Chonde, chonde! Huenda hili ni onyo la mwisho kwako!

Chonde, chonde! Huenda hili ni onyo la mwisho kwako!

Inatia moyo sana, leo Satan ameipa 👍 mada yangu. Mungu ambariki sana. Ila hilo jina lake sijui kwanini alilichagua.
Bado akina Infropreneur na captain Kiranga aliyeniweka kwa ignore list kwa sababu ya vifungu vyangu🙂
Mungu atawagusa tu na kuwarehemu. Amina
Madam.

Mungu huyo angekuwepo kweli, Hata kusingehitajika imani ya kuamini uwepo wake.

Kila mtu angejua Mungu yupo kwa uhakika kabisa bila imani.

Na hata haya mabishano yasingekuwepo.
 
Kisasi ni haki mkuu.
Nani amekudanganya kwamba kisasi ni haki yako?
Soma Warumi 12:19
“Wapenzi, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana."
 
Maandiko yafuatayo yanaonyesha wazi nyeto ni dhambi:
1 Wakorintho 3:16-17
"Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni nyinyi wenyewe.”

Nyeto inaleta madhara mengi ya kimwili. Ni kuuharibu mwili. Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hatupaswi kuiharibu.

Wagalatia 5:19-21
"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi ufalme wa Mungu."

Nyeto ni tendo linalofanana na uasherati na uchafu

Wagalatia 5:16

"Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."

1 Petro 2:11
"Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho."

Mathayo 5:27-32
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Mara nyingi nyeto huendana na kumtamani mwanamke/mwanaume fulani

Waefeso 5:3
"Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu."

Yuda 1:7
"Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote."

Nyeto ni tendo lililo kinyume na maumbile. Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke, waishi pamoja katika ndoa. Mwanadamu hakuumbwa aishi peke yake na kujiridhisha kimwili. Ndio sababu tunaambiwa:
1 Wakorintho 7:9
"Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa."

Kipenzi Changu kwa maandiko hayo kama bado utaendelea kukumbatia nyeto basi hutaki kwenda mbinguni
Mimi sikumbatii nyeto lakini sijaona kipengele cha kukataza nyeto
 
Hivi timotheo alipoambiwa kwa sasa usitumie maji pekee bali na mvinyo kwa ajili ya tumbo lako !Paulo mtume hakumaanisha hii wine ya kupima ya Dodoma hasa ya mzabibu!!?
 
Nimekusikia na nitajitahidi kadri niwezavyo kutekeleza
Amen, Mungu akusaidie ndugu yangu.
Kwa nguvu zako peke yako huwezi lakini kwa uwezo wa Bwana, utashinda na zaidi ya kushinda
Flp 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
 
Yakobo 1:27
Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii: Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa
 
Ulokole ni upumbavu, unafiki na ujinga wa kiwango cha juu kabisa
Mkuu, dunia hii tunapita. Hakuna mtu atakayeishi milele hapa duniani. Kwa sababu hiyo ni vema kujiandaa na maisha baada ya kifo. Kifo sio mwisho wa maisha. Baada ya kifo, kama ulikuwa unaishi maisha matakatifu, utaenda peponi kwenye raha ya milele; na kama ulikuwa unaishi maisha ya dhambi, utatupwa kuzimu kwenye mateso yasiyokoma. Hizi ni habari za kweli, sio stori za kijiweni. Ndiyo sababu shetani na mapepo yake wanahangaika kuzipinga na kuwapotosha watu wasiamini.

Mpumbavu ni yule anayesema eti "hakuna Mungu"

Zaburi 53:1
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema.
 
Nakusihi kwa Jina la Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana
1. Usifanye tena uzinzi na uasherati na wala 'usipige nyeto'
2. Acha ulevi
3. Usiibe tena
4. Usirudie kusema uongo
5. Futa kabisa mawazo yako ya kulipa kisasi
6. Acha kutukana na kuwachafua wengine kwa maneno yako
7. Acha dharau, waheshimu wanaostahili heshima

TUBU! GEUKA! ACHA DHAMBI ZAKO NA UMRUDIE MUNGU!
Yaani eti WATEKAJI NA WAUAJI WA WATANGANYIKA HAWAJAKEMEWA,HUU NI WIZI WA MAOMBI.
 
Ameshakuwa sugu huyu anahitaji uponyaji!
Usiwe na shaka. Neno la Mungu lina nguvu ya kubadili maisha ya watu. Hiyo dozi (post #20) itamletea tu uponyaji.
Na mimi nitamuombea apone kabisa na awe Mwinjilisti atakayekemea hadharani dhambi ya nyeto
 
Kuna Idara nyeti sana umezitaja hapo wewe mpinga uhai (Shetani) unawaambiaje watu wasitombane unataka wasizaliane?
Uzinzi na uasherati ni mahusiano ya kimwili nje ya ndoa. Ukifunga ndoa huna hatia. Nje ya hapo ni kibano tu siku ya hukumu (Gal 5:19-21)
 
Back
Top Bottom