umesahau kitukimoja, kwamba ni raia wa Uingereza, aliukana utanzania. ila nina mawazo kwamba tz tukubaliane tu na uraia pacha kwasababu hauna madhara yeyote kwetu, wengi wanafikiri mtu akiwa na uraia pacha ataisaliti nchi au atakuwa loyal kwa nchi zingine, wanasahau kuwa hata raia wenye uraia wa nchi moja kama kina Tundu Lisu wameisaliti nchi kuliko hata wenye uraia pacha. mtu yeyote awe raia moja au raia pacha anaweza kuisaliti nchi. tujifunze nchi zingine kama rwanda, kenya, israel etc, wana uraia pacha, wamedhurika nini? zaidi sana wale walio nje wanarudi kuwekeza nchini kwao kwasababu sheria zinawalinda na wanaonekana ni raia halali. hao ni damu yetu tu, wengine wamefanya hivyo ili kupata pesa zisaidie hata hawa waliobaki huku ndugu zake, lakini moyoni yeye bado ni mtanzania. achilia mbali hao mercenaries waliojiunga jeshi la marekani, hao wamepitiliza.