Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

dogo aliyezunguka naye miezi 3 kenya,amemwacha mumewe huku bongo, alishatoa sana hizo allegations kwamba alikuwa anamtaka na alivyogoma anamroga. hatusemi kuwa ya kweli, hatujui, ila mtu kama ameachana na mumewe, akipewa allegationkuwa anataka vijana wadogo nani atashindwa kuamini, mtu mwenyewe kajaa kiburi, dharau na macho juu juu vile? kwamba kweli ameshindwa kufanikiwa kwa kuinuliwa na Mungu ameamua afanikiwe kwa kuinuliwa na kick za kuwa na diamond, anataka diamond ampe umaarufu badala ya Mungu ndio ampe umaarufu? kwani yule dadangu wa mbeya aliyeimba wimbo na hamonize ameishia wapi? hamonize ameshaokoka? au ndio vitimbwi vilizidi na Jina la BWana likazidi kutukanwa? watu wanatafuta kufanikiwa kwa njia ya kimwili badala ya kufuata njia za rohoni. Mungu awasaidie.
kwa kuwa yule alimpata harmo na huyu naye akaamua ampate mond, wanajimaliza wenyewe hawa waimba injili tuliozipenda nyimbo zao sasa hatuna hamu nazo, tunawaona ni wahuni tu
 
Alivyotangaza habari za ufufuo wa Yesu...

Tena alikuwa na macho ya Rohoni...

Maana hata hao mitume wengine hawakuwa na macho ya Rohoni, ni Petro tu alimjua kuwa Yesu ni nani...

Mariam Magdalene mwanamke ambaye alikuwa wa kwanza kutanganza injili ya ufufuo wa Yesu...
Hapa Nabii Isaya hakumjua Yesu hata kabla hajaja dunian?

ISAYA 9:6-7.
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.
[7]Maongeo ya enzi yake na amani
Hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;
Kuuthibitisha na kuutegemeza
Kwa hukumu na kwa haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

Endelea kuenenda kinyume na Maandiko Matakatifu "Biblia".

YOHANA 22:18-19.
 
Mtu wa Mungu akianguka, tumuombee na sio kumsema vibaya...

Mungu atusaidie.
Tunamuonya ili asipotoshe kondoo wa Mungu.

2 TIMOTHEO 3:16-17.
[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
[17]ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
 
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
Yupo sahihi, naungana na maoini yako pia.
Ila hawa waimbaji wa injili wanaongoza kwenye kataa ndoa.
 
Ndoa ilihasisiwa na Mungu, acha Ku promote udangaji! Ndoa ya, kikristo inavunjika mpaka mmoja afe,Ila kuolewa sio lazima, Ila, kwa, hawa dada zetu,kinachowavutia ni udangaji tu na tamaa, wakimuona Zuchu anavyofaidi kwenye ufuska,wanajiuliza kwanini wao wafungwe na ndoa
....... wakati nao wana mbususu?
 
ni mpuuzi tu yule mwanamke, aliingiza siasa kwenye ndoa yake
Nikuambie sisi me ama wewe na mimi ndio wapuuzi. Mwanamke Hana huruma pindi anapokuwa kwenye maslahi yao. Yaani wao ni high stake traders na Wana trade market ambayo Ni volatile. Me unaingia kwenye relationship kisa ya sex, family, watt na kuitwa baba , wao wanawaza kuishi maisha mazuri, pesa, jina, tittle, umaarufu na Wala Hawana jingine.
Mwanamke ana trade low value kwa high value from men

1-Yeye umri mdogo anataka mwenye umri mkubwa ili aweze kuku manipulate ndani kuwa wewe Ni mkubwa pambana.

2- kipato Chaka kidogo ama zero Ila
anataka uwe na kipato Cha kuanzia hata 3M and above ili awe na uhakika.

3-elimu yake ndogo anataka uwe na elimu kumzidi, imagine mtu ni Engineer or dokta Ila anaoa la Saba. Sasa tafuta wanawake wenye iyo elimu halafu waume zao la Saba otherwise awe na cash mbaya.

4- Koo ya mwanamke ni masikini Ila anataka aoelewe na Koo yenye pesa, jina , yenye viongozi. Ulizia ni ke gani asiyependa kuolewa na Koo ya kiongozi fulani nchini.
5- mengine wataongezea wadau Ila kikubwa tungekuwa na akili ambayo mwanamke anayo katika mahusiano. Ke wengi mno wasingeolewa.

Ngoja nikuache na kibwagizo hapa chini.
Hypergamy is baked into the female brain. It works ruthlessly and swiftly. If she sees a better option, she won't hesitate to jump from her current branch to a higher branch,
ni mpuuzi tu yule mwanamke, aliingiza siasa kwenye ndoa yake
 
Bila akili, nguvu, busara, juhudi na mali za mume wake (Pastor Shusho) huenda leo hii hakuna mtu angekuwa anamjua Shusho kwa level ile ya umaarufu wa kuimba. Kwa sasa Christina Shusho ameamua kuizamisha boti (ndoa) iliyombeba kumsafirisha katika bahari yenye mawimbi mengi akiamini boya (umaarufu) litamsaidia kusafiri mbali.

Muda ni mwalimu mzuri sana.
Tusubiri zaidi.
Nothing lasts forever than the God's word.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Hata Lwakatare aliasi ndoa lakini alikuwa anafungisha ndoa na alikuwa akiwaasa wanawake kutulia kwenye ndoa zao na walikuwa wanamuelewa bila tatizo. The same case applies to Shusho na maisha yanaendelea.
ila inaleta utata fulani hivi, hata hivyo mama huyo alikuwa na utata kanisani kwake, itoshe tu kumuona kama alikuwa mtimilifu
 
misalaba ni alama za mashetani ndo maana hata masonic wanazitumia na wasanii wanazitumia piah huwa nashangaa kuyaona makanisan...........watu wengi hushindwa kutofautisha msalaba (kama kifaa cha mateso kilichotumika kusulubu) ...na neno la msalaba.........ila itabid niudhurie hapo kwa shusho siku 1 nikajionee live bila chenga kama kwel kuna mambo mazur hvo ya vimino
kumbuka kuwa kuna aina mbalimbali za misalaba ikiwemo hiyo ya masonic. Nenda makaburini utaiona ilivyo na maumbo ya ajabuajabu na ndugu za marehemu hawajui kuwa kuna misalaba ya mason wanaweka tu ili mradi ni msalaba
 
Njaa mbaya sana, kwahio aliolewa ili ajiondoe kwenye umasikini. Sahizi kapata umaarufu zaidi na vichenchi kaona amtupe mwamba. Wanawake wanafiki sana aisee!
Sasa angepata vipi pa kuishi na Kongo vita?? Ndio umuhimu wa kuwa KE huo. Ss hivi simba la masimba amemfungulia dunia kuwa unachotaka amgande babu wa nini?? 🤣🤣🤣🤣

Lakini na nyie mwanaume mwenzenu si kamtumia jamani 😜
Ukute hata usiku alikuwa anamuamsha ampe mbuzi kagoma 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Maono yalikuja akiwa tayari kwenye ndoa mkuu. Mwacheni ayatimize.
huo ni uharibifu, tusichukulie poa, wanawake wengi watatoka kwenye ndoa kwa staili hii kuwa wamepata maono na wanatoka kwenye ndoa kwenda kutumikia maono yao nje ya ndoa
 
Back
Top Bottom