taiwan China ikiamua ndani ya sekunde inadakwa.
Halafu kuna mtu anasema washirika wa China hawana nguvu.
Iran kila siku anamchezesha sindima USA pale middle east.
Russia unapozungumzia mataifa yenye nguvu hapa ulimwenguni hukosi kulitaja.
2)Hong Kong imeanguka kiuchumi baada ya China kuhamisha nguvu zake za uzalishaji Macau.
Sasa hivi Macau ndipo ilipo nguvu ya uzalishaji ya China.
Asa hv wanaelemewa Hong Kong matatizo kibao yanawakuta.Na siku China ikikata uzalishaji wa kila kitu huko HK ndio wataelewa kuwa nazi haiwezi shindana na jiwe.

CHINA IS THE UPCOMING SUPER POWER IFUATILIENI VIZURI ACHENI USHABIKI MAANDAZI.
 
Hakuna nchi hapo itakubali kuingizwa kwenye mgogoro wa moja kwa moja na China kisa Taiwan, unafikiri wao hawajui madhara watakayoyapata?
Japan, SK n.k hawawezi nunua vita sio ya kwao usijidanganye mkuu..., tena Japan ndio kabisaaa hana huo muda na hataki vita...

Marekani ana base ngapi middle east? kwa nini hawakuzitumia hizo base kujibu mashambulizi walioahidi baada ya Iran kupiga zile kambi zao 2 Iraq?
hakuna nchi yeyote ingetaka kununua vita na Iran, yaani nchi yako iwe ndio uwanja wa vita, yeye kwake wanakula raha... kwa accuracy ya zile kombora za Iran, endapo Saudia angeingilia kati, basi Iran angepiga sehemu yeyote ile aitakayo, hata Israel mwenyewe aliufyata... tusiongelee ushabiki ndugu zangu...
wewe ndiyo ungelikuwa Rais wa marekani ungeliingiza nchi vitani kisa Drone 1 imetunguliwa?.
Ikiwa jibu ni ndiyo basi hupaswi hata kuwa kiongozi wa familia yako.

then wakati unaona Drone ni kitu cha thamani sana fikira black hawks ngapi na ma-Hamvee Us kayaacha fghanistan wakati anaondoka..
mzigo uliachwa Afghanistan jeshi letu hatuna na wameyaacha kwa wajahidina, sasa hivi wanajifunza kuyarusha.
 
Hao wavimba macho hawawezi kupambana na wazungu hata siku moja watachakazwa vibaya na hata wenyewe wanalijua hilo.

Pia kuna maelfu ya wanajeshi wa Marekani nchini Taiwan ambao wanasubiri China arushe hata manati akione kilichomnyoa kanga manyoya.
 
Bila kusahau wale majirani aliowapora visiwa na sehemu ya bahari,hawa wanasubiri China aivamie Taiwan na wao wakinukishe sababu wataona akimalizana na Taiwan atawafuata wao.
Hizo ni ndoto tu.
Kama walishindwa kutetea visiwa vyao viliponyakuliwa ndio wataweza kumtetea mwenzao kisa kavamiwa?
Acheni ushabiki maandazi ninyi!!
 
Hao wavimba macho hawawezi kupambana na wazungu hata siku moja watachakazwa vibaya na hata wenyewe wanalijua hilo.

Pia kuna maelfu ya wanajeshi wa Marekani nchini Taiwan ambao wanasubiri China arushe hata manati akione kilichomnyoa kanga manyoya.
China imechukua baadhi ya kilometa za maji za ufilipino na hiyo Taiwan yenyewe na kubeba visiwa juu.
USA ilifanya nini?
Rudi vita ya mgawanyo ya Korea USA kilimkuta nn alipojishaua kumsaidia South korea kurudisha Jangsari?
 
Back
Top Bottom