Chini ya uongozi wa Rais Samia viwango vya furaha kwa Watanzania vyaongezeka mitaani

Tanzania ya leo sio kama ya zamani Tanzania ya Rais Samia Suluhu kuna fursa kila kona
 
Kabisa mpaka UFIPA Wana raha yaani Rais Samia kaja kuweka mambo sawa
 
Mtu mzima kuwa chawa ni upunguani ulioje.
 
Mkuu ushauri wangu kwako usiweke namba 1 tu ya simu,zipangilie zote hapo juu uonekane upo serious na jambo lako,wale jamaa wakipiga mara moja hupatikani ndio basi hawarudii tena nakwambia.
 
Maoni Mazuri.
Lakini Mtaani watu vichwa chini. Lo
 
Kuna wakati huwa nawaza sana juu ya huyu Mungu. Yaani anawaskiliza sana watanzania. Iko hivi: Baada ya JK kumaliza muda wake, niliwasikia wa-tz wengi wanalaumu sana, na kusema "huyu raisi gani anachekacheka tu. Nchi ilipofikia tunahitaji raisi dicteta" naamini Mungu alijibu. Akaja mtu yule. Jamani. Ingawa mzee Makamba alituonya kuwa "mnaenda kubatizwa kwa moto" sijui kama naye alibatizwa kwa moto maana kauli yake ile ya WATU WEMA HAWAFI sikuielewa. Baadaye mateso yalipozidi kwa baadhi ya wa-tz, walianza kuomba tena na walitumia mstari huu wa ZABURI 109:8-9 unaosema "siku zake na ziwe chache, usimamizi wake na atwae mtu mwingine, wanawe na wawe yatima na mkewe na awe mjane". Sijui kama Mungu alijibu ama laa. Ila usimamizi akapewa mtu mwingine. Sasa huyu naona anajitahidi sana kuwaunganisha watanganyika, ingawa kazi kubwa anayo. Ila kweli ni mtu mwema kwa nionavyo mimi. Huenda akaandika historia kwa kuleta katiba mpya.
 
Mke mwema lazima amsifie mumewe kwamba ni bonge la HB hata kama ana kengeza.
 
Hata redio msoga ilitangaza habari kama hizi wakati wa mkesha wa mwaka mpya
 
Watanzania siyo kwamba wanafuraha! Ila wamekufa ganzi! Hawajui linalo endelea, hivyo hawawezi kufurahia au kuhoji kitu chochote wamepigwa (wamekufa) ganzi.
Hebu nikuulize
Je unajua SGR imejengwa mpaka wapi na kwa asilimia ngapi?
Je daraja la Busisi limejengwa? Limefikia wapi (%l Na je litamalizika lini? Je! Bandari ya Bagamoyo inatekelezwa? etc. Watanzania hatuna habari na maendeleo yanayo tokea nchini - tumekufa ganzi. Hakuna kitu unacho ambiwa kinacho kuhusu.
Habari iunayoijua ni umbari wa diamita ya kilometer 2 tu - dukani. Hushirikishwi popote.
Awamu iliyopita ngazi yoyote ya miradi ya maendeleo ulikuwa unataarifiwa - kupitia njia nyingi. Sasa hivi ukienda shell unachukia! Ukienda dukani unafura etc. Dr Samia inabidi ajitahidi zaidi.
 
Bei ya mbolea haikupandishwa na Rais Samia na serikali yake, Bali Ni mfumuko wa Bei katika soko la Dunia,Ndio maana mama Yetu Rais Samia akaamua abebe mzigo huo wa kutoa mabillioni ya Ruzuku ili kuwapunguzia maumivu wakulima
Si kweli.Wafanyi biashara hawajadhibitiwa ipasavyo kwa hiyo wanatumia loophole ya upuuzi mwingi uliopo duniani sasa hivi Kama wa Ukraine kupandisha bei kiholela,we know it.Hata kwenye mafuta upuuzi huu unaendelea.TPDC ndio waliokuwa wameomba tender ya kuagiza mafuta lakini wakanyimwa wakanyimwa wakapewa watu binafsi kwa ajili ya rushwa.TPDC waliokuwa wameahidi kuagiza mafuta at cheaper prices.

Mkuu kwa taarifa yako,Urusi wameshusha bei ya mafuta na mbolea, sasa kwa nini bado ni ghali?India na China wanapata mafuta na mbolea at a discount,why not us.
 
Jamaa anajitutumua sana na mazeri wake. Hongera kwa moyo huo. Huenda ukaonekana
 
Jamaa anajitutumua sana na mazeri wake. Hongera kwa moyo huo. Huenda ukaonekana
Huo ndiyo ukweli kuwa Watanzania wana amani sana mioyoni mwao unaochagizwa na uongozi wa Rais samia uliojaa upendo mkubwa kwa watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…