The best_of _me
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 242
- 486
Hakuna nchi ambayo haiwezi kufanya innovation, maendeleo ya teknolojia yanategemeana sana, ndo maana nchi kama china unakuta na wao wameiga halafu baadae wakaendeleza na kubuni vya kwao.Mshamba ni ambaye hawezi kufanya innovation, kwa maoni yangu
Nchi nyingi za Asia zilijikita kwenye kuzalisha Nguvukazi yenye ujuzi kitu ambacho kilivutia Kampuni nyingi kutoka nchi zilizoendelea kwenda kufanya uzalishaji katika nchi kutokana na nguvu kazi yenye juu na maarifa lakini ambayo ilikuwa na gharama nafuu ukilinganisha na nchi zilizoendelea.
Hali hiyo ilizisaidia hizo nchi kupata teknlojia kirahisi sana. Ndo maana kwa sasa bidhaa nyingi husasan za gharama za kati ni made in China, Bangladesh, Thailand, Pakstan n.k
Nchi nyingi za Africa hususan kusini mwa jangwa la sahara hazijaweza kuvutia mitaji kutoka nchi zilizoendelea kutoka na kuwa na nguvukazi isiyo na ujuzi unaohitajika, miundo mbinu mibovu, kukosekana nishati ya kutosha na ya uhakika n.k. Ndo maana unaziona kwamba hazina ubunifu, kwa upande wangu naona hiyo ndo shida.
Nchi yenye umeme wa kuungaunga na miundombinu mibovu hususan barabara, reli n.k kama Tz haiwezi kuwa na ubunifu ambao ni endelevu kwa sababu hakuna nyenzo za kuuendeleza.