Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Mwanamke akiwa na hivi vitu mume anaonekana hana maana. Huyu dada ni katika ile mifano hai inayozidi kujionyesha, na hii ji true nature ya mwanamke
 
Kwa hiyo Shusho kapata maelekezo ya kumuacha mumewe baada ya kuitwa ?.....acheni kutumia vibaya maandiko
 
Nimekwambia, yapo makubwa zaidi mbeleni.

Nitarudi kutukumbusha.

Tusubiri.
Watu wengi huwa wanashangaa kwanini watu maarufu wanawindwa sana na shetani. ukienda kwenye dunia, hata hao mafreemasons, au cult zozote zile, huwa zinapenda sana kuwachukua watu maarufu, kwasababu shetani akiwaingia impact yao kwa wanadamu inakuwa kubwa,shetani anavuna matunda mengi. mfano, diamond tu na wengine wanamuziki wa marekani, nyimbo zao zinachafua sana nafsi za watu na kufungua milango shetani kuingia kwao, na kwa watoto pia.

ukija kwa waliookoka na ni maarufu, shetani atawinda sana ndoa zao au hata maisha yao awadondoshee kwenye uzinzi au dhambi inayokera kwa macho ya kibinadamu, na anguko lao linaondoka na kundi kubwa sana la watu waliokuwa wanawafuatilia. shusho mfano, ana wafuasi wengi kwa sababu ya nyimbo zake, akifanya chochote cha ajabu mioyo ya wengi itarudi nyuma na kuona walikuwa wanafuata kisicho sahihi, na yeye atalipa garama hiyo mbele za Mungu. ukikabidhiwa uwakala wa chochote na Mungu hakikisha unakilinda kisilete negative impact kwa wanadamu.

hatutakiwi kumpiga mawe weee, ila tunatakiwa kumwombea Mungu amrehemu, na akishupaza shingo yake, yeye mwenyewe atarudi na kukiri kwamba alipotea baada ya kukutana na aliyemwita awali.
 
Uzi UFUNGWE hapa..[emoji375][emoji375][emoji375]
 
Ni Kweli tumwombee arudi Kwa mstari,

Lakini akikataa, apumzishwe Ili asiharibu zaidi.
 
Amekengeuka muda sana
 
Advice kwa vijana mna oa sasa, kama unajua mchumba wako analanyaga kwenye makanisa aina hiyo( kuacha yale regular ), moige marufuku, mpe ultimatum either achague ndoa au hilo kanisa, otherwise hilo kanisa especiall wachungaji wa kisasa, wata m brainwash to extent atakuoma wewe ndio shetani
 
Wengi hapa mahusiano yao yapo juu ya mawe[emoji28][emoji28][emoji28]

Ila kiukweli ukiwa mwanamke kama una ndoto/malengo zako ni mara chache sana kutimiza ukiwa kwa mume.
So Shusho is right atimize ndoto zake...maisha ndo haya haya
Afu tunaishi mara 1 tyuuh dear, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuwa mwili mmoja si kufanya kazi au huduma ya aina moja pamoja. Bali ni kuwa na makubaliano ya pamoja ya kuheshimu na kujali kazi au huduma ya mwenza wako kama ya kwako.

Kuwa mwili mmoja ni kusaidiana, kutiana moyo na kujenga mahusiano mema pasina kutengana. Christina angeweza kuendelea na ndoto zake, huduma yake au uchungaji wake pasina kumwacha mumewe. Mume anaweza kuwa mchungaji na mke pia, au wakawa na huduma tofauti pasina kutofautiana.

Mume anaweza kuwa askari, mke akawa muuguzi.
Mume anaweza kuwa mhandisi wa umeme, mke akawa mchungaji.
Mke anaweza kuwa mfanyabiashara, mume akawa mchungaji, nk. Kila mtu katika ndoa ana kipaji chake, fani yake, utaalamu wake, huduma yake, wito wake au ndoto zake tofauti pasina kuathiri ndoa.

Christina kakosea kwa kutojua au kwa makusudi. Au la, kuna sababu nyingine asiyoisema ya kutengana kwake na mumewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…