Chini ya uongozi wa Rais Samia viwango vya furaha kwa Watanzania vyaongezeka mitaani

Huyo mamako huku kanda ya kati wakulima wa alizet hatuna hamu naye, ameshindwa kulinda viwanda vidogovidogo vya ndani karuhusu mafisadi kuingiza mafuta kutoka nje matokeo yake bei imeanguka vby
Alizeti zenu pekee haziwezi kutosheleza Mahitaji ya mafuta hapa nchini ndio maana serikali inatoa kibali Cha uagizaji wa mafuta nje ya nchi ili kuziba pengo, tukifikia hatua ya kujitosheleza kwa uzalishaji wa ndani tu na kukidhi Mahitaji bila Shaka serikali yetu itapitia upya Sheria na Sera zetu za kikodi na ushuru ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa ndani,lakini serikali yetu imizuia wakati uwezo wetu wa kukidhi Mahitaji ni mdogo tutajikuta Bei inapata juu Kama mwanga,mama yetu yupo Nasi na anatujali Sana watanzania na wakulima kwa ujumla
 
Nilishangaa vp huko porini hujaona speech ya mama?? hatimae umekuja.
Mimi nipo mkuu na ninaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia mzalendo wa kweli na aliyejitoa na kujitolea kulitumikia Taifa letu
 
Wewe usitafute Pesa kaa shabikia siasa mwisho wa siku utavuna ulichopanda. Siasa ni ujasiria Mali siasa ya kweli ni kupambana kutafuta Pesa Kijana.

Unasema udikteta kwani huyo dikteta Alikuzuia usilale na mkewako? Au Alikuzuia usiende chooni? Wacha ujinga Uhuru usio na mipaka ni ukichaatu.
 
mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
shukuru Mungu kama unapata mkate wa kila siku,
leo i met mvulana wa miaka btn 24-27 amevaa smart, travota, koti la suti but sijui alivyonitazama akapata tumaini na kuja kuniomba Buku imsaidie kwenye Daladala kwenda Tabata, anadai amemaliza Agro ecomic SUA kama miaka miwili na yupo tu home, aifanikiwa kupata mkopo lkn ndo hivyo ajira hakuna!!

alopoomba nauli siku na pesa ndogo nilichofanya baada ya kumdadisi na kuona its true ni mtu amesoma nikajipa moyo na kwenda nae hs restraunt tukapiga tea baadae nikamuacha na 5k....

ninachotaka kusema ni kwamba mtaani hali ni mbaya sana, watu hawana pesa, bidhaa zimepanda sana, kuna kaya wanashindia mlo mmoja.......kama taifa tunatakiwa kuangalia khs hilo!!!
 
 
Unafurahia Mchele kutoka 1,500 mpaka 3,000 na unga wa ugali kutoka 800 mpaka 1,700 haujui kuwa hii mfumuko wa Bei wa asilimia 100.
 
 
Mtoto wa kambo wa Mama Samia.
CCM choir ( kwaya kuu Lumumba )
 
Furaha hiyo ndio imepelekea nchi kuwa Tulivu,yenye amani na usalama wa kutosha,Hii ndio imepelekea umoja wa kitaifa kuimarika Sana wakati huu,furaha hii ndio imepelekea watanzania kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za ujenzi wa Taifa let
 
Mda mwingine huwa najiuliza mnalipwa sh ngp kwa mapambio haya? Mama ana mazuri yake Ila kwenye ishu za kiuchumi kachemka vby, maisha magumu mno mtaani hela Haina thamani, kila kitu Bei juu, Hadi mahitaji ya kila siku mfano sabuni, maharage, mchele, unga nk....
Watumishi waliongezewa kiasi kidogo mno tofauti na ahadi lakini hata kile kidogo kimefuatwa kwa njia ya indirect maana baada ya nyongeza Bei ya kila kitu kilipaa, anyway hatuna pa kwenda hatuna Cha kufanya
 
Bado naunga hoja ya "mwaka huu ufutwe tuanze upya"
 
Umetumia kipimo gani kupima furaha?Nadhani tuanzie hapo.Usikubali kupigia mwingi wana siasa mkuu,huo ni utumwa.
 
Hali ya uchumi chini ya uongozi wa Rais wetu Ni nzuri Sana,Hali ya biashara na shughuli nyinginezo za kiuchumi Ni zenye Afya Sana ,Ndio maana unaona hata makusanyo yameongezeka na kufikia Trioni mbili kwa Mwezi
 
Mimi Ni mkulima na kilimo ndio ajira yangu kuu ya kujipatia kipato Cha kuendeshea maisha yangu na mambo mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…