Hapa hatuzungumzii mabomu ya nyuklia, tunazungumzia matumizi ya amani ya nyuklia yaani kuzalisha nishati.
Kiteknolojia Marekani iko nyuma ya China kwa miaka 10 hadi 15 katika nishati ya nyuklia kwa sasa.
Kwa nini?
China wamekuja na teknolojia mpya (innovation) ya kwanza duniani iitwayo Fourth-Generation Nuclear Reactors. Vinu hivi vinatumia gesi kupoozea badala ya maji yenye presha kama ilivyo kwa generations zilizopita.
View attachment 3019306
Generation IV
Generation IV reactors include gas-cooled fast reactors (GFR), lead-cooled fast reactors (LFR), molten salt reactors (MSR), sodium-cooled fast reactors (SFR), supercritical-water-cooled reactors (SCWR), and very high-temperature reactors (VHTR).
Teknolojia hii imekuwa suluhusho la tatizo la muda mrefu la ukosefu wa usalama katika vinu vingi vya nyuklia duniani.
Faida zingine za Generation 4 Nuclear Reactor:
Kinu cha kwanza duniani cha Generation 4, Shidao Bay High kilizinduliwa huko China Dec 06, 2023. High Temperature Gas-cooled Reactor (HTGR)
View attachment 3019316
Hivi sasa China inaendesha vinu 55 vya nyuklia, ikiwa ni pamoja na hiko cha Shidao Bay-High, na vinu 27 vya ziada vinajengwa kwa wakati mmoja.
Hii inaiweka China katika mstari wa mbele katika upanuzi wa nishati ya nyuklia, kupita mataifa mengine katika miradi inayoendelea ya ujenzi wa vinu vya nyuklia
Kwa wastani kinu cha nyuklia nchini China kinachukua muda mfupi ili kianze rasmi kuzalisha nishati - kwa kasi zaidi kuliko nchi zingine nyingi.
Marekani imejenga vinu viwili pekee katika miaka 10 iliyopita, ambavyo vyote vilitumia miaka mingi na mabilioni ya dola ya bajeti.
CREDIT: US falling far behind China in nuclear power, report says