Kwani mafundisho tofauti ya ukristo,uislam WA Africa na WA ulaya na uarabuni,maandiko na yale yale hapa shida ni mtazamo mfano mwafrika anaenda ibadani ili apate kazi,mke au mme mzungu anaenda kanisani ili aende mbinguni.
Umekariri tu brother, asilimia kubwa ya wazungu wa leo hawamini tena kuhusu mbinguni, na wala hawana mpango wa kutaka kwenda mbinguni.
Wengi wanaona kuwa kilichomo katika biblia ni history tu kama zilivyo story zingine, yani hakina ukweli wowote, ni watu tu wameutengeneza uongo na kuupamba vizuri ili uvutie watu na kuupenda, ndo maana unakuta asilimia kubwa ya wazungu haswa vijana, hawaenda tena kanisani.
Unakuta mzungu siku ya J2 badala ya kwenda kanisani yeye anakwenda zake Park, Beach, Shopping nk, tena na familia yake. Ni wachache mno ambao bado wanawaza swala la mbinguni. Uliza mtu yoyote anaeishi katika nchi zenye wazungu wengi atakwambia.
Ni afrika tu ndo bado asilimia kubwa ya wakristo wanakwenda kanisani, ndo bado watu wanauziwa ticket za kwenda mbinguni, watu wanalipa hela ili wafanyiwe miujiza ya kupata kazi, wafanyiwe miujiza ya kwenda Marekani bila kuwa na visa wala ticket ya ndege 😄😂😂
Ukienda Saudi Arabia sidhani kama utakuta watu wamefunga mtaa mzima kwa ajili ya kufanya maulid, sidhani kama utakuta watu wanalipuana kama Somalia, Mali au Nigeria kisa dini. Wao wasaudi washaona ni ujinga mtupu kuendekeza itikadi za kuchinjana kwa sababu ya dini, huku uchumi wa nchi ukiporomoka kutoka na nchi kuwa katika hali ya tahadhari ya vita.
Hivyo upuuzi huo unafanywa na nchi zilizo nje ya Saudia haswa Africa.
Ukristo na uislam umeenezwa na wafuaasi wa Yesu na Muhammad,hakuna serikali iliyoeneza dini maana dini ni suala binafsi la mtu na sio serikali.
Si kwamba China hakuna misikiti na makanisa yapo tele.
Hata huo ubudha ni kwa wachache.
Ni kweli ukristo na uislam umeenezwa na wafuasi wa hao majemedari wawili, lakini ukute lengo lilikuwa kutafufa watu wa kuwaweka mtegoni kwa masilahi ya wajanja wengine.
Wazungu, waafrika na race zingine duniani tumeaminishwa kuhusu Yesu kuzaliwa na kufia huko uyahudini Israel, na sisi tumekubali bila kuona au kushuhudia kuwa alikuwepo kweli au.
Lakini wayahudi wenyewe tunaoambiwa ndio lilikuwa kabila au dini ya asili ya Yesu wanakataa kuwa kwao hakujawahi kuzaliwa huyo Yesu katika nchi hiyo. Wanatutaka kuwa makini na uongo huo, lakini ndo hivyo waafrika tumeshanasa mtegoni, hatuna ujanja wa kujitegua.
Ni kama leo mtu aende kuwambia watu kuwa umepata mgeni nyumbani kwako, wakati wewe huyo mgeni haujamuona na wala haumjui, yani unalala na kuamka peke yako.
Kwa upande wa Mwamedi tunaambiwa kwao kwenyewe alipozaliwa hawakukubaliana nae kama ni mtume, alafu mtu anataka mimi mpogoro au mmwela nikubali tu kichwa kichwa kuhusu utume wake.